Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema njia ya kusafirisha nishati hiyo ya Ilala -Kurasini itazimwa kwa muda kupisha matengenezo ya dharura.

Taarifa ya Tanesco iliyotolewa leo Jumamosi Januari 27,2018 kwa wateja wa Mbagala, Kurasini na Bandari imesema njia hiyo itazimwa kwa muda wa saa tatu kuanzia saa nne asubuhi.

Maeneo yatakayo athirika yametajwa kuwa ni yote ya Mbagala, Kurasini na Bandari.

Tanesco imewatahadharisha wananchi kutoshika waya uliokatika.