Michuano ya Kombe la Mapinduzi itaendelea Alhamisi ya Januari 04 2018 kwa michezo mitatu kufanyika kwenye uwanja wa Amaan Visiwani Zanzibar ambapo Simba na Yanga watajitosa uwanjani. 
Mchezo wa kwanza utakuwa wa kiporo kati ya Taifa Jang'ombe dhidi ya Singida United mchezo ambao utafanyika saa 8.30.
 Aidha mchezo huo ambao ulilazimika kuhairishwa Baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza kufuatia mvua kubwa  ilionyesha na kusababisha uwanja wa Amaan kujaa maji ambapo Singida United walikuwa wakiongoza mchezo huo kwa mabao 3-0.
 Saa 10.30 jioni itakuwa zamu ya Mabingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bars Yanga SC dhidi ya wapinzani wao JKU ya kutoka Visiwani Zanzibar huku Sumba SC wakikabiliana na timu ya Jamuhuri katika mchezo ambaoao utafanyika saa 2.15 usiku.
Katika mchezo mwingine uliofanyika Jumatano ni URA ya Uganda waliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mwenge Fc.