Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), yashusha gharama za kupiga simu kutoka shilingi 26.96 kwa dakika moja hadi shilingi 15.60 kuanzia 2018. Mkurugenzi wa TCRA James Kaliba amesema kuwa gharama hizo zitaendelea kupungua kadiri miaka inavyozidi kwenda kama ambavyo imeanishwa hapa. Gharama za mwingiliano zitakazotozwa kwa dakika na mwaka kwenye mabano ni Sh15.60 (Januari Mosi, 2018), Sh10.40 (2019), Sh5.20 (2020), Sh2.60 (2021) na Sh2.00 (2022). Viwango hivyo vimepungua kulinganisha na miaka mitano iliyopita ambayo gharama zake za mwingiliano zilizokuwa zikitozwa kwa dakika na mwaka wake kwenye mabano ilikuwa Sh34.92 (2013), Sh32.40 (2014), 30.58 (2015), Sh28.57 (2016) na Sh26.96 (2017). Hata hivyo amesema kuwa kampuni za simu zimekuwa na kigugumizi kukubaliana na viwango hivyo na kuingia mikataba ya mwingiliano kwa sababu ya masilahi ya kibiashara hivyo TCRA ililazimika kuingilia kati na kuvipangia kwa kufuata utaratibu kama ilivyoainishwa katika sheria namba 12 y...