FASIHI ANDISHI



USHAIRI, RIWAYA,HADITHI, TAMTHILIYA




I. USHAIRI

Kuna mitazamo ya aina mbili katika kuelezea dhana ya ushairi. kuna wanamapokeo na mamboleo. Hata hivyo kabla ya kuendelea zaidi kuwachambua tuangalie wataalam mbalimbali wanavyofasili dhana hii . Dhana ya ushairi imejadiliwa na wataalamu mbalimbali huku kila mmoja akitoa fasili yake. Baadhi ya wataalam hao ni kama ifuatavyo:


MAPOKEO

Mssamba, (2003) akimnukuu Shaban Robert, anasema; “ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi zaidi ya kuwa na sanaa ya vina ushairi unaufasaha wa maneno machache au muhtasari.”

Mnyampala (1970) anasema kuwa “ushairi ni msingi wa maneno ya hekima tangu kale ndicho kitu kilichobora sana maongozo ya Dunia kwa kutumia maneno ya mkato na lugha nzito yenye kunata iliyopangwa kwa urari wa mizani na vina maalum.”


Amri Abeid (1954:1) anasema kuwa “ushairi au utenzi ni wimbo, hivyo kama shairi haliimbiki halina maana

Abdulatifu anasema kwamba ushairi ni ule ulio na sifa ya ulinganifu wa vina na mizani, lugha laini (lugha tamu) na lugha hii iweze kugusa moja kama ilivyokusudiwa.

Encyclopedia American (EA) inaeleza kuwa ushairi ni kauli zenye hisia na ubunifu, mpangilio fulani wenye urari, uwasilishaji wa tajiriba au mawazo ya mtunzi kwa maana ambayo huibua tajiriba kama hiyo katika nyayo za wasomaji au wasikilizaji na kutumia lugha ya picha yenye wizani wa sauti

MAMBOLEO

Kezilahabi ( )anasema kuwa “ushairi ni tukio hai au wazo ambalo limeonywa kwetu kutokana na upangaji uzuri wa maneno fasaha yenye mizani Fulani ili kuonyesha ukweli”

Topan (1996) anasema kuwa “shairi ni unaoeleza hisia za ndani za binadamu kwa mpangilio Fulani wa maneno” hivyo kwa mujibu wa Topan ushairi lazima uguse hisia za ndani ya moyo wa binadamu.

Njogu na Chimerah (1999) wanasema “ ushairi ni sanaa ya lugha inayoeleza jambo kwa njia ya mkato na kwa namna inavyoteka hisia za msomaji au msikilizaji”

Mulokozi na Kahigi (1982:25) wanasema ushairi ni “sanaa inayopambanuliwa kwa mpangilio maalum na fasaha na wenye muwala, kwa lugha ya picha, sitiari au ishara katika usemi, maandishi au mahadhi ya wimbo ili kuleta wazo au mawazo, kufunza au kueleza tukio au hisia fulani kuhusu maisha au mazingira ya binadamu kwa njia inayogusa moyo.”

Hivyo basi tunaweza kusema kuwa ushairi ni kazi ya sanaa yenye kuandikwa au kuimbwa kwa kufuata kanuni za ushairi au

kutofuata kanuni za ushairi ikiwa na maana kuwa ushairi waweza kuwa wa kimapokeo au wa kisasa ilimradi ushairi huo uwe na ujumbe

Katika ushairi FANI na MAUDHUI ni muhimu sana, mawazo fikra au sihi za ndani ni vitu muhimu sana katika ushairi



CHANZO/CHIMBUKO LA USHAIRI



Dhana ya chimbuko inafasiliwa na TUKI (2004) kuwa ni mwazo au asili ya.


kitu

Baadhi ya wataalamu wameweza kuelezea chimbuko la ushairi wa Kiswahili kwa kuzingatia mitazamo au nadharia mbili ambazo ni kama ifuatavyo:



1. Nadharia ya kwanza inadai kuwa; Chimbuko la ushairi wa Kiswahili ulitokana na ujio wa Waarabu.


2. Na nadharia ya pili inasema kuwa; Chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni zao la jamii ya waswahili wenyewe.



Hapa tunaenda kuzielezea nadharia hizi kila moja na kujaribu kuona ubora wake na udhaifu wake katika kuelezea chimbuko la ushairi



1.Na nadharia ya pili inasema kuwa; Chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni zao la jamii ya waswahili wenyewe.



Kwa kuanza na Lyndon (1962) “Swahili Poetry” anatoa hoja tatu ambazo ni:



ushairi wa Kiswahili umetokana na Uislamu,


ushairi ulianzia kwenye upwa wa kaskazini mwa Kenya hususani Lamu.



Na maudhui ya ushairi wa Kiswahili yalitokana na ushairi wa Kiarabu. Utungo wa kwanza wa ushairi andishi wa Kiswahili ni Tambuka, Mwengo bin

Athmani (1728)

Ubora wa Nadharia hii



Ubora wa nadharia hii au mtazamo wa Harries kuhusu chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni kwamba umesaidia wengine kuendelea kuchunguza zaidi kuhusu chimbuko la ushairi wa Kiswahili.



Udhaifu wa nadharia hii



Udhaifu wa nadharia hii ni kuwa si kweli kwamba ushairi wa Kiswahili uliletwa na Uislamu bali ulikuwepo hata kabla ya ujio wa Uislamu, kwani ushairi hautenganishwi na jamii husika. Hivyo jamii za waswahili walitumia Nyanja mbalimbali za ushairi katika shughuli zao mbalimbali au shughuli zao za kila siku, kama vile; shughuli za kilimo na ufugaji.


Pia ushairi wa Kiswahili ulianza karne ya 10BK na ushairi wa Kiswahili ulikuwa ukitungwa na kughanwa kwa ghibu bila kuandikwa. Wataalam wengi wanakubaliana kuwa asili ya ushairi wa Kiswahili ni tungo simulizi hasa ngoma na nyimbo.



Udhaifu mwingine katika mtazamo wake wa kusema kuwa ushairi ulianzia pwani ya kaskazini ya Kenya si kweli kwa kuwa waswahili walikuwepo hata sehemu nyingine kama vile Kilwa na Bagamoyo ambapo ushairi wa Kiswahili ulitumika.



