NADHARIA YA MWITIKO WA MSOMAJI
Yaliyomo NADHARIA YA MWITIKO WA MSOMAJI MAANA YA NADHARIA (Williady, 2013), Nadharia ni maelezo yakinifu kuhusu kitu, tajiriba, mahalifa au upumbavu na mafanikio au maangamizi yanayochomoza katika jamii. Hivyo nadharia hufungamana na mambo mbalimbali ya jamii kama vile mbinu, maarifa, tasinifu, mikabala na mienendo mbalimbali ya jamii. 1. NADHARIA YA UPOKEZI (MWITIKO WA MSOMAJI) Nadharia ya Upokezi (mwitiko wa msomaji) ambayo husisitiza nguvu ya msomaji. Nadharia ya Upokezi (Reception Theory) iliasisiwa na wahakiki wa waasisi wa Kijerumani mwishoni mwa miaka ya 1960.Miongoni mwa waasisi wa nadharia hii ni Robert C. Holub,Hans Robert Jauss na Wolfagang Isser.Katika kitabu chake Reception Theory (1984), Holub anaelezea nadharia ya Upokezi kuwa ni Mabadiko ya jumla ya umakinikiaji kutoka kwa mwandishi na kazi yake kwenda kwa matini na msomaji” Nadharia ya upokezi inaakisi mabadiliko ya mbinu katika historia ya fasihi na ilizingatiwa ka...