kubainisha alofoni na mifano ya alofoni
Kigezo cha mfanano wa kifonetiki ni mojawapo ya vigezo muhimu katika kucbunguza ikiwa sauti zinazotokea katika lugha ni alofoni za fonimu. Pamoja na mfahano wa kifonetiki, kigezo kingine, na cha lazima ni mazingira ya kifonolojia sauti hizo zinamotokea. Katika mfano wa Kiingereza uliotolewa hapo nyuma (7a and b), ilionyesbwa kuwa utokeaji wa alofoni [t] na [th] za fonimu /t/ unategemea mazingira maalumu. Alofoni [t] hutokea wakati fonimu /t/ inapotanguliwa na konsonanti nyingine, kama [s], ambapo alofoni [th] hutokea mwanzoni mwa neno. Tulisema kuwa sauti hizi haziingiliani katika mazingira yao. Hakuna wakati ambapo alofoni [th] itatokea baada ya sauti [s], au alofoni [t] kutokea mwanzoni mwa neno. Sauti hizi ziko katika uhusiano wa mgawo-kamilishi. Maana yake ni kuwa hizi sauti zinagawana mazingira ya utokeaji wao katika maneno ya Kiingereza; na kuwa ukijumlisha mazingira kila moja inamotokea, unapata ujumla wa matamshi ya fonimu /t/ katika lugha hii. Kwa maneno meng...