EPUKA VYAKULA HIVI NDANI YA MWEZI WA RAMADHANI
KUNA aina sita za vyakula na ulaji ambao mfungaji anashauriwa kuepuka ili kulinda afya yake wakati huu wa mfungo wa Ramadhani, vyakula hivyo ni kama ifuatavyo: Vyakula vya kukaanga na vyakula vya mafuta mengi kama chips, sambusa, biriyani, pilau na kadhalika vinafaa kuepukwa kwa sababu vina calories nyingi na virutubisho vichache hivyo kusababisha mlo uwe usio na uwiano. Hii husababisha shibe isiyo na faida na huongeza uchovu wakati wa Ramadhani kwa mfungaji. Pia mfungaji aepuke kula vyakula vilivyo na chumvi nyingi kama achari pickles, sauces, chips na kadhalika kwa sababu chumvi hunyonya maji mwilini. Kutokana na unywaji mchache wa maji ndani ya Ramadhani, utumiaji wa chumvi nyingi unaweza kusababisha upungufu wa maji mwilini, kitaalamu huitwa dehydration na udhaifu wa mwili ndani ya Ramadhani Mfungaji pia aepuke kula vyakula na vinywaji vilivyo na sukari nyingi kama soda, pipi, vinywaji vya kuongeza nguvu n.k. Ingawa vinaweza kukupa nguvu ya haraka lakini vyakula hivi ...