Posts

Showing posts with the label Kilimo

MKULIMA AMKA: HIZI HAPA FAIDA ZA UPIMAJI WA UDONGO

Image
Leo nimekusogezea elimu juu ya kilimo ili kilimo chako kiwe na tija, Pengine ulikuwa unapata mazao machache kwa kutoujua udongo wa shamba lako,  na virutubisho muhimu vinavyo patikana au kukosekana katika udongo huo   Bofya video hii umtazame mtaalamu kutoka Green Agriculture akitoa elimu juu ya udongo pia wasiliana nae akupe ushauri katika namba zinazoonekana katika video hiyo Usiache kushare na wakulima wengine ili tuwe na uhakika wa chakula katika nchi yetu

NUFAIKA NA KILIMO CHA TIKITIMAJI NA FAHAMU SOKO LAKE

Image
UZALISHAJI WA TIKITIMAJI Tikitimaji ni zao la kitropiki linalo tumia siku 65-90 kutoka kupandwa hadi kuvunwa kulingana na aina ya mbegu uliyotumia na hali ya hewa ya eneo husika kwani maeneo ya pwani na yenye joto sana tikitimaji na mazao mengine hukomaa mapema ukilinganisha na maeneo ya milimani yenye baridi kwa hiyo tunashauri kama unataka kulima tikitimaji basi tafuta sehemu zenye hali ya hewa nzuri kuendana na mahitaji yako na soko lako lilivyo ENEO Chagua eneo ambalo halina historia ya kuwa na magonjwa au wadudu wanaoshambulia tikiti maji.Eneo ambalo maji yanapatikana kwa urahisi kwa ajili ya umwagiliaji wa tikiti maji ,pia eneo lisilo na udongo wenye chumvi chumvi na unaotuamisha maji soma hapa kujua aina za udongo  Namna ya kutambua udongo wenye chumvi na namna ya kuondoa chumvi , Njia za kupima na kutambua aina ya udongo kwenye shamba lako , tikiti maji linastawi sana katika udongo tifutifu na kichanga lakini udongo wa mfinyanzi sio mzuri sana kwa tik...