UTANGULIZI.

Niukweli usiopingika kuwa pamoja na kutofautiana kwa baadhi ya sifa mbalimbali za  lugha zipo sifa majumui ambazo huweza kupatikana katika lugha zaidi ya moja

Sifa hizo za lugha huweza kugawanywa katika makundi matatu ambayo ni , 

Sifa majumui halisi za lugha

Sifa majumui pana za lugha

Sifa majumui tabirifu za lugha.

Kwa kuzichanganua zifa hizo nikama ifuatavyo,

     SIFA MAJUMUI HALISI ZA LUGHA.

Hizi nizile sifa ambazo ni za kawaida na  hupatikana katika lugha zote halisi za binadamu  kwamfano katika lugha zote za binadamu huwa na irabu [a]  katika orodha ya sauti zake , katika utaratibu wa lugha zote asilia za binadamu huwa na utaratibu wa irabu na konsonanti,  ingawa kwa habari ya idadi ya irabu na konsonanti huweza kutofautiana baina ya lugha moja na nyingine. Vilevile katika lugha zote za asilia  irabu na konsonati hupangiliwa katika silabi.


SIFA MAJUMUI ZA LUGHA PANA.

Hizi ni zile sifa ambazo hupatikana katika lugha nyingi, ingawa sii zote, kwamfano, wana isimu wanakubaliana kuwa  lugha nyingi za binadamu zina angalau irabu tano, pamoja na hayo kuna lugha nyingine zina irabu saba au nane , pia kunalugha nyingine zenye irabu tatu tuu.

SIFA TABIRIFU ZA LUGHA, Hizi nizile sifa ambazo wanaisimu wanakubaliana kuwa , kuna mazingira ambayo kutokea kwa sauti flani katika lugha kunaashiria au kunatabiri kutokea kjwa sauti au irabu nyingine ambazo huambatana pamoja. Huo ndio utabirifu unaotajwa. 

Katika fonolojia za lugha nyingi, konsonanti na irabu, ni sifa za msingi, Aidha katika lugha nyingi imedhihirika kwamba kutokea kwa baadhi ya sauti  huwa kunaashiria kuwa sauti nyenzie (yani zinazofanana au kuendana nazo)  pia zitakuwepo.  Mara nyingi hutokea katika katika sauti ambazo zinmasifa za uziada.  Kwamfano kama  kunasauti [d} yenye sifa ya ziada [+ ghuna] basi kutatabiri uwepo wa sauti ya kinyume cha [t] yenye sifa ya [-sighuna] hata hivyo ieleweke kuwa sio katika  lugha zote hali hii hutokea kwani kunalugha nyine kama  Ki- fini, kikorea  na kipiute  ambazo zina konsonanti ambazo si ghuna  lakini hazina kinyume chake.


Mfano mwingine tunaweza kuona kuwa lugha zenye toni. Yani tukigundua lugha hiyo ina toni juu, tuna weza kutabiri kuwa lugha hiyo ina sauti za toni chini.  Pia tutagundua kuwa lugha hiyo ina toni panda  na toni shuka.


Mpaka kufikia hapa naamini kuwa kwa msomaji yeyote Yule makini atakuwa mefahamu kwa undani kuhusu kuwepo kwa sifa majumui za lugha katika fonolojia ya lugha.

Soma zaidi

Chapisho la maasamba fonolojia ya lugha

Emanuel.Gaspa  masshele 2022 (mwandishi) wa chapisho hili