Kigezo cha mfanano wa kifonetiki ni mojawapo ya vigezo muhimu katika kucbunguza ikiwa sauti zinazotokea katika lugha ni alofoni za fonimu. Pamoja na mfahano wa kifonetiki, kigezo kingine, na cha lazima ni mazingira ya kifonolojia sauti hizo zinamotokea. Katika mfano wa Kiingereza uliotolewa hapo nyuma (7a and b), ilionyesbwa kuwa utokeaji wa alofoni [t] na [th] za fonimu /t/ unategemea mazingira maalumu. Alofoni [t] hutokea wakati fonimu /t/ inapotanguliwa na konsonanti nyingine, kama [s], ambapo alofoni [th] hutokea mwanzoni mwa neno. Tulisema kuwa sauti hizi haziingiliani katika mazingira yao. Hakuna wakati ambapo alofoni [th] itatokea baada ya sauti [s], au alofoni [t] kutokea mwanzoni mwa neno. Sauti hizi ziko katika uhusiano wa mgawo-kamilishi. Maana yake ni kuwa hizi sauti zinagawana mazingira ya utokeaji wao katika maneno ya Kiingereza; na kuwa ukijumlisha mazingira kila moja inamotokea, unapata ujumla wa matamshi ya fonimu /t/ katika lugha hii. Kwa maneno mengine, matamshi haya tofauti ya fonimu /t/ yanakamilishana.

Uhusiano uliopo hapo juu kati ya vipasuo sighuna pumuo na sipumuo katika Kiingereza, ni wa jumla kwa sauti zote zenye sifa kama hizo; hivyo uhusiano kama huo upo pia kwa fonimu /k/ na /p/ kama inavyoonyeshwa katika maneno yafuatayo:

13 a) [khil] {kill} : [skil] {skill}
b) [phil] {pill} : [spil] {spill}.

Mfano mwingine unaoonyesha mgawo-kamilishi unaonekana katika utokeaji wa irabu sing’ong’o na ng’ong’o katika Kiingereza. Kwa kawaida irabu katika lugha hii ni sing’ong’o. Lakini katika mazingira maalumu ya utokeaji, irabu hizi hupata sifa ya ung’ong’o kama katika maneno yafuatayo:

14 a) [bid] {bead} : [bîn] {bean}
b) [les] {lace} : [lêm] {lame}
c) [baed] {bad} : [baeh] {bang}

Katika mifano hiyo, inadhihirika wazi kuwa irabu ng’ong’o hutokea tu ikiwa zinafuatwa na konsonanti ng’ong’o, mahali pengine pote irabu huwa sing’ong’o. Hivyo tunasema kuwa ‘katika Kiingereza, irabu sing’ong’o na ng’ong’o zinazohusiana katika sifa nyingine zote ziko katika mgawo-kamilishi’. Katika mifano iliyotolewa hapo juu:

fonimu /i/ inazo alofoni [i] na [î]
fonimu /e/ inazo alofoni [e] na [ê]
fonimu /ae/ inazo alofoni [ae] na [ae].

Katika kujumuishahayo tuliyosema mpaka hapa, yafuatayo ni baadhi ya mazingira ya kifonolojia yanayoweza kutawala utokeaji wa alofoni za fonimu moja:

i) mahali fonimu inapotokea katika neno au katika silabi;
ii) sauti inayotangulia au kufuata;
iii) uhusiano na shada au mkazo katika neno;
iv) mchanganyiko wa zaidi ya moja ya hayo matatu.

Katika sehemu iliyotangulia tuligusia baadhi ya sauti ambazo tulisema zikitokea katika lugha moja, kuna uwezekano wa sauti hizo kuwa na uhusiano wa kialofoni, na hasa ikiwa hakuna jozi-sahili zinazoweza kusaidia kutofautisha sauti hizo. Zifuatazo ni baadhi ya sauti ambazo zinaweza kutiliwa mashaka, na hivyo kumtahadharisha mchunguzi kuwa mwangalifu:

15 a) sauti ghuna na sighuna zinazoshiriki mahali pa kutamkia kama [b:p] [g:k], [d:t], [z:s], [v:f], n.k.

b) vipasuo na vikwamizi vinavyochangia mahali pa kutamkia kama [d:d], [t:q]...

c) vipasuo na vikwamizi au ving’ong’o vya mdomo na vile vya mdomo-meno kama [p:f], [b:v]...

d) vikwamizi vya ufizi na vya kaakaa gumu: [s:Å¡], [z:]...

e) vipasuo pumuo na sipumuo: [ph:p], [th:t]...

f) ving’ong’o (ingawaje mara nyingi [m] ikiwepo huwa ni fonimu pekee na haiingii katika uhusiano wa kialofoni na sauti ng’ong’o nyingine).

g) vilainisho (vimadende): [r:l].

h) viyeyusho: [j:w].

Hizi ni baadhi tu ya sauti zinazoweza kutiliwa mashaka. Katika hali halisi ya kuchunguza mifumo-sauti ya lugha, kuna tofauti nyingi zinazoweza kujitokeza, na ni vigumu kutoa mahitimisho kamilifu kuhusu sauti zinavyojitokeza katika lugha maalumu bila kuangalia mfumo mzima wa lugha hiyo.

Ingawa kigezo cha mgawo-kamilishi ni cha uhakika zaidi katika kutambua alofoni, inawezekana kuwa hata baada ya kupata sauti zote ambazo ziko katika mgawo-kamilishi, na kuainisha fonimu za lugha husika kwa kutumia kigezo cha jozi-sahili, n.k. bado kukawa na sauti ambazo hadhi yake si wazi katika mfumo mzima wa lugha hiyo. Hizi ni sauti ambazo mchunguzi anaweza kuzisikia wazungumzaji wakizitamka, lakini hana hakika ikiwa zinatofautisha maneno ya lugha hiyo. Katika kuchunguza tabia za utamkaji za wazungumzaji, anagundua kuwa wazungumzaji hawazioni kuwa sauti hizo ni tofauti, ingawa yeye anazisikia kuwa ni tofauti kifonetiki. Turudie mfano wa (2) tuliotoa mwanzo wa sauti [t] na [th] katika Kiswahili. Tuliona kuwa sauti hizi hazitofautishi maneno ya lugha hii, na wala wazungumzaji hawazihisi kuwa ni tofauti. Hivyo katika neno hilo hilo mzungumzaji anaweza kutamka mojawapo ya sauti hizi bila kubadili maana ya neno hilo. Kifonolojia tunasema kuwa sauti hizi ni alofoni za fonimu moja, na kuwa ziko katika uhusiano wa mpishano-huru. Maana yake ni kwamba alofoni hizo zinatokea katika mazingira yaliyo sawa, lakini haziundi maneno tofauti kama fonimu zifanyavyo, na wala haziwezi kuunda jozi-sahili. Hivyo tunasema kuwa katika Kiswahili Sanifu vipasuo sighuna sipumuo na pumuo viko katika uhusiano wa kialofoni wa mpishano-huru. Kwa kawaida, katika kuandika kanuni za fonolojia ya lugha inayochunguzwa, alofoni za namna hii hazipewi umuhimu kama zile ambazo ziko katika uhusiano wa mgawo-kamilishi.