Hoja ya kusema ushairi wa Kiswahili ulitokana na Kiarabu haina mashiko kwa kuwa waswahili walikuwepo hata kabla ya waarabu na walikuwa na ushairi wao isipokuwa ujio wao ulileta athari kubwa kwa kuwa ulichanganya na mambo ya dini ya kiislamu na hati.


Knappert (1979) “Four centuries of Swahili verse” anasema; “Ushairi wa Kiswahili ulichipuka kwenye upwa wa Kenya kutokana na nyimbo na ngoma za waswahili na ulianza katika karne ya 17 na pia ni ushairi wa Kiislamu wenye kuchanganya sifa za tungo za kiafrika na za kiajemi.

Ubora wa hoja hii ni kwamba, ni kweli Knappert amekubali kuwa,ushairi wa Kiswahili ulitokana na waswahili wenyewe.

Hata hivyo hoja yake ina udhaifu kwa kuwa ushairi wa Kiswahili ulianza kabla ya karne ya 10 BK na pia amejikita katika maudhui ya mambo mengine kama vile siasa, uchumi na kijamii. Vilevile amechanganya chimbuko la ushairi wa Kiswahili na Uarabu.



2. Nadharia ya pili inasema kuwa ushairi ni zao la waswahili wenyewe.



Nadharia hii imejadiliwa na wataalam mbalimbali akiwemo Shaban Robert, Jumanne Mayoka (1993) na Senkoro, Mulokozi na Sengo.



Jumanne, M. Mayoka (1993) anasema ushairi umetokana na jamii ya wanadamu wenyewe na umesheheneza ukwasi mkubwa wa lugha ambayo imekuwa ikitumika katika hatua zote za kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni katika historia ambayo mwanadamu amepitia, Kwa mfano kuwa msamiati uliotumika tangu enzi za kuishi mapangoni, enzi za uwindaji, ujima,


utumwa, vita vya makabila, uvamizi wa wageni, ukoloni na harakati za kupambana na ukoloni hadi kupata uhuru na maendeleo yake.



Ubora wa hoja



Ubora wa hoja hii ni kwamba ina mashiko ndani yake kwa sababu, kila jamii ina sanaa yake na ushairi ni moja kati ya sanaa hizo ingawa inaweza ikaathiriwa na sanaa ya jamii nyingine. Pia ushairi umekuwa ukikua na kuendelea kadri jamii inavyokuwa na kuendelea.



Udhaifu wa hoja.



Udhaifu wa hoja hii ni kwamba si kweli kuwa katika kipindi hicho ushairi ulikuwa tayari umesheheni ukwasi mkubwa wa lugha, na kama ulikuwa kweli umesheheni huu ukwasi wa lugha alipaswa kutuonesha huo utajiri wa lugha anaouzungumzia katika ushairi.



Senkoro (1988) anasema kuwa ushairi uliibuka pale lugha ilipoanza katika kipindi cha uhayawani (kipindi ambacho mwanadamu alipoanza kupambana na mazingira yake) kwenda katika kipindi cha urazini (maana) ili kumwezesha binadamu na mazingira yake kwa mfano, zana za kazi zilizotumika ziliwafanya waimbe kwa kufuata mdundo wa zana hizo.



Masamba anasema kwamba kimsingi chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni waswahili wenyewe katika nyimbo, ngoma nk ambazo ziliimbwa katika masuala ya kilimo, jando na unyago n.k. Massamba anaendelea kusema kwamba nyimbo hizi zilikuwa zikiimbwa bila kufuata vina na mizani lakini kwa kadri muda ulivyoenda walizidi kuziendeleza na kuziboresha. Hivyo





6


 


suala la vina na mizani lililetwa na wageni sio kiini cha ushairi wa kiswahili



Mulokozi fasili ya fasihi haiwezi kutenganishwa na utamaduni wa maisha ya watu. Anaelezea kuwa ushairi wa Kiswahili hutumia lugha ya Kiswahili, hivyo ili kujua chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni lazima ujue juu ya waswahili wenyewe

Pamoja na kuwa nadharia hii imeonesha kukubalika na wataalamu mbalimbali kama vile Senkoro, Mayoka na Shekhe Amri Abeid, lakini bado ina mapungufu. Hii ni kwa sababu imeshindwa kuonesha muda maalumu ambapo ushairi wa Kiswahili ulianza na ni wapi ulianza kutumika. Hili ni suala ambalo linaumiza vichwa vya wataalamu mbalimbali hadi hivi sasa, kwani hakuna mtaalamu yoyote aliyefanikiwa kuonesha ni wapi na ni lini ushairi wa Kiswahili ulianza.

Hivyo basi, kutokana na nadharia hizo mbili tunaungana na nadharia inayosema kuwa, chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni zao la waswahili wenyewe, kwa sababu waswahili wana utamaduni wao ambao ulikuwepo kabla ya ujio wa Waarabu. Na waliutumia ushairi huo katika shughuli mbalimbali za kijamii, kwa mfano katika harusi, jando na unyago.


AINA ZA USHAIRI/BAHARI ZA USHAIRI

Kwa ujumla ushairi upo katika makundi mbalimbali. Uainishaji wa ushairi unategemea wataalam. Mlokozi (1996) anadai kuna bahari 13 za ushairi ambazo kwa mujibu wa tapo la wataalamu wa Mombassa



1. Wimbo/Tathilitha

Shairi la aina ya wimbo lina mishororo 3 inayoweza kuwa na mikondo tofauti, unaweza kuwa na kina kimoja mwishoni


Mara nyingi wimbo huwa na vipande viwili


2. Shairi/Tarbia


Utungo ambao una mishororo 4 katika kila beti na kila mshororo una vipande 2


Shairi huweza kuwa na maudhui ya namna yoyote ile


3. Utenzi/utendi

Ni ushairi wenye mizani michache kuliko 12

Una vina vinavyobadilikabadilika isipokuwa cha mwisho


Kwa kawaida husimulia visa virefu vya kihistoria.mfn vita nk


4. Zivindo

Ni shairi linalofafanua maana ya maneno

Lengo kuu ni kufunza lugha. Mfn shairi la Kihindi.


