maana ya fonimu pdf

dhana ya fonimu Fonimu ni nini TUKI (1990:45) wanasema fonimu ni kipashio kidogo kabisa cha kifonolojia kinachobadili maana. Hyman (1975:59) yeye anasema fonimu ni kipashio kidogo kabisa cha sauti kinachoweza kutofautisha maneno yenye maana tofauti. Mfano: ‘bata’ kuwa ‘pata’. Fonimu inawakilishwa katika maandishi kwa kutumia alfabeti za kifonetiki katika mabano mshazali / /. 2.1.1 Historia ya Fonimu Dhana ya fonimu ina historia ndefu sana ambayo ilitokana na nadharia ya wanamuundo inayoitwa “nadharia ya fonimu”. Katika kuitalii historia hii tunaanza na asili ya istilahi ‘fonimu’ na kisha tutaangalia ‘nadharia yenyewe ya fonimu’. Kwa miaka mingi dhana ya fonimu ilikuwa katika akili za wanaisimu wa wakati huo lakini istilahi yenyewe iliundwa baadaye sana. Hata hivyo, wanaisimu wanatofautiana juu ya nani alianzisha istilahi hiyo na au kuipa fonimu dhana inayot6umika hivi leo. Jones (1957) anasema istilahi hiyo iliundwa na Baudouin de Courtenay. Robins (1967) naye anaunga mkono mawaz...