Je nikweli kuwa kuna utofauti katika mazungumzo baina ya mzungumzaji mmoja na mwingine?....

info.masshele@gmail.com

Jibu  ni ndio , na tofauti hizo katika uzungumzaji huweza kuchangizwaa na mambo kadhaa Mwansoko 1991 anasema
" Na hii ina maana kwamba kunahaja ya kuziangalia zile sababu zinazoathiri maumbo ya maneno katika mawasiliano na uchaguzi wa zana za kiisimu zitakazotumiwa na mwandishi au mzungumzaji. Sababu hizi hugawanyika katika mafungu mawili makubwa.:
1. sababu dhahania (subjective factors)
2. sababu yakini (objective factors)
Baadhi ya sababu dhahania ni:
1. hali za kiuchumi na kijamii za washiriki wa mawasiliano (kazi zao, elimu yao, tabaka lao katika jamii... n.k.)
2. hali ya kisaikolojia ya wawasilianao (k.m. tabia zao)
3. jinsi mtu anavyojisikia (mood)wakati wa mawasiliano (mwenye furaha? huzuni? majonzi? wasiwasi?)
4. rika (umri) la washiriki katika mawasiliano.
Ni kweli kabisa kwamba namna ya uzungumzaji wa mtu akiwa katika hali ya mshituko wa furaha huwa ya maneno mengi yenye maumbo yanayoonyesha furaha hiyo, ambapo katika hali ya kawaida kabisa maneno na maumbo haya hayawezi kujitokeza. Hali kadhalika hali ya kisaikolojia (mf. tabia), kiwango cha maendeleo ya kiutamaduni na kielimu cha mtu... n.k. huathiri kwa hali fulani namna ya uzungumzaji (na uandishi) wake.
Lakini sifa hizi haziwezi kuathiri ujenzi na ujipambanushaji wa mitindo ya lugha. Zinachoweza kufanya ni kuathiri tu uzungumzaji wa mtu. Mitindo ya lugha haijengwi na sifa dhahania, bali huletwa na sifa/sababu yakini, ambazo ni pamoja na:
1. njia za kutekeleza mawasiliano (kwa maandiko au kwa mazungumzo);
2. aina/namna ya mazungumzo [mazungumzo ya mtu mmoja akisema pekee (monologue); mazungumzo ya watu wawili(dialogue); mazungumzo ya watu wengi (polilogue)];
3. nyenzo za mawasiliano (za umma k.m. redio, magazeti, vitabu, simu, n.k. au za kibinafisi k.v. barua ya mtu binafsi);
4. tanzu (genre) ya mawasiliano (hotuba mkutanoni, kushiriki katika semina/mjadala, barua, tangazo, hati ya mkataba... n.k.);
5. kazi au shughuli muhimu za jamii.
Hebu sasa tuangalie jinsi sifa hizi yakini zinavyoathiri uundaji wa nutindo katika lugha. Moja ya sifa hizi ni ile ya njia za utekelezaji wa mawasiliano. Ni dhahiri kabisa kwamba uchaguzi wa zana za kiisimu kwa ajili ya mawasiliano ya kimaandiko uhatofautiana sana na ule wa mawasiliano kwa njia ya kuzungumza. Na tena utofautiano huo wa maumbo ya maneno haujitokezi kutokana na matakwa ya mwandishi au sifa fulani maalum za mwandishi huyo, bali unatokana na mahitaji maalum ya kiisimu ambayo ni lazima yajitokeze katika mawasiliano ya kimaandiko.
Ukweli umeonyesha kwamba wakati wowote tuandikapo kitu chochote kama barua za kirafiki, barua za kiofisi au makala kwa ajili ya majarida ya kitaaluma... n.k. hujikuta tunalazimika kufikiria zaidi juu ya sura au miundo ya sentensi tutakazoziandika, mpangilio wake wa maneno utakavyokuwa n.k.... kuliko tnambo yanavyokuwa katika mawasiliano ya kuzungumza. Kwa kifupi, wakati wowote mtu anapotarajia kuandika, lazima kujitokeza “hali fulani ya kujitayarisha” ili kupanga mawazo, maneno na miundo ya sentensi. Kwa upande mwingine mambo haya hayatiliwi maanani au mkazo sana wakati wa kuzungumza. Na hii inaeieweka: mazungumzo yanaruhusu utumiaji wa mbinu nyingi zisizo za kiisimu (m.f. mazingira, kutoa ishara mbalimbali kwa kutumia viungo vya mwilini k.v. vidole, macho n.k., kiimbo) katika kuyafanya mawasiliano yaeleweke, wakati ambapo mawasiliano kwa maandiko hayana nafasi hii. Mawasiliano kwa maandiko yanahitaji mpangilio maalum wa maneno ambao ndio unaweza kubashiri intonesheni itakavyokuwa. Tena uandikapo lazima utilie maanani uwezo wa unayemwandikia wa kuuelewa muundo wa sentensi zako, ama sivyo lengo lako la mawasiliano linaweza lisieleweke vizuri na yule unayewasiliana naye.
Nyenzo za mawasiliano vilevile humlazimisha mtu “kurekebisha” ipasavyo maandiko au nzungumzaji wake. Kwa mfano, mtu (mzima) akikaribishwa kuzungumza kwenye redio uzungumzaji wake utatofautiana kwa hali fulani na jinsi anavyoongea k.m. na familia yake nyumbani. Na “kujirekebisha” huku hakutegemei umri wala tabia ya mtu, bali kunaletwa na urasmi wa chombo hicho na labda pia uzito na umuhimu wa mambo yanayojadiliwa.
Sifa nyingine yakini ni tanzu za mawasiliano na namna ya mazungumzo. Ni ukweli ulio bayana kabisa kwamba bila kutegemea hali ya kisaikolojia au jinsi mtu anavyojisikia au rika lake uandishi wake wa makala ya kitaaluma utatofautiana na ule wa barua ya kibinafsi. Ndio maana mtindo wa makala ya kitaaluma yanayotolewa, kwa mfano, katika semina za Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili na wataalam mbalimbali una hali fulani ya ufanano licha ya kwamba wataalam hao wanatofautiana (sana) katika rika, elimu, tabia zao na kadhalika. Hali kadhalika mazungumzo ya mtu mmoja (k.m. hotuba mkutanoni au mhadhara darasani) bila shaka yatatofautiana na mazungumzo ya watu wawili au wengi zaidi juu ya mada hiyohiyo. Katika kuzungumza watu wengi lazima kutajitokeza kufupisha/kukatisha kwa sentensi, kurudiarudia mambo na sifa nyinginezo za mazungumzo ya hali hii.
Sasa tuangalie jinsi sifa, kazi au shughuli muhimu za jamii, inavyoathiri ujenzi wa mitindo kwa kutumia mfano ufuatao:
Iwapo shughuli yajamii itahusu mambo ya kitaaluma au kisayansi, basi mawasiliano katika shughuli hii yatahitaji kueleza mambo kama yalivyo, kwa kweli tupu bila kuonyesha upendeleo wa wazi au maono ya wawasilianao. Na ili kukidhi haja hii itabidi zichaguliwe oa kutumika zile zana za kiisimu ambazo hazionyeshi upendeleo na maono ya mwandishi au mzungumzaji. Yaani kwenye shughuli za kisayansi kunahitajika utumizi wa lugha bayana (referential language), lugha inayotoa sifa na maelezo yaliyo halisi na ya waziwazi. Kwa mfano, mhadhara darasani juu ya matatizo ya ulevi hauwezi kubadilishwa kichwa cha habari na kutumia nahau - matatizo ya kuvaa miwani kwa sababu nahau hailengi kweoye dhana inayokusudiwa mara moja, ina utata katika kuielewa. Hapa tunataka lugha iliyo bayana na wazi kabisa.
Kwa upande mwingine hali ya uchaguzi wa zana za kiisimu inabadilika kabisa iwapo mawasiliano yanahusu shnghuli za kisiasa. Tuangalie kwa mfano mwanasiasa mashuhuri anapohutubia mkutano. Hapa itambidi atumie lugha ya kuvutia sana na iliyopambwa vizuri kwa nahau, methali, mafumbo, misimu, maelezo kwa kutumia mifano na ulinganisho mbalimbali, tasfida, sitiari... n.k. ili kuwafanya wasikilizaji wavutiwe na waifurahie hotuba na kuisikiliza kwa makini. Isitpshe lazima mhutubiaji aonyeshe maono na msimamo wake kuhusu jambo analolizungumzia, upande anaouunga mkono na kujaribu kadiri awezavyo kuwavutia wasikilizaji upande wake. Kwa hali hii uchaguzi wa msamiati na mpangilio wa maneno katika sentensi utatakiwa ukidhi haja zilizoorodheshwa hapo juu. Hii ina maana kwamba mfumo wa “muni” (ingawa “muni” hiyo inaweza kuwa kwa niaba ya kundi fulani la watu au chama) unatumika sana katika shughuli za kisiasa. Rejea, kwa mfano, hotuba zinazotolewa na wagombea viti vya ubunge wakati wa kampeni za uchaguzi. Wanasiasa wengi hntumia mtindo huu, k.m.