5. Tumbuizo

Hauna idadi kamili ya mizani na mishororo


Nia yake ni kutoa hisia ambazo zimembana mtu. Mfn Mbolezi-nyimbo za misibani, nyimbo za kubembelezea watoto


6. Hamziyya


Una mishororo miwili miwili na vina vyake viko mwisho tu wa beti


Ulitungwa na Sharif Aidarus bin Uthman

Ulikuwa ni wa kumsifu mtume Mohamadi S.W.A


7. Dura Mandhuma au Inkishafi

Unatokana na utenzi wa mtu aliyeitwa Inkishafi


Una mambo ya kuonya, kufuata mambo ya kidini na kuelekeza



8. Ukawafi


Una mstari mmoja wenye vipande vitatu Ukwapi-silabi 6


Utao-silabi 4 Mwandamizi 5

Zinahusu maudhui ya kidini


9. Wajiwaji


Ni utungo ambao una mishororo 5 kila ubeti wenye mizani 5


Zinahusiana na mambo ya kidini, kumsifu mtu shujaa na bingwa


10. Wawe au Vave


Asili yake ni kaskazini ya mwambao wa Pwani hasa sehemu za Amu na Pate


Unahusu kilimo, ziliimbwa wakati wa kufyeka mistu, kuchoma pori nk


11. Kimai


Ni utungo unaohusu mambo ya baharini au wakati wavuvi wanapomtafuta mwenzao ambaye amepotea


Ni utungo unaohusu ubaharia


Idadi ya mizani hubadilika badilika na vina si vya lazima


12. Ngonjera


ni mazungumzo au mabishano ya kishairi kuhusu mada Fulani


huundwa kwa kulumbana pande mbili

suluhisho la kile kinachojadiliwa hupatikana mwishoni


13. Kikwamba


Ni utungo ambao neno moja hutumiwa kila mwanzo wa ubeti na neno hilo hufululizwa na mabadiliko mbalimbali.



MABADILIKO NA MAENDELEO YA USHAIRI WA KISWAHILI

MAENDELEO YA KIHISTORIA:

Wataalamu ambao wanajaribu kutupa taarifa kuhusu maendeleo ya ushairi wa Kiswahili ni pamoja na M.M. Mulokozi (1996) ambaye anatuambia kwamba ulianza karne ya 10BK

Katika kipindi hiki hakukuwa na ushairi ambao ulikuwa umeandikwa kwa utamaduni wa Waswahili bali kulikuwa na ushairi simulizi uliganwa kwa ghibu


Kuanzia miaka ya 1000BK wakati wa ukoloni kulitokea athari kubwa katika ushairi wa Kiswahili k.v hati ya maandishi na dini ya kiislamu


Ushari uliwaunganisha Waswahili na duni pana ya umma na taaluma ya uandishi kwa hati ya Kiarabu uliwapa wenyeji ujuzi wa kusoma na tabia ya kuandika



1000-1500BK

Katika kipindi hiki kulikuwa na ustawi na ustaarabu wa kimji wa waswahili katika miji yote ya Pwani na biashara ilistawi kati ya wageni na wenyeji


Katika kipindi hiki fasihi pia ilistawi


Mashujaa wanaosimuliwa katika tendi k.v Fumo Lyongo waliishi kipindi hiki

Ushairi uliendelea kuwa simulizi


Ushairi wa mwanzo uliitwa SWIFA



1500-1750BK

Hiki ni kipindi cha tatu na kilikuwa kipindi cha misukosuko ya wenyeji na Wareno


Kulikuwa na tungo zilizohidhiwa zilizowahusu Wareno, Migeni, Poatugei afila


Tungo nyingine zilikuwa ni utendi wa Hamziyya, Siri Lasinari, Utendi wa Tambuka 1723 nyingi zilikuwa zikiwapa moyo Waswahili


Waswahili walifanikiwa kuwaondoa wareno.


1750-1900


Hiki kilikuwa ni kipindi cha nne, na kilikuwa ni kipindi cha utawala wa Waarabu


Kulikuwa na migogoro mingi ya kivita katika utawala wa Waarabu


Tabia za Mamwinyi, wafanya biashara, matajiri na wamisionari vilistawi


Kipindi hiki kilitawaliwa na fasihi ya kidini ambayo ilitafakari theologia na falsafa ya maisha


Kulikuwa na tendi nyingi zilizoibuka kuko Arabuni wakati wa mtume Muhamed. Mfn Shutaki, Angamia, Nakaa, Masahibu nk


Pia kulikuwa na tungo za kitamaduni, mawaidha na tumbuizo. Mfn utendi wa Mwanakupona


Washairi walijitokeza kuhusu mashairi ya kisiasa ambao ni Myaka bin Haji (1776-1840), huyu aliishi Mombassa


KARNE YA ISHIRINI 

Katika kipindi hiki uchapishaji wa magazeti na vitabu ulijitokeza. Kulikuwa na Asasi za kudai uhuru. Waandishi waliandika sana kuhusu kudai uhuru. Mfn Saada Kandoro


Baada ya uhuru ushairi wa kisiasa ulienea zaidi kama vile Ngonjera na makue.




MAJARIBIO NA MABADILIKO KATIKA USHAIRI WA KISWAHILI



Senko ( ) anasema baada ya fahamu zake kufunguliwa alianza kuangalia mabadiliko katika ushairi.alidai kuwa kuwa kuwa dunia inabadilika hivyo na ushairi hauna budi kubadilika.



Wangai Mwai (2008:73) fasihi hubadilika badilika katika kumbo na maudhui kwa hiyo ushairi wa Kiswahili sharti uruhusu mabadiliko yanapotokea.



MGOGORO WA USHAIRI WA KISWAHILI


Baadhi ya washairi kama vile E.Kezilahabi, M.M Mulokozi, K.K Kahigi na wengineo walinza kuandika kazi za ushairi zisizo na urari wa vina na mizani


Wengi walichukulia na kurudi nyuma kwa ushairi lakini waandishi hao waliona ni hatua ya maendeleo


Hivyo mashairi yaliyotungwa kwa mfumo huo yalipata majina mbalimbali kama vile Makue, Mtiririko, Mapingiti. Nk


Na hivyo watungaji wa mashairi haya waliwaita wanamapinduzi na wengine wakawaita wachochezi


Ibrahim Noor Shariff (1988:183) amedai kuwa mzozo uliibuka pale wanamabadiliko walipodai mambo matatu:


1) Mbinu za kutunga mashairi zilikuwa chache mn


2) Sharia za kutunga mashairi ziliwanyima uhuru wa kutunga


3) Muundo wa tungo za kishairi uliokuwa wa Kiswahili hapo awali haukuwa na vina wala mizani, hivyo sharia si za lazima.


