900 wasimamishwa shule, kisa binti mmoja


KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, karibu wanafunzi 900 wa Shule ya Sekondari Kabale katika Manispaa ya Kabala nchini Uganda wamesimamishwa masomo kutokana na vurugu kubwa zilizoibuka shuleni hapo, chanzo kikielezwa ni kumgombea kimapenzi binti mmoja ambaye pia ni mwanafunzi shuleni hapo.

Wanafunzi hao waliibua vurugu kubwa na kuanza kupigana mchana wa Ijumaa iliyopita shuleni hapo. Inaelezwa kuwa, mwanafunzi wa kidato cha sita aliomba kuwa na uhusiano na binti ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi mwingine wa kidato cha nne.

Kutokana na kuvuja kwa taarifa hizo, makundi mawili ya wavulana hao yaliibua uhasama ulioishia kupigana. Ugomvi huo haukuishia kwa wanafunzi tu, waliharibu pia mali za shule na hata za majirani wanaoishi karibu na shule hiyo.

Kutokana na hali hiyo, jeshi la Polisi lililazimika kuingilia kati kutuliza ghasia kwa kutumia mabomu ya machozi na silaha nyingine kutawanya wanafunzi hao. Kaimu Ofisa anayeshughulikia usalama wilayani Kabale, Kenneth Birungi amethibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kuongeza kuwa, timu ya wanausalama baadaye ilikutana na uongozi wa shule na kukubaliana kuwasimamisha masomo wanafunzi hao, huku Bodi ya Shule ikitarajiwa kutoa uamuzi juu ya hatima yao.

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?