Mifumo Tofauti ya Fonolojia

Tumesisitiza tokea mwanzo kuwa kila lugha inachagua baadhi tu ya sauti zinazoweza kutolewa na viungo-sauti vya mwanadamu. Na hata ikitokea kuwa kiuchunguzi lugha mbili zinatumia sauti zinazofanana, (yaani zenye sifa sawa za kifonetiki), zinaweza kutofautiana katika jinsi sauti hizo zinavyotumika katika lugha hizo. Kwa biyo ni kawaida kutarajia kuwa lugha zitakuwa na mifumo tofauti ya fonolojia. Hapa, isieleweke kuwa tunasisitiza mno tofauti kuliko mfanano. Ikiwa msisitizo unajitokeza, ni kwa tahadhari tu, kwa sababu hata wachunguzi (wanaisimu) wanaathiriwa na mazoea. Kwa mfano, ikiwa mchunguzi amezoea tofauti fulani katika sauti za lugha yake, ni rahisi kufikia hitimisbo la haraka akikuta sauti zinazofanana na za lugha yake katika lugha anayocbunguza, kwa sababu atakuwa anahusisha sauti za lugha hiyo na zile za lugha yake mwenyewe. Anaweza kuona mfanano mahali ambapo pana tofauti, au kuweka tofauti mahali ambapo hapahusiki. Na hili sijambo la kustaajabisha, kwa sababu viungo-sauti vya mwanadamu vyote vinafanana, kadhalika na jinsi za utamkaji. Hivyo ni lazima kutakuwa na mfanano mkubwa, si kati ya sauti zinazotolewa tu, lakini pia katika sulubu zinazojitokeza za sauti hizo katika lugha tofauti. Katika mifano ifuatayo, itadhihirika kuwa mambo yote mawili huenda sambamba, yaani mfanano na tofauti kati ya fonolojia za lugha.

Tulikwishaona jinsi kundi la sauti zenye sifa ya vipasuo sighuna linavyojitokeza katika lugha tatu: Kiingereza, Kipemba na KiThai. Katika sehemu iliyotangulia, tuliangalia tu kipasuo sighuna kimoja [t]. Sasa tunaweza kutoa picha kamili ya sauti hizi katika lugha zote tatu, na jinsi zinavyojitokeza. Katika mfano wa (13) tulitoa uhusiano wa sauti sighuna pumuo na sipumuo katika Kiingereza, na tukasema kuwa ni uhusiano wa mgawo-kamilishi. Tunaweza kusema kuwa lugha ya Kiingereza inazo fonimu tatu za vipasuo sighuna, na kila fonimu inazo alofoni mbili, moja pumuo, na nyingine sipumuo. Lugha za Kipemba na Kithai, kwa upande mwingine, kila moja inazo fonimu sita za vipasuo sighuna, kama maneno yafuatayo ya lugha hizo yanavyodhihirisha.

KiThai:

16

a)

/paa/

msitu

/phaa/

kupasua


b)

/tam/

kutwanga

/tham/

kufanya


c)

/kat/

kung’ata

/khat/

ingiliakati

Kipemba:

17

a)

/paa/

ezeko la nyumba

/phaa/

paa - mnyama


b)

/taa/

taa ya kuonea

/thaa/

aina ya samaki


c)

/kaa/

kaa la moto

/khaa/

kaa mnyama

Katika kielelezo, sauti hizo zitaonekana kama ifuatavyo katika lugha zote tatu:

Kiingereza

KiThai

Kipemba

18

a) /p/ ® [p, ph]

19

a) /p, ph/

20

a) /p, ph/


b) /t/ ® [t, th]


b) /t, th/


b) /t, th/


c) /k/ ® [k, kh]


c) /k, kh/


c) /k, kh/

Mfano wa pili unahusu irabu ng’ongo na sing’ong’o. Tulipokuwa tunajadili dhana ya mgawo-kamilishi, tulisema kuwa lugha ya Kiingereza inazo fonimu irabu zenye alofoni mbili kila moja: ng’ong’o na sing’ong’o (angalia mfano wa 14). Lugha ya Akan kwa upande mwingine, inazo fonimu irabu ng’ong’o na sing’ong’o kama inavyodhihirishwa na jozi zifuatazo za maneno ya lugha hiyo.

KiAkan.

21

a)

/ka/

ng’ata

/kâ/

sema


b)

/fi/

toka

/fî/

chafu


c)

/tu/

vuta

/tu/

shimo, pango


d)

/nsa/

mkono

/nsâ/

pombe


e)

/ci/

chukia

/cî/

kamua


f)

/pam/

shona

/pâm/

jumuika

Mifano hiyo inaonyesha wazi kuwa ung’ong’o katika irabu za lugha ya Akan ni sifa bainifu, ambapo katika irabu za Kiingereza ung’ong’o si sifa bainifu, kwa sababu katika Kiingereza kuna kanuni ya jumla inayoweza kutabiri utokeaji wa irabu sing’ong’o na ng’ong’o kama tulivyokwishaona.

Hata lugha ambazo zina uhusiano wa ‘kidugu’ zinaweza kutofautiana katika mifumo yao ya fonolojia. Mfano tutakaochukua ni wa vipasuo katika lugha mbili za kundi la lugha za KIBANTU, Kiswahili Sanifu na Kishambala. Lugha zote zinazo fonimu sita za vipasuo, na zinatofautisha kati ya vipasuo ghuna na vipasuo sighuna, kama ifuatavyo: /b, p, d, t, g, k/. Lakini lugha hizi pia zina fonimu nyingine za vipasuo zinazoandamana na ung’ong’o, na hizi tumeziita vipasuo-ng’ong’o, na katika fonimu hizi, lugha hizi mbili hutofautiana.

Orodha zifuatazo za maneno zinadhihirisha kuwa katika lugha ya Kishambala, kuna fonimu sita za vipasuo-ng’ong’o, mbali na zile ambazo ni sing’ong’o:

Kishambala:


Orodha A

Orodha B

22

a) bea

(beza)

23

a) mambeza

(uwongo)


b) pea

(kisamvu)


b) humpa

(homa)


c) dodoa

(okota)


c) ukando

(ukuta)


d) toa

(piga)


d) kanta

(vaa)


e) gea

(tia)


e) kungu

(mwamba)


f) kea

(kata(mti))


f) kunka

(beua)

Tofauti kubwa iliyopo kati ya Kishambala na Kiswahili ni kuwa katika Kiswahili, ung’ong’o huandamana tu na ughuna. Hivyo, mbali na fonimu sita za vipasuo sing’ong’o, lugha ya Kiswahili inazo fonimu tatu zaidi; tutaziita vipasuo-ng’ong’o ghuna, kama katika maneno yafuatayo. Kiswahili:

Orodha A (vipasuo ghuna)

24 a) kaba
b) daka
c) chuga

Orodha B (vipasuo-ng’ong’o)

25 a) kamba
b) kanda
c) chunga

Fonimu hizi zikiwekwa katika kielelezo zitaonekana kama ifuatavyo:

Kiswahili

26 /b,d,g/
/p, t, k/
/mb, nd, ng/

Kishambala

27 /b,d,g/
/p, t, k/
/mb, nd, ng/
/mp, nt, nk/

(Matatizo yanayobusu unukuaji na badhi ya kifbnetiki ya sauti hizi yamekwishajadiliwa katika sura iliyopita (angalia 2.4). Hapa, kwa sababu za kiothografia, imebidi tuziandike kama zilivyo katika maandishi ya kawaida).

Katika Kiswahili, basi, ung’ong’o ni sifa bainifu katika vipasuo-ghuna, ambapo katika Kishambala, ungo’ong’o ni sifa bainifu katika vipasuo vyote, ghuna na sighuna, na hivyo kufanya Kiswahili kuwa na fonimu tisa za vipasuo, na Kishambala kuwa na fonimu kumi na mbili za vipasuo.

Hii ni mifano michache tu inayodhihirisba dai la wanafonolojia kuwa kila lugba inao mfumo pekee wa fonolojia. Labda tofauti zinazojitokeza baina ya lugha moja na nymgine ni zile za fbnimu za lugha moja kukosekana kabisa katika lugha nyingine (yaani kutotumika katika kuunda maneno ya lugha hiyo). Tumekwishaona kuwa sauti zifuatazo ambazo zipo katika mfumo wa fonolojia ya Kiswabili, hazimo kabisa katika mfumo-sauti wa Kishambala /r, q, d/. Lugha ya Kibena haina sauti /Å¡/ ambayo inatokea katika maneno ya Kiswahili kama {mashaka, shika}, na katika Kisbambala {shuke, ushua) (nguo, utomvu).

Tofauti kati ya mifumo-sauti ya lugha zinadhihirika zaidi wakati mtu anapojifunza lugha ya pili baada ya kuwa amekwishajua lugha yake ya mwanzo. Wakati huo, mfumo-sauti wa lugha yake umekwishaimarika kwa kiasi kikubwa na akijifunza lugha ya pili, mara nyingi anatafsiri sauti za lugha hii mpya kwa misingi ya fonolojia ya lugba yake ya kwanza.

