TANGA RAHA SEHEMU YA 50

AGE………………18+ WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA ILIPOISHIA Niliwauliza baada ya kuona mshangao wao unazidi, kidole kimoja cha nesi mmoja kikaniashiria nigeuke nyuma yangu kuangalia kitu kinacho toka kwenye droo nililo lifungua.Nikageuka kwa haraka, sikuamini macho yangu, hii ni baada ya kukutana na mtu niliye fanana naye kuanzia juu hadi chini, isitoshe nguo zake na zangu zimefanana sana, jambo lililo nistua kupita maelezo.Akaanza kupiga chafya nyingi, nikastukia kishindo nyuma yangu, nikageuka na kumkuta nesi mmoja akiwa ameanguka na kupoteza fahamu huku mlinzi naye akifwatiakuanguka na kukaa kimya “Mambo Eddy” Jamaa alinisalimia, na sauti yangu inafanana sana na sauti yangu, nikabaki mdomo wazi nisijue nini nimjibu ENDELEA Jamaa akatoka kwenye droo ya kuhifadhia maiti na kusimama karibu yangu, mwili mzimwa ukaanza kunitetemeka kwa maana katika maisha yangu sijawahi kukutana na vihoja kama hivi japo kuna matukio mengi ya kutisha yalisha wahi kupita kipindi cha nyuma ila...