KUMRADHI: Tunaomba Radhi kwa kutoa Habari hii isiyo ya kweli


Tunaomba Radhi kwa familia ya mzee kingunge kwa kuandika habari zisizoB

sahihi kuhusu Mzee wetu mpendwa mzee Kingunge.


Habari za kweli ni hizi..

MTOTO WA MZEE KINGUNGE AKANUSHA TAARIFA ZA KIFO CHA BABA YAKE ZINAZOSAMBAA MITANDAONI..

Mtoto wa mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombae Mwiru,Tonny Ngombale Mwiru amekana taarifa zinazozagaa mitandaoni kuhusu kifo cha baba yake mzee Kingunge Ngombale Mwiru.

Tonny amefanya mahojiano na waandishi wa habari jioni ya leo na kuwaeleza kuwa baba yake yuko hospitali akipata matibabu baada ya kung’atwa na mbwa hivyo kupata majeraha Kwenye miguu ambayo ndiyo anayouguza hospitalini kwa sasa.

Kuhusu mazishi ya mke wa mwanasiasa huyo ambaye alifariki jana katika hospitali ya Muhimbili Tonny Ngombale Mwiru amesema familia itatoa taarifa mapema kesho baada ya baba yao mzee kingunge kuelezwa na kutoa maelekezo kama baba mzazi na kiongozi wa familia hiyo.

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?