Tuchukue mfano mmoja tu, ambao unajulikana kwa wengi wetu. Kwa vile katika Kiswahili Sanifu kuna irabu tano tu, mjua Kiswahili akijifunza Kiingereza, anapata taabu sana kutofautisha kati ya irabu za Kiingereza ambazo ni nyingi zaidi ya zile za Kiswahili. Kwa mfano maneno yafuatayo ambayo katika Kiingereza yanatofautishwa, wazungumzaji wengi wa Kiswahili wanayatamka sawa: {bid : bead} ambayo katika Kiingereza hutamkwa [bid : bi:d]. Hapa tofauti ni urefu wa irabu [i] ambayo ni fupi katika neno la kwanza na ndefu katika neno la pili. Katika Kiswahili urefu wa irabu si sifa bainifu kwa hiyo wazungumzaji wa Kiswahili watayatamka maneno hayo kama [bid]. Vilevile neno {man} [maen] linatamkwa [man] na wazungumzaji wa Kiswahili kwa vile sauti [ae] haimo katika mfumo sauti wa Kiswahili. Tunaweza kuendeleza mifano ya namna hiyo bila kikomo.

Ni rahisi kupata mifano mingi kati ya watu wanaojifunza Kiswahili kama lugha yao ya pili au ya tatu, n.k. Mzungumzaji wa Kishambala, atayatamka maneno yafuatayo ya Kiswahili {raha, thamani, dhulwna} kama [laha, samani, zuluma]. Sauti zinazo- karibia [r, qd] katika Kishambala ni [l, s, z] na hivyo mzungumzaji huyu huzitumia hizo. Hata maneno ya Kiswahili yenye sauti hizo yakikopwa na kuingizwa katika Kishambala, yatatamkwa kwa sauti zilizoko katika mfumo-sauti asilia wa lugha hiyo. Hali hii ni kweli katika lugha nyingine za Kibantu. Mara nyingi, kama utasikia mtu anaongea lugha yako, na mara moja ukagundua kuwa ni mgeni wa lugha hiyo, sababu mojawapo inaweza kuwa kwamba anakosea kuweka tofauti za kifonimu (au kialofoni) zinazohitajiwa, au anaingiza ‘taratibu’ za fonolojia ya lugha yake ambazo hazimo katika lugha anayojifunza.

Mfano mwingine tunaweza kuuchukua kutoka kanuni za mfuatano wa konsonanti katika neno. Katika lugha nyingi za Kibantu, kuna kanuni inayotawala mfuatano wa ving’ong’o ha vipasuo. Sauti hizo zinapofuatana inapasa ziwe zinapatana katika mabali pa kutamkia. Hivyo mtu anayezungumza lugha yenye kanuni kama hiyo, (kwa mfano Kiyao) ataona arahisi wa kutamka neno la Kiswahili {nta}, lakini neno {mtu} yeye atalitamka *{ntu}, na {mkate} atalitamka *{nkate}. Hapa tunaona kanuni hii inavyojitokeza: sauti [n] na [t]; [n] na [k] zinapatana katika mahali pa kutamkia, lakini siyo [m] na [t]. Maneno kama {mbabe} na {mpaka} yataonekana ya kawaida kwa mzungumzaji wa Kiyao.

Bila shaka tofauti nyingi zingejitokeza ikiwa tungechunguza kikamilifu fbnolojia za lugha tofauti, lakini ni vigumu kufanya hivyo katika utangulizi kama huu. Na hata hivyo, si rahisi, kukamilisha kazi ya nanma hiyo bila kuchukua muda mrefu sana, kwa sababu hata katika lugha ambazo zimechunguzwa sana kama Kiingereza na lugha nyingine za Ulaya bado kuna mapengo mengi katika ufafanuzi. Pia yapo mambo mengi ambayo wataalamu wa fonolojia hawajakubaliana wayaelezeje, au wayaundie kanuni gani. Jinsi taaluma ya fonetiki inavyozidi kuimarika, na mifumo-sauti ya lugha nyingi kufafanuliwa, ndivyo na tofauti zaidi zitajionyesba. Lugha nyingi za Kiafrika hazijaanza kuchambuliwa kikamilifu, na pindi jitihada za kuzichambua zitakapoimarika, wanafonolojia watagundua minyumbuo mingi sana ambayo ni tofauti na ile inayojitokeza katika lugha za Kiulaya na za makundi mengine.