NOTES ZA KF 202 FASIHI ANDISHI
FASIHI ANDISHI USHAIRI, RIWAYA,HADITHI, TAMTHILIYA I. USHAIRI Kuna mitazamo ya aina mbili katika kuelezea dhana ya ushairi. kuna wanamapokeo na mamboleo. Hata hivyo kabla ya kuendelea zaidi kuwachambua tuangalie wataalam mbalimbali wanavyofasili dhana hii . Dhana ya ushairi imejadiliwa na wataalamu mbalimbali huku kila mmoja akitoa fasili yake. Baadhi ya wataalam hao ni kama ifuatavyo: MAPOKEO Mssamba, (2003) akimnukuu Shaban Robert, anasema; “ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi zaidi ya kuwa na sanaa ya vina ushairi unaufasaha wa maneno machache au muhtasari.” Mnyampala (1970) anasema kuwa “ushairi ni msingi wa maneno ya hekima tangu kale ndicho kitu kilichobora sana maongozo ya Dunia kwa kutumia maneno ya mkato na lugha nzito yenye kunata iliyopangwa kwa urari wa mizani na vina maalum.” Amri Abeid (1954:1) anasema kuwa “ushairi au utenzi ni wimbo, hivyo kama shairi haliimbiki halina maana Abdulatifu anasema kwamba ushairi ni ule ulio na sif...