KIFO CHA MWANAMALUNDI , MWANAMALUNDI SEHEMU YA TISA
Hadithi; MWANAMALUNDI Sehemu Ya Tisa ILIPOISHIA... "Mwanangu mpenzi, Mungu asifiwe ile shoka nilikuwa sikosi kuiangalia. Ilikuwa ikipanda tu bila kushuka. Ilipofika juu sana ilisimama kwa miaka Saba. Hatimaye nilifanikiwa kuiona ikiteremka, nilijawa na furaha isiyo kifani. Tena iliteremka kasi sana kisha ilitulia kwa muda wa siku moja. Kisha ikaanza kushuka pole pole. Leo asubuhi nilifurahi mara baada ya kufika ulipoiweka. Isiende mbele wala kurudi nyuma na punde nawe ukatokea. Pia yale maziwa uliyoyaacha hayakuganda ila yalitaka kuganda miaka miwili iliyopita. " Aliongea Mama huyo. Na kweli aliyakuta bado mabichi. ENDELEA... Huko Nera alimkuta yule yule Mtemi Masanja. Watu walipomuona Igulu walianza kunong'onezana, hata mwisho tetesi zikamfikia Mtemi, ambaye bila kukawia alimfukuza pale Nera. Hivyo yeye pamoja na familia yake walihama na kuelekea Seke katika Wilaya ya Shinyanga karibu na Mjini Shinyanga. Huko walimkuta Mtemi Mahizi, ambaye ...