Kutoka kwa moja ya wasomaji wetu

Kilio cha haki

Na Mwandishi wetu.

Ni dhahiri kuwa, mawasiliano kwa njia ya simu yamerahisisha ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi. Katika hatua hii, yapo mambo yanayotumika kinyume na lengo lililokusudiwa ambapo wapo baadhi ya watu wenye kutumia mawasiliano kwa njia za kiuhalifu na kupeana mbinu hasi zenye kujenga chuki, umasikini, hofu na visasi.





Kutoka kwa moja ya wasomaji wetu


Kwa sasa hapa nchini wapo baadhi ya watu wenye kutumia mawasiliano ya simu kutapeli na kuwahadaa watu kwa lengo la kufanya uhalifu ama kutekeleza dhamira ovu, jambo ambalo linapaswa kukemewa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
lakini ajabu ni kwamba vyombo vinavyo husika vimeendelea kukaa kimya hadi hali iwe mbaya zaidi


Kutoka kwa moja ya wasomaji wetu


Simu za mkononi zimekuwa zikitumika sana sio tu kwa ajili ya mawasiliano (kupiga, kupokea ama kutuma ujumbe mfupi wa maneno), bali pia zimekuwa zikitumika kama nyenzo ya kufanyia miamala mbalimbali ya kifedha, mitandao ya kijamii kama whatsApp, Instagram, facebook na mambo mengi mengineyo.



Kutoka kwa moja ya wasomaji wetu


Kutokana na kuimarika kwa matumizi ya simu kwenye miamala ya kifedha, wahalifu nao wamekuwa wakiitumia fursa hiyo katika kufanikisha malengo yao ya kuwaibia watu fedha zao.





Wahalifu hao wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali katika kuwaibia watu ikiwamo kuwapigia simu na kujifanya watu fulani ambao wanataka kufanya biashara na wewe hivyo muwasiliane kwa ajili ya kufanya miamala ya kifedha.

Na kwamba ili kukamilisha biashara hiyo, unahitajika kutuma kiasi fulani cha fedha na ukituma fedha hiyo inakuwa tayari umeshaibiwa.

Mbali na mbinu hiyo, wapo pia wanaoiba simu za watu na kuzitumia simu hizo kuwaibia hela ndugu na jamaa wa mwenye simu kwa kuwatumia ujumbe mfupi wa maneno kuwa mwenye simu ana shida ya kiasi fulani cha fedha na alipo hawezi kupokea ama kupiga simu hivyo umjibu kwa meseji.

Hapa hata ukiwa mjanja utajikuta umeingia kingi.

Watu wengi wameshakutana na wizi wa mitandao aidha wao wenyewe ama jamaa zao na wengi wamekuwa wakiishia kulalamika bila kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika.

Pengine ni kutokana na kutofahamu nini cha kufanya au wengine kwa kufahamu ila hawaoni umuhimu wa kuchukua hatua za kisheria kwa kuripoti matukio hayo katika vituo vya Polisi
Kwa sasa kero kubwa imehamia upande wa SMS ,pengine wahalifu hao hujifanya waganga wa jadi , au kukutumia akikutaka umtumie fedha kana kwamba alikuwa akikudai ukijichanganya imeenda




Swali la kujiuliza ni kuwa je mitandao ya simu haina kitengo cha filter SMS , ili waweze kuzuia Meseji za kihalifu zinazotumwa kwa muundo mmoja kwa watu wengi ?

Au je ni marangapi mitandao hiyo imewatahadharisha Wateja wake kuhusiana na utapeli wa kimtandao?






Rai yangu kwa mitandao ya simu ni kushirikiana na Wateja wake kuwapatia elimu na jumbe za tahadhari ili kuhakikisha Wateja wao wanakuwa makini

Aidha washirikiane na jeshi la polisi kwani

Jeshi la Polisi lina kitengo kinachoshughulikia masuala ya uhalifu wa mitandao (Cyber Crime). Kitengo hiki kinao utaratibu wa kufanya doria za mitandao ikiwa ni pamoja na kupambana na wahalifu wanaowabaini kujihusisha na uhalifu kwa njia ya mitandao.


Wanao husika na washika dau wote naamini hili mtalifanyia kazi ili watumiaji wa Huduma za simu waondokane na kero hii



Kutoka kwa moja ya wasomaji wetu
Aidha watumiaji wa simu wanao endelea kupokea kero hii ni muhimu kutoa malalamiko kwa jeshi la polisi ili kukomesha tabia hii