UMEISIKIA AHADI YA KAGERE MICHUANO CAF

MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere amefunguka kuwa atahakikisha anapambana kufa na kupona kwa kuwafunga wapinzani wao, TP Mazembe katika mchezo wa marudio kwa kuwa anataka kutimiza ndoto yake ya kutwaa kiatu cha ufungaji bora Afrika. Kagere mwenye mabao sita akizidiwa bao moja na mshambuliaji wa Al-Nasr ya Libya, Moataz Al-Mehdi, ameyasema hayo kufuatia mchezo wa mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Hatua ya Robo Fainali dhidi ya TP Mazembe ambao utapigwa kesho Jumamosi, Lubumbashi nchini DR Congo. Kagere alisema amejipanga kupambana mwanzo mwisho kwa kuhakikisha Simba inafanikiwa kushinda mchezo huo huku yeye akitimiza ndoto yake ya kuwa mfungaji bora Afrika kutokana na mtu anayemzidi mabao timu yake kutolewa. “Najua huu mchezo utakuwa mgumu lakini sisi tunakwenda kufuata ushindi kwa sababu ni jambo ambalo linawezekana kwetu, maana wachezaji wote tunaelewa umuhimu wa mchezo huo, sisi hatuangalii mechi zilizopita lakini watu wanatakiwa kuelewa kwamba hii ni robo faina...