Masshele Swahili

Chuo- BBC
Podkasti ni kama kushughulika na tovuti yako, lakini podkasti unatumia sauti.
Kila nakala ni sawa na nakala ya tovuti, itahusu mada fulani.
Kama unapotaka kuandika katika tovuti, tafuta pahala/mada fulani; yaani kitu ambacho watu wanataka kujifunza au kujua ambacho hakipo kwengineko.
Kumbuka kuwa watu wanaosikiliza podkasti wanatafuta ujuzi/ufundi maalumu na watapenda kuwasikiliza wajuzi wa yale yanayozungumzwa.
Podkasti inaweza kuwa ya mtu mmoja tu,
yaani wewe
watu wawili
watu wengi
Mtindo huu wa podkasti umesambaa sasa kila pahala. Kuna waandishi wa habari au wasanii ambao wanavutia na wanazungumzwa sana watu wanapokutana. Podkasta maarufu wanavutia mamilioni ya wasikilizaji, na wenye matangazo ya biashara wanaanza kuvuna. Lakini podkasti zenyewe ni za zamani. Zilianza kabla ya Facebook, YouTube na Twitter; na mtindo wa sasa wa kutoa mtiririko wa maneno yaliyorikodiwa ulianza mwaka 2003. Google inasema neno podkast likaanza kutumika mwaka uliofuata.
Imechukua muda kwa mtindo kusambaa, lakini sasa umekuwa na washabiki wengi. Podkasti ziko kila pahala. Hata BBC imefuata mkondo sasa katika jukwaa jipya la BBC Sounds. Sababu ni kwamba kuna vitu vingi vizuri vya kuweka katika podkasti. Wazalishaji wanatoa vitu vya kuvutia na matayarisho hayahitaji zana za ghali. Na watu wanaohisi hawawakilishwi vya kutosha katika vyombo vya habari, wanapata nafasi ya kurekibisha kasoro hiyo. Ni njia ya demokrasi ya kweli kweli.
Watu wanaona hawahitaji ruhusa ya mtu yoyote kutengeneza makala yao wenyewe; wanaweza tu kujitokeza na sauti na maoni yao yatasikika. Na kila makala yakiwa mengi na mazuri , wasikilizaji wanaongezeka. Inakisiwa kuwa asilimia 23 ya Waingereza wamesikiliza podkasti katika mwezi uliopita.
Wasikilizaji wanaona kusikiliza podkasti ni kama kuwa na mtu ubavuni nawe, anayezungumza nawe kwa karibu, badala ya kusoma makala. Kinachovutia piