UHAKIKI WA RIWAYA YA ROSA MISTIKA

UHAKIKI WA RIWAYA YA ROSA MISTIKA UHAKIKI WA RIWAYA YA ROSA MISTIKA Riwaya ya Rosa Mistika iliyoandikwa na E. Kezilahabi mwaka 1971, ni moja kati ya riwaya zinazotumika katika utafiti huu kama data ya msingi. Kwa kiasi kikubwa, masimulizi ya riwaya hii yamejikita katika kueleza maisha ya mhusika, Rosa, tangu akiwa mtoto mpaka kifo chake na maisha baada ya kifo. Masimulizi yamehusisha maisha ya wahusika wengine ambao kimsingi ndio ambao wamemjenga mhusika mkuu Rosa. Hivyo, katika utafiti huu, wahusika, Regina ambaye ni mama yake Rosa, Zakaria baba yake Rosa, Flora mdogo wake Rosa, Charles mpenzi wa Rosa na Padre anayetaka kuokoa nafsi ya Rosa, wamechambuliwa. Kwanza tunaona wasifu wa Rosa akiwa mtoto mdogo. Mwandishi anamchora Rosa kama kifungua mimba cha familia ya Zakaria na Regina kati ya wasichana watano na mvulana mmoja. Rosa akiwa mtoto mdogo anaonekana ni msichana mrembo na mwenye aibu, mrefu kiasi, mnyenyekevu na mkakamavu. Rosa ...