Kauli hizi za wanamabadiliko zilipingwa sana na wanamapokeo ambao waliamini kwamba urari wa vina na mizani ndiyo roho ya ushairi, ruwaza ya vina na mizani ndizo zinazoufanya ushairi wa Kiswahili ujitambulishe.


Njogu na Chimerah (1999:113) wanadai kwamba mgogoro huu ulikuwa baina ya vijana na wazee waliokuwa wamekulia katika mazingira ya tungo za vina na mizani


Mawazo yao kwa ujumla yalipingana kwa kiasi kikubwa na mawazo ya wanamapokeo japo kuna mazingira Fulani walifanana. Wanamabadiliko waliamini kuwa



Hakuna sheria za kutunga mashairi (Kezilahabi 1977:60), kila shairi lina njia yake ya kutunga na njia yake ya kutoa mawazo.


Dhamira/maudhui, mawazo, maadili na falsafa zitawale fani ya ushairi


Walidai kuwa mabadiliko ya umbo la ushairi yamefungamana na maendeleo ya historia ya jamii zetu, ni sehemu ya jamii yetu,hivyo kubadilika kwa ushairi wa Kiswahili si kitu cha kigeni


Vina na mizani ni kunga za utungaji zilizozuia ushairi wa Kiswahili kukua na kusambaa kwa mapana yake na marefu yake.

Soma Njogu na Chimerah (1999) ufundishaji wa fasihi.




II. RIWAYA

Riwaya sio utanzu wa muda mrefu sana bali ni utanzu ambao umeanza kushika mashiko hivi karibuni kuanzia karne ya 19 huko Ulaya


Encloypedia hudai kuwa riwaya ni ubunilizi ya kinathari1 inayotosha kuwa kitabu (kitabu kwa mujibu wa UNESCO ni chapisho lolote lenye kuanzia kurasa 48 na kuendelea.) bunilizi


ya kifasihi ni ambapo matukio mengi yamebuniwa



Enclopedia Bratanica wanasema “riwaya ni masimulizi marefu ya kubuni ya kinathari yaliyochangamana kiasi na yenye kuzungumzia tajiriba2 ya binadamu. Wanaendelea kusema kwamba kwa kawaida riwaya huwa na mfululizo wa matukio yanahusiana na yenye kulihusu kundi Fulani la watu kaka manthari mahususi



Mphahlele (1976) anasema kwamba riwaya fupi huwa na kati ya maneno thelathini na tano elfu (35,000) na hamsini elfu (50,000) na riwaya ndefu zaidi inaweza kuwa na maneno zaidi ya sabini na tano elfu (75,000)



Mhando na Balsidya wanadai kwamba katika riwaya lazima kuwe na mchanganyiko wa matukio na ujenzi wa wahusika naye Foaster (1949) anachangia kwa kusema kwamba riwaya lazima iwe na wakati.



SIFA ZA RIWAYA


Ni masimulizi ya kubuni


Ni hadithi ya nathari katika masimulizi



1 nadhari-ni maelezo ya kina yanayoelezea jambo kwa mapana (hii inafanya itofautiane na ushairi na tamthiliya


2 Tajiriba ni uzoefu alio nao mtu. Uwe mbaya au mzuri

 

Ni ya mpangilio au hakuna mpangilio


Inafungamana na wakati (yaani yale yanayotendeka katika jamii hiyo)


Ina sifa ya urefu kama tulivyoona hapo juu


Ina mawanda mapana (yaani inaweza kuzungumzia mambo kwa upana sana)


Lazima kuwe na mchangamano wa visa mfano; katika riwaya ya Janga Sugu la Wazawa ina visa kama, ushirikina, vifo, mapenzi ya kweli na ya uongo,ndoa, mila nk


Ina wahusika wengi





CHIMBUKO LA RIWAYA

Riwaya imejazwa na mambo makubwa mawili:

1) Fani za kijadi za fasihi


2) Mazingira ya kijami

a) Ngano-hadithi za kubuni zinazohusu wanyama, watunzi wengi wameathiriwa na ngano kw wasababu wanachota visa, mbinu za kifani , dhamira katika ngano (zinaonekana kwamba ni za kingano zaidi)

b) Visasili-masimulizi ya kubuni ambayo yanaeleza juu ya maisha, asili, ya vitu na hatima yake. Kwa kawaida visasili huaminiwa kuwa ni hadithi za kweli


c) Visakale-ni hadithi za kale zinazohusu kabila la kale, udini nk. M.M.Mulokozi anasema kuwa kila kabila lina visakale vyake. Katika riwaya visakale vinajitokeza katika riwaya ya Kisima cha Giningi



d) Hekaya-ni hadithi za kusisimua kuhusu masaibu na matukio ya ajabu yasiyo ya kawaida, mara nyingi masaibu yanasababishwa na mapenzi, huwa ni ndefu kuliko hadithi nyingine lakini si ndefu kuliko riwaya. Katika taaluma ya Kiswahili ni riwaya ya Adili na Nduguze-Shaaban Robert,


Riwaya ya Ubeberu Umeshindwa ya KIIMBILA( 1971)


e) Tendi-ni hadithi ya kishairi kuhusu mashujaa wa kihistoria na wakubuni wa jamii au taifa.mfano Utendi wa Fumo Lyongo, kuna baadhi ya riwaya zimeiga mbinu za kiutendi. Mfano huko Ulaya Illiad Odyssey, Don Tuliv 1928, Toistoi (1828-1910). Mfano katika Afrika ni riwaya ya Ngugi wa


Thiong’o ya Matigali.


f) Masimulizi ya wasafiri-ilihusu masaibu waliyopata wasafiri mbalimbali. Mfano Riwaya ya kiingereza ya kwanza ni Robinson Kruso ilihusu habari ya mhusika mkuu ambaye alikuwamo katika merikebu iliyozama na akaokoka na kuamua kuiishi katika kisiwa peke yake. Katika Kiswahili


kuna riwaya kama vile “utumwa” “Kwa Heri Iselamagazi” hizi zote ziko katika muundo hu



Katika karne ya 16 fani nyingi ziliendelea. Na mojawapo ya sababu ya kuendelea kwa riwaya ilikuwa ni:

1) Ukuaji mkubwa wa shughuli za kiuchumi huko Ulaya baada mapinduzi ya kiviwanda


2) Mageuzi ya kijamii na kisiasa yaliyofungamana na mabadiliko ya kiuchumi


3) Ugunduzi wa teknolojia ya upigaji chapa


Mpaka sasa hakuna vigezo maalumu vya uainishaji wa riwaya, kila mtaalamu huangalia kwa jinsi anavyoona yeye.

