NADHARIA YA FONIMU

UTANGULIZI,

Dhana ya fonimu inahistoria ndefu sana. Na ilitokana na nadharia ya wanamuundo iliyojulikana kama nadharia ya fonimu.

Asili ya istilahi fonimu. 

Ingawa inawezekana kuwa dhana ya fonimu ilikuwamo katika mawazo ya wanaisimu na wanafilolojia wa zama hizo kwa miaka mingi  lakini istilahi yake iliundwa baadaye kabisa kama asemavyo Maasamba. Kwamujibu wa Jones (1957)  istilahi hii iliundwa na Baudouin de Courtenay, madai hayo ya Jones yanaungwa mkono na  Robins (1967:204) ambaye anaeleza kwamba katika kitabu chake cha theory of Phonemes  (yaelekea hii ni tafsiri ya baadaye) ambaco kimechapishwa  mwaka 1884 ambacho de Courtenay alitumia neno la Ki-Rus fonema kama istilahi,


Hata hivyo Firth (1957:1) anasema kwamba inaelekea de Courtenay aliliazima istilahi hiyo fonema kwa manafunzi wake Kruszewiski ambayo aliitumia katika insha yake  iliyokuwa na mada  ya “ athari za mkazo  katika ubadilishanaji wa irabu  katika Rig-Veda insha iliyochapishwa huko Kazan mnamo mwaka 1879. 

Hata hivyo wataalamu bado hawakubaliani  kuhusu muasisi wa istilahi hiyo kwamfano baadhi ya wataalamu wengine wanadai kuw aistilahi hiyo iliundwa na  Dufriche –Desgenettes mnamo mwaka 1873 na kuitumia kama kibadala cha istilahi ya Ki-jerumani Sprachlaut “sauti ya usemaji”  hata hivy nilazima tukubaliane  kuwa wazo la fonimu  nilazima lilikuwamo  katika fikra za wanafonetiki na wanaortografia ambao kwa namna Fulani  walitumia unukuzi mpana wa sauti.


Kwavyovyote vile kuhusu istilahi fonimu Kramsky (1874)  anaelekea kutupa historia ambayo ina muoano mzuri ambapo kwa mujibu wa maelezo yake mwanazuoni wakwanza kabisa kutumia istilahi hii  Fonimu alikuwa ni Dufriche Desgenettes katika mkutano wa societe de linguistique de paris (Chama cha isimu cha paris) 24/mei 1873.  Alipendekeza kutumia istilahi ya phoneme (fonimu)   ukiwa ni utohozi wa Ki-faransa  wa neno la Ki-giriki  lenye maana ya sauti kama kisawe cha neno la kijerumani  sprachlaut.

Kwa mujibu wa kramsky mtu  wapili kutumia istilahi hiii  alikuwa ni Havet taz (havet “ol et Ul en francais, Romania 1874:321 kwa mujibu wa dondoo la Kramsky . aidha akimdondoa  Jakobson  (1871:396-397)  Kramsky anasema baada ya Havet istilahi hiyo ikatumiwa na De Saussure aliyeitumia istilahi hiyo kwa mtazamo wa kihistoria, kwani kwa mujibu wa de Saussure  hilo lilikuwa umbo la kidhahania lakifdonetiki ambalo lilisemekana kujitokeza mara kwa mara  katika faridi za kimofolojia za lugha zenye mnasaba mmoja. Umbo ambalo lasemekana kutokana na mame-lugha moja.

Kramsky anadai kwamba  baada ya de ssausure  istilahi fonimu ikatumiwa na  Kruszewski (1851-1887)  kruszewski alikiuwa mwanfunzi wa de Courtenay  ambapo Kramsky anasema pia katika mwaka 1880 Kruszewski alichapisha tahakiki ya Memoire sur le system primitive des voyelles dans languages indoeuropeennes ambayo ilikuwa imeandikwa na de Saussure  katika chapisho lake hilo istilahi fonimu ilitumika kwa mara ya kwanza  katika msamiati wa Ki-slavu.

Kwa mujibu wa wa maelezo ya Kramsky, Kruszewski alipotumia istilahi hiyo aliitolea maelezo maalumu yaliyoelekeza kwamba istilahi hiyo  ilikuwa na faida ya kutofautisha sauti kama faridi ya kifonetiki na sauti kama tukio la kifiziolojia. Kisha mnamo mwaka 1881 Kruszewski  akaeleza wazi kwamba  alikuwa napendendekeza  kuitumia istilahi fonimu kwa maana ya faridi ya kifonetiki ambayo haiwezi kugawanyika tena  pasi na kupoteza uamilifu wake. 

Tukizingatia maelezo haya ya Kramsky  tutaona kwamba  Kruszewski  aliichukua istilahi hii  katika makala hayo ya Memoire ya de Saussure (siyo katika maandishi ya baadaye ya de Saussure  ambamo  analitumia neno hilo akimaanisha  “sauti za lugha” )  na kulitumia kwa matumizi yake ya wakati huo. Kwahiyo nimuhimu tukasema hapa kwamba ingawa kruszewski hakutoa fasili ya nono hilo lakini angalau alilipa fahiwa mpya. 

Kama asemavyo Maasamba akimnukuhu Anderson (1985:67) de Courtney  ndiye ambaye angalau alijaribu kufasili  dhana ya fonimu. Kwa de Courtney fonimu, za lugha ni, vibadala vya mwisho kabisa vya muundo wa sauti, kisaikofonetiki  fasili hii ipo karibu na fasili ya fonimu ilivypochukuliwa baadaye.