Wananchi! kama mtanichaguamimi, basi nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu kuyatatua matatizo yetu. Shida zetu nazijua kwani nami ni mkazi wa wilaya hii...
Sasa ingefaa tuzitaje kazi au shughuli muhimu za jamii. Kusema kweli shughuH za jamii zinaweza kuwa nyingi sana, laldni wataalam weagi wa elimumitindo (k.m. Kozhina 1977:37, Krilova 1979:36) wamejaribu kuziunganisha shughuli hm katika mafungu matano makubwa:
1. taaluma/sayansi,
2. sheria na utawala,
3. shughuli za kijamii na kisiasa(social and political activities),
4. sanaa na fasihi,
5. shughuli (za nyumbani) za kawaida za kila siku.
Kuna swali moja muhimu linalojitokeza hapa. Je, ni sifa gani kati ya zile zilizo yakini ambayo tunaweza kusema ni muhimu knzidi nyingine zote katika ujenzi wa mitindo? Jibu la swali hili lina umuhunu mkubwa sana kwani litatusaidia kujua idadi ya initindo katika lugha.
Iwapo tutasema kuwa njia za utekelezaji wa mawasiliano ndiyo sifa iliyo muhimu zaidi, basi itabidi tukubali kwamba katika lugha idadi ya mitindo iko sawa na idadi ya njia za kutekeleza mawasiliano - yaani mlrili: “mtindo wa maandiko” na “mtindo wa mazungnmzo”. Kama namna ya mazungumzo tutaichukulia kuwa sifa yenye uzito zaidi kuliko sifa yakini nyinginezo na kwamba sifa hii ndio inayojenga mitindo, basi tutakuwa na mitindo mitatu na sio miwili na itakuwa tofauti kabisa na ile miwili ya mwanzo. Yaani tutapata “mtindo wa mazungumzo ya mtu nunoja”, “mtindo wa mazungumzo ya watu, wawili” na “mdndo wa mazungumzo ya watu wengi”.
Hivyo ili kuipata mitindo iliyomo katika lugha sharti tupate uamuzi juu ya sifa iliyo muhimu zaidi inayoathiri ujena wa nutindo hiyo. Sifa hiyo, kwa kulingana na maoni ya wanamitindo wengi wa mtazamo wa mitindo kufuatana na utendaji wa lugha, ni kazi au shughuli za jamii.
Kusema kweli nutindo ni nufumo ya zana za kiisimu inayoambatana na kazi au shughuli muhiniu za jamii - kila mtindo ukiihudumia kazi au shughuli moja maalum ya jamii:
1. shughuli za kisayansi - mtindo wa mambo ya kitaaluma,
2. shughuli za kisheria na kiutawala - mtindo wa kirasimu,
3. shughuli za kijamii na kisiasa - mtindo wa magazetini na shughuli za kisiasa,
4. shughuli za kawaida za kila siku - mtmdo wa mawasiliano yasiyo rasmi.
Kama inavyoonekana sifa ya “kazi au shughuli za jamii” si sifa ya kiisimu. Lakini katika kuigawa na kuipambanusha mitindo mbalunbali ya lugha ni muhimu na yatubidi kutafuta sifa za kiisunu ili kukidhi haja hiyo. Hii ina maana kwamba kama kuna mtindo mmoja ambao unaihudumia kazi au shughuli moja maalum ya jamii, basi katika mtindo huo kutajitokeza namna fulani ya maneno, msamiati, miundo ya sentensi, hali fulani ya lafudhi... n.k. ambayo hujikita (hujishamirisha) na kuanza kutumika zaidi katika mtindo huo. Yaani kunatokea kitu kama “mihuri” fulani ya kiisimu ambayo ni lazima itumike zaidi katika mawasiliano yahusuyo kazi au shughuli husika ya janui. “Mihuri” hii itajikuta kuwa si mahala pake iwapo itatumika katika mawasiliano yahusuyo nyanja nyingine za kazi za jamii.
Kwa mfano, miundo ya sentensi nyingi zinazotumika katika mtindo wa mawasiliano yasiyo rasmi ni ya mikato (yaani inaruhusu kukatiza sentensi) ambapo kwenye mtindo wa mambo ya kitaaluma kwa kawaida hutumika sentensi zilizo kamilifu - zenye kiima na prediketa. Hali kadhalika lafudhi ya kuchekesha ya akina “Pwagu na Pwaguzi” tunayoisikia kwenye redio itajikuta kuwa si mahala pake iwapo itatumiwa kwa mfano, na mtoa hoja bungeni. (Linganisha vile vile utofautiano wa lafudhi ya “uncle J. Nyaisanga” kwenye kipindi cha Klabu Raha Leo Shoo na ile ya “Julius Nyaisanga” wakati anaposoma Taarifa ya habari).
Zana maalum za kiisimu zinazotumika mara kwa mara katika mawasilaino yahusuyo shughuli fulani za jamii huonekana kama kwamba zina “kivuli” maalum kimtindo. Na kivuli hiki kinaweza kuhisika hata kama zafla hiyo itasimama peke yake (bila kutumika katika sentensi) au iwapo itatumika mahala pasipo pake kimtindo. Kwa mfano, ni wazi kabisa kwamba maneno kama “chauchau”, “daladala”, “sanyasanya”, “mitumba”, “so” n.k. yana hali fulani ya kivuli cha mtindo wa mawasiliano yasiyo rasmi, yawe yametumika katika sentensi au hata kama yamesimama pekee. Kwa hiyo itakuwa ni makosa kwa namna fulani kimtindo kuyakuta maneno haya katika mitindo mingine, mathalani mtindo wa kirasimu. Kwa mfano, hatuwezi kusema: “Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ameidhinisha Sehemu ya Kamusi kupewa so kumi (yaani shilingi elfu moja) kwa ajili ya kununua kamusi za marejeo” wakati wa kutoa ripoti kwenye mkutano wa Wakuu wa Sehemu. Vivyo hivyo neno “ndugu” lina kivuli cha mtindo wa kirasimu na si kawaida mtu nyumbani kwake, wakati wa maongezi na mke na watoto wake kulitumia. Kumwita mke nyumbani “Ndugu mama Zuberi!” ni kulitumia neno “ndugu” mahali pasipo pake kimtindo. Na hili ni kosa.
Hivyo basi kwa kuzingatia mambo yote tuliyoyajadili hapo juu tunaweza kuifasiri mitindo kama mifumo ya zana za kiisimu inayotokana na maendeleo ya kukua kwa lugha ambayo hutofautiana kufuatana na kutumiwa kwake katika mawasiliano yahusuyo nyanja mbalimbali za kazi au shughuli muhimu za jamii.
Kulingana na fasiri hii tunaweza kuigawa mitindo ya lugha ya Kiswahili (na lugha yoyote nyingine) katika makundi yafuatayo:
1. mtindo wa kitaaluma,
2. mtindo wa kirasimu,
3. mtindo wa magazetini na shughuli za kisiasa,
4. mtindo wa mawasiliano yasiyo rasmi.
Pamoja na hayo yote kuna suala moja ambalo limekuwa likileta kero na mabishano makali sana baina ya wataalam wengi wa elimumitindo, nalo linahusu kuwepo au kutokuwepo kwa mtindo maalum unaotumika katika fasihi (yaani maandishi ya kisanii kama vile riwaya, tamthilia, mashairi, tenzi, ngonjera, hadithi fupi... n.k.). Baadhi ya wataalam wanakubali kwamba mtindo wa shughuli za kifasihi upo kwa madai kwamba unahudumia nyanja maalum ya kazi za jamii - fasihi na sanaa. Lakini uchunguzi na upekuzi wa ndani zaidi wa suala hili umeonyesha kwamba iasihi haina mtindo maalum, bali hutumia mitindo yote minne tuliyoitaja hapo awali, tena kwa pamoja. Tena fasihi si lazima itumie kisanifu tu, bali hata lahaja, misimu na pengine hata lugha za kienyeji na za kigeni zinaweza kupenyezwa.