Wengine wanaangalia muundo, mtindo, umbo, lengo/shabaha/historia. Madumula (2009:61 anasema “riwaya inaweza kuainishwa kifani, kidhamira, kihistoria na kiitikadi



Naye Mulokozi M.M (1996) anaonyesha michepuo miwili ya riwaya:



1) Riwaya ya dhati

2) Riwaya pendwa



Katika mhadhara huu tutaangalia riwaya kama alivyoainisha Madumula


Inahusu maisha ya mtu binafsi, yaani mwandishi mwenyewe, tatizo hapa ni uaminifu wa mwandishi, si rahisi kuandika kweli yote.


Mfano katika Kiswahili ni Riwaya “Maisha yangu baada ya miaka 50” ya Shaaban Robert


Inahusu mtu mwingine na siyo mwandishi mwenyewe


Pia inahusu maisha ya mtu binafsi lakini ni maisha ya mtu mwingine na siyo ya mwandishi mwenyewe


Ni matukio ya kusisimua ambayo hayajawatokea watu wengine


Lengo kuu ni kueleza ugumu wa maisha ya maisha ya mhusika mkuu jinsi anavyopambana na maisha. Mfano


Wasifu wa Siti Binti Saadi ya Shaaban Robert






Ina lengo la kufundisha maadili mema ambayo ndiyo msingi katika maisha


Inahusu: mateso na uvumilivu, majuto baada ya kutambua kosa. Mfano katia Kiswahili ni Adili na Nduguze,


Kusadikika, Kufikirika-zote za Shaaban Robert



Huchanganya historia halisi na sanaa ili kuleta maudhui Fulani


Hazielezi matukio yote ya kihistoria bali yale ya muhimu tu, yaliyoathiri mwelekeo na mwenendo wa jamii Fulani


Maudhui yake ni kumbukumbu ya mambo yaliyopita na dhamira zake huwagusa watu wengi. Mfano katika Kiswahili ni Riwaya ya Uhuru wa Watumwa ya J. Botela,


Kwa Heri Iselamagazi ya J Mapalala, Zawadi ya Ushindi ya Beni Mtobwa, na Njozi iliyopotea ya Mung’ong’o



Inahusu maisha ya watu na msisitizo wake ni katika mila, desturi na mabadiliko ya kijamii


Dhamira huanzia ngazi ya familia hadi kitaifa na hata kiulimwengu


Husawiri matatizo yaliyo katika jamii kwa kuonyesha chanzo chake. Mfano katika Kiswahili ni Dunia Uwanja wa Fujo ya Kezilahabi, Siku ya Watenzi Wote ya Shaaban Robert na Harusi ya J.Safari



Aina hii inaweka mkazo juu ya mikinzano ya ndani ya binadamu, kiakili, kinafsi na kijinsia


Huonyesha uwezo na udhaifu wa binadamu katika kuzikabili hali ngumu za maisha


Mhusika mkuu husukumwa katika ukingo wa aidha kufa ili ayaepuke matatizo au aishi na hayo matatizo. Mfano katika Kiswahili ni riwaya ya KIU ya Muhamedi S.Abdalah, Nyota ya Rehema ya huyu huyu Muhamed, Rosa Misitika ya Kezilahabi na Kichwa Maji ya Kezilahabi


Ni riwaya ambayo inajadili matatizo ya kisiasa


Inalenga kuleta mabadiliko ya kisiasa na kijamii


Mara nyingi riwaya za kimapinduzi zina mwelekeo wa kisosholisti ambapo mlengwa mkuu ni umma kushika hatamu


Mkazo upo katika ITIKADI kama msingi na dira ya kuongoza jamii

Wahusika wake wanatoka katika matabaka mbalimbali


Mfano  katika  Kiswahili  ni  riwaya  ya  KULI  ya  Adamu


Shafi, Utengano ya Saidi A Mohamed, Dunia Mti Mkavu ya S.A.Muhamedina KASRI MWINYIFUAD ya Shafi A Shafi



Inajadili migogoro na maisha ya binadamu kwa kutafakari kwa mantiki na kwa kina kuhusu mambo yanayohusu maisha


Inajadili maswali kama vile: maana ya maisha nini? Hatima ya binadamu nini? Uhusiano wa binadamu na malaika ukoje?


Mifano ya riwaya ya kifalsafa ni: Mzingire, dunia uwanja wa fujo, Nagona, babu alivyokumbuka ya S.A Muhamedi, Riwaya ya Binadamu-ya K.w Wamitila. Riwaya hizi ni ngumu sana kuelewa zinaelezea, hata wahusika wake ni wa kufikirika zaidi, mfn wanyama nk






 




Ni riwaya ambazo hujishughulisha na masuala ya upelelezi, mapenzi na ujasusi, mara nyingine zinahusisha mapigano ya kimwili na ya kiakili kati ya mtu mmoja na watu wengi. Na mara nyingi huyu mtu mmoja huwashinda watu wengi


Riwaya hii inakuwa na mhusika mkuu mkweli (ambaye anapewa sifa ambazo zinazidi uwezo wa mwanadamu wa kawaida-yaani huwezi kumshinda kuanzia mwanzo hadi mwisho). Riwaya za namna hii zina chumvi nyingi.


