ANDALIO LA SOMO

Andalio la somo ni utaratibu au mpangilio wa hatua za kufundishia unaotayarishwa na mwalimu kwa kipindi husika na kwa darasa fulani. Siku zote Andalio la Somo ndio dira ya kumuongoza mwalimu wakati wa kufundisha kwake. UMUHIMU WA ANDALIO LA SOMO Huonesha wazi malemgo ambayo mwalimu anatarajia yafikiwe na mwanafunzi wake katika kipindi Ni muongozo wa kufuata hatua kwa hatua mwalimu anapofundisha darasani Humuonesha mwalimu sehemu za somo za kuuliza maswali, kutumia zana au kuhusisha wanafunzi katika vitendo. SIFA ZA MALENGO MAHSUSI YA SOMO A) Kipindi kimoja lazima kisiwe na malengo mengi Kila lengo kuu liandikwe kwa mtindo unaoonesha jambo watakaloweza kufanya wanafunzi na linaweza kuthibitishwa au kubainika. ...