Mfano Riwaya ya “Kifo ni haki yangu” mhusika wake mkuu Camila anayekata nyeti za wanaume. Mfano mwingine ni Simu ya kifa ya Faraji Katambula, Kikosi cha Kisasi ya E.Musiba. Mzimu wa watu wa kale, Kosa la Bwana Msa-vya Muhamedi S.Abdula-mhusika wake mkuu ni Msa





Utanzu wa riwaya umekuja baada ya utanzu wa ushairi na tamthiliya lakini ukuaji wake umekuwa kwa kasi kubwa. Inasemekana kwamba riwaya ya Kiswahili ilianza kujitokeza katika mwisho mwa karne ya kumi na tisa. Kwa nini ilichelewa sana hapa Afrika? Sababu yake ni kwamba


1. Hadhira kubwa ya watu haikujua kusoma na kuandika


2. Hadhira kubwa ya watu haikuweza kununua vitabu


3. Jamii ya waswahili haikuwa na mitambo ya kupigia chapa na pia haikuwa na mfumo mzuri wa usambazaji vitabu(hapakuwa na printers nk)



20


 


Hivyo tunaona kwamba wakati wa ujio wa wakoloni ulisababisha kuanzishwa kwa baadhi ya vituo vya kupigia chapa, kwa mujibu wa Mulokozi ( ) anasema ukoloni uliweka mazingira ambayo yameweza kuilea riwaya. Mfano: hati ya maandishi ya Kirumi, mfumo wa usambaji wa vitabu



Mwanzo riwaya ya Kiswahili ilianza kujitokeza kwanza kama tafsiri ya kazi za nje, hivyo tafsiri nayo ilisaidia sana kuchipuka kwa riwaya. Kwa kadri tafsiri zilivyokuwa zikifanywa, waswahili walianza kuiga vitabu hivyo.








Kamati hii ilihimiza uandishi katika lugha ya Kiswahili kwa njia ya kushindana. Hivyo ilianzisha mashindano ya uandishi wa Kiswahili. Riwaya ya kwanza ya Kiswahili ilikuwa Uhuru wa Watumwa ya MBOTELA Ilichapwa mwaka 1934, riwaya nyingine ni riwaya ya “Mzimu wa watu wa kale”na “Simu ya Kifo”






Kulijitokeza riwaya ambazo zilikuwa zikifuata mkondo wa


kingano.Njogu na Chimerah (2008) wanaeleza kuwa”kimaudhui riwaya nyingi zilikuwa na mambo ya kimila na tabia kama njia ya kutunza maadili. Miongoni mwa riwaya hizo ni Utu bora mkulima, Kufikirika, Kusaidikika, Adili na Nduguze na Siku za watenzi wote zote za Shaaban Roberti.



Kulikuwa na mambo yafuatayo:



Ukombozi wa bara la Afrika na ujenzi wa jamii mpya, hivyo maudhui yake yalikuwa ni ujenzi wa jamii mpya na:





 

Kusuta ubinafsi na ukandamizaji


Zilikuwa zikihakiki unyama wa maisha ya kimiji


Zilikuwa zikiielekeza jamii katika mkondo wa kibinadamu katika usawa na ustawi. Mfano riwaya hizo ni LILA NA FILA, KABURI BILA MSALABA-iliandikwa na KAREITHI



Katika kipindi hiki pia kulijitokeza kundi la Riwaya Pendwa zilizohusu upelelezi na uharifu mfano Mzimu wa watu wa kale, Kisima cha Giningi, Simu ya Kifo



Zile za uharifu ni MTAKA YOTE HUKOSA YOTE ya Leo Odera Omera, Tatizo Kisauni ya CHADHORO

Ni kipindi cha kupevuka na kushamiri kwa riwaya ya Kiswahili, katika kipindi hiki riwaya nyingi zilianza kujishughulisha na uongozi na usaliti wa kisiasa.


Njogu na Chimerah (2008) wanadai wasanii walianza kutafakari jinsi ukoloni ulivyoanza kufungua milango kwa watu wachache na kutumia mali kwa manufaa yao wenyewe


Katika kipindi hiki kuliibuka riwaya za kihistoria kwa mfano KWA HERI ISELAMAGAZI iliyoandikwa na Mapalala. Miradi Babu ya wazalendo.


Katika kipindi hiki kulizuka riwaya ya kifalsafa na ya majaribio. Mfano Nagona 1987, Mzingile(1991)-Kezilahabi. Riwaya ya Zilahiri na Zirani ya William


Katika kipindi hiki kulikuwa na ongezeko la riwaya ya vijana na watoto. Mfano wa riwaya hizo ni Mashujaa wa Kaza kamba-ya Shija (1980) wimbo wa Sokomoko (1990), Ngome ya Mianzi (1990), Ngoma ya




 


Mianzi(1991) Moto wa Mianzi (1995) zote hizi ni za Mulokozi.


Fasihi huithamini jamii kihistoria, kiitikadi, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni na kijamii, na kwa kuwa jamii imekuwa ikibadilika badilika kimtazamo, fasihi nayo imekuwa ikibadilika kwa sababu jamii inabadilia. Na hivyo fasihi nayo inahitaji kupokea mabadiliko hayo ili kwendana na jamii husika.



Mabadiliko katika riwaya (fasihi) yanatokea kwa sababu ya wasanii kutumia vionjo vipya katika kuziumba kazi zao. Kama anavyosema Khamisi (2007) anasema,mara moja tunaona neno kionjo linajisemea lenyewe kimya kimya juu ya mabadiliko ya utanzu wa fasihi. Lengo la mabadiliko hayo ni kwamba “chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho”



Utanzu wa riwaya ya Kiswahili haukuepuka mabadiliko. Sababu zilizobadilisha mabadiliko haya ni makali ya wembe wa kisiasa, mfano nchini Kenya makali ya kisiasa yalikuwa dhidi ya Masosholisti. Mfano wa riwaya ni Gamba la Nyoka,



Majaribio na mabadiliko ya riwaya ya Kiswahili yalianza pale ambapo waandishi wengi wa Kenya na Tanzania walipoanza kukataa kukubali kila kitu walichokisikia. Walipoanzaa kukataa kanuni za jamii za ughunaji, hivyo wakaanza kuandika riwaya tofauti na za mwanzo.





23


 

Madumula anawanukuu SCHOLES na APLLOE riwaya huweza kubadiliko kutokana na utanzu wenyewe kuwa hauna mashiko legelege na tepetepe, hubadilika badilika



Hivyo kutokana na majaribio na mabadiliko katika riwaya ya Kiswahili tunaona upywa katika kazi za riwaya katika fani na maudhui yake. Kisanaa riwaya hizi zinachanganya uhalisia na falsafia. Mfano wa riwaya ya Kufikirika. Mfano mwingine ni UKIUSHI-Mtiririko haueleweki, na riwaya hizi zinakuwa na mwingiliano matini yaani kuchanganya kazi nyingi katika kazi moja.kisanaa pia zina wahusika wa kidhani



Pia riwaya hizi zina mazingaombwe sana, kwa mfano katika Nagona lugha yake ni ya mafumbo, visasili, pia ni lugha inayoelekeza, haifafanui sana.kimaudhui riwaya hizi za majaribio inatazama matatizo kwa mtazamo wa ndani. Inashughulikia masuala ya ulimwengu wote, riwaya hizi pia kimaudhui zinaitetea dunia dhidi ya maangamizi ya uovu mkubwa.



3. TAMTHILIYA NA DRAMA



Kumekuwa na mkanganyiko kati ya dhana hizi mbili, watu wamekuwa wakizichanganya sana.



Tamthiliya ni drama na kinyume chake

Tamthiliya ni drama lakini si drama zote ni tamthiliya



A. TAMTHILIYA


Mulokozi (1999:88) tamthiliya ni kazi iliyokusudiwa kutendwa jukwaani kwa ajili ya hadhira fulani



Tamthiliya huitwa mchezo wa kuigiza. Istilahi hii tamthiliya imetokana na neno methali lenye maana ya mfano/ishara ya kitu


Wamitila (2003)tamthiliya ni kazi ya kidrama na ya kimaongezi ambayo huigizwa mbele ya hadhira/kazi iliyoandikwa ili kusomwa


Kimuundo tamthiliya hudhihilika katika:


matendo na maonyesho, mazungumzo huchukua sehemu kubwa katika uwasilishwaji wake wa maudhui (huwa katika diolojia)


haiweki msisitizo mkubwa katika uwasilishwaji wake jukwaani wakati drama inaweka msisitizo mkubwa katika uwasilishwaji wake


Penina Mhando anadai kuwa “Tamthiliya ni ule utungo unaoweza kuwa umeandikwa au haukuandikwa ambao ambao unaliweka wazo linalotaka kuwasilishwa katika umbo la tukio la kiliwezesha kutendeka mbele ya hadhira”


Kutokana na sifa hii ya kutendeka jukwaani tamthiliya inawekwa kwenye kundi la sanaa za maonyesho(Mulokozi)



SANAA ZA MAONYESHO



Mohamedi na Balysidya wanasema kuwa sanaa za maonyesho ni kitendo chochote chenye sifa 4



a) Mchezo

b) Mchezaji


c) Uwanja wa kutendea

d) Watazamaji



©tamthiliya ni andiko la kiuigizaji linalotoa simulio kwa kuonyesha maneno na matendo



 

B. DRAMA

Wamitila (2003) anasema “ ni aina ya utanzu wa fasihi ambao kimsingi hudhamiriwa kuigizwa mbele ya hadhira” inaweza kuwa imeandikwa au haikuandikwa lakini msisitizo wake ni kuigizwa

Msingi mkuu wa drama ni utendaji na utanzu huu umebuniwa kwa ajili ya thieta


Wahusika hupewa majina ya kuigiza mbele ya hadhira



Iwochukuu (2000) anasema “drama ni mabadiliko, ubunifu na usawiri wa uhalisi jukwaani. Msingi mkuu wa drama ni matendo. Hoja hii imeungwa mkono na Aristotle anayeifafanua drama kama uigaji wa matendo



Bretcht anasisitiza kuwa drama si uigaji wa matendo pekee pia ni chombo cha ufafanuzi wa hali za kijamii, chombo cha mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi


Kitendo huitwa drama endapo kitendo hicho ni mwigo wa kitendo cha kilichokwishatangulia.


DRAMA ZA KIJADI



Jamii ya waafrika ikiwemo ambayo utamaduni wake ulikuwa haujaingiliwa na wakoloni ilikuwa na sanaa ya maonyesho zilizogawanyika katika makundi mbalimbali. Balisdya na Mhando walianisha aina mbalimbali za drama hizo



1. SHEREHE


Zilihusishwa na kundi moja kwenda kundi jingine mfano. Jando na unyago, jina kwa mtoto, kuota meno nk


Ziliambatana na madaraka kwa mwanajamaii ya mwanajamii aliyeingia katika kundi jipya. sherehe


ziliwekwa katika katika umbo la vitendo na vikapewa uzuri wa kisanaa


2. NGOMA

Mhando na Balisdya wanasema ni chombo, sherehe au uchezeshaji wa viungo vya mwili. Malengo yake ni kuburudisha


3. MASIMULIZI YA HADITHI


Katika usimuliaji wa hadithi kuna vipengele vya kidrama vinavyojitokeza. Yaani:

Usimuliaji


Uigizaji


Uimbaji


Muziki


4. KUSALIA MIUNGU


Jamii fulani inapopata mafanikio au matatizo fulani ndipo huenda kutambikia miungu yao kwa kushukuru au kuomba kutatuliwa matatizo yao


5. MAJIGAMBO


Masimulizi ya kujigamba ya mtu kuhusu mambo ya kishujaa aliyopata kuyatenda maishani mwake


Kwa kawaida hutumia lugha ya kishairi na masimulizi huambatana na vitendo vya majigambo yenyewe.


Pia yaliambatana na matumizi ya maleba





AINA ZA TAMTHILIYA



1. TANZIA


Ni tamthiliya yenye huzuni inayogusa hisia za wasomaji kiasi cha kuogopesha na kumuonea huruma mhusika mkuu ambaye hupatwa na masahibu/matatizo/majanga hayo




27


 

Msingi mkuu inalenga msomaji kupata hisia

Mhusika mkuu huwa ni maarufu


Aristotle anasema kuwa “ mhusika mkuu lazima atoke katika familia yenye nasaba bora/tabaka la juu”


Si tanzia zote mhusika anatoka tabaka la juu. Mfano KIFO KISIMANI-mhusika mkuu hapa anatokea katika tabaka la chini kabisa



Misingi ya utokeaji wa tanzia


Iamushe hisia za woga na huruma miongoni mwa hadhira


Shujaa lazima awe mtu mwema, sura nzuri,umbo zuri, ili yanayomtokea yasitarajiwe


Mhusika huonyesha kuumia kadri mtu anavyoonekana kuwa ni mwema na ana umbo zuri.


Anguko la shujaa huja kutokana na uamuzi wake ama kosa lake mwenyewe


Katika tanzia ya kirasimi shujaa hutoka katika nasaba bora

2. RAMSA/KOMEDI


Ni tamthiliya ambayo inachangamsha na huishia kwa kufurahisha/ni tamthiliya ya vichekesho, hii haina maana kwamba haina maudhui mazito ndani yake.


Inashughulikia mambo yale yale yanayoweza kushughulikiwa na tanzia. Mfano masuala ya unafiki,uzembe, wivu nk, hata hivyo inayashughulikia kwa namna tofauti na tanzia


Kwa kawaida wahusika wa Ramsa huumbwa vibaya kuliko walivyo


Udhati wa ramsa si kwamba usanii humalizika katika kicheko/furaha zaidi ni kuishia mhusika mkuu kufanikiwa




shujaa wa kiramsa



Si lazima awe mtu maalum/mbabe au shujaa, anaweza kuwa mtu wa kawaida


Kwa mujibu wa Aristotle anasema mhusika wa ramsa lazima awe mtu wa wastani chini ya wastani, awe ni mtu ambaye hatarajiwi kujitokeza na mtu wa nasaba duni na matendo yake yawe ya ucheshi


Ni lazima awe mtu ambaye akifanikiwa wasomaji au watazamaji watafurahi



uhusika wa wahusika wa ramsa


Ramsa inawahusu watu wa kawaida kuliko ilivyo tanzia

Inawahusu watu wa kipato cha kati na cha chini


Na dhamira zote huelekezwa kwa watu wa kipato cha chini na duni. Mfano walalahoi


AINA ZA RAMSA


a) UTANI


Ni aina ya ramsa ambayo mambo inayozungumzia yanaokana kuwa ya kipuuzi


Mambo hugeuzwa kuwa kinyume kabisa na jinsi yalivyo


Kwa kawaida sura za wahusika hubadilishwa kuwa kama vinyago


Lengo kuu ni kuchekesha-ambalo ndilo haswaa, lengo la tamthiliya ya ramsa



b) RAMSA ZA MAPENZI/MAHABA


Hizi zinahusu mapenzi ambapo wapendanao huwekewa vikwazo kama vile fedha, elimu, din, kabila nk


Wahusika hawa hushinda vikwazo hivyo


c) TASHTITI/DHIHAKA


Zinalenga kwa viongozi wa kisiasa au dini

Zinawahusu matapeli, wanafiki, wala rushwa, ni


Mhusika mkuu anakuwa na sifa za utapeli nk


Lengo kuu ni kumdhihaki huyu kiongozi ili aachane na tabia hizo


ni njia ya walalahoi kupeleka malalamiko yao kwa viongozi



SIFA ZA RAMSA



Sharti ivutie akili na siyo hisia


Ni lazima kuwa na matendo bila kufikiria hii itapelekea msomaji au mtazamaji kujua kwamba wahusika hawa hawana akili


lazima iwe na hali ya utu (ikitukumbusha ubinadamu wetu)


sharti iwe na mila na desturi ambazo hadhira inazifahamu toka katika jamii yake


Hadhira isiogope au kupata uchungu kwa sababu hii sio lengo lengo la ramsa


Wahusika wa ramsa hujaribu kuepuka vikwazo ambavyo vimewekwa


Inaonyesha haja ya  kuikomboa nafsi

Mfano wa ramsa ni kama vile MFALME JUHA


d) TANZIA-RAMSA

Hii ni tamthiliya ambayo inaonyesha mabaliko ya aina fulani yanayogeuza matukio ya tanzia kuwa ya ramsa


Ni tamthiliya inayochanganya vipengele vya tanzia na ramsa


Hutumiwa sawa na tamthiliya ya kibwege-hii ni tamthiliya ambayo inaonyesha kwamba kicheko au furaha ndiyo jibu pekee la maisha kwa watu ambao hawana imani na maisha ambao kwao misingi dhabiti ya maisha imeondoleo. Mfano tamthiliya ya AMEZIDI ya S.A Mohamedi


e) MELO-DRAMA

CHIMBUKO , MABADILIKO NA MAENDELEO YA TAMTHILIYA YA KISWAHILI


CHIMBUKO: Tamthiliya chimbuko lake duniani kote linashahibiana/zinapatikana duniani kote na kuonekana katika maumbo tofauti tofauti. Tamthiliya inahusishwa sana na visakale na matendo ya kidini. Katika bara la Ulaya tamthiliya inahusishwa na miviga ya kidini katika jamii ya Wayunani/Wagiriki wa zamani/ancient Greek. Miviga hii katika jamii ya wayunani iliambatana na dua ya kuzaliwa..mpaka kufa na kuoza na kuwa binadamu tena Huko India tamthiliya zilitokana na tenzi zilizoitwa Mahabharata na ………pia zilitokana na miviga

zilizoendana na utendi wa tendi hizo kutika mahekalu ya kidiniKule Japani na China-drama inatokana na dansi na miviga ya kidini baadaye miviga hii ilijitenga na dini na kuanza kujishughulisha na sanaa


Katika Afrika-maigizo ya tamthiliya yalikuwa yanapatikana huko Misiri na maigizo haya yalikuwa


yanahusu kufa na kufufuka kwa mungu wa wamisiri aliyeitwa osiais. Miviga hii ilikuwa inaigizwa kila mwaka kwa miaka kama elfu mbili. Pia katika Afrika kulikuwa na maigizo ambayo hayakuwa yameandikwa lakini yalikuwa ni sehemu ya matendo ya kijamii yaani miviga na ngoma. Kulikuwa na tamthiliya bubu, maigizo ya wato

maigizo ya watani. Drama hizi zilikuwa zikifungamanishwa na fasihi simulizi

ivyo tamthiliya inatokana na mambo makuu matatu a. Miviga na viviga vya kijamii, na dini pamoja na tendi


b. Usawilishaji wa maisha ya kawaida kwa ajili ya burudani, elimu nk


c. Sanaa za maonyesho za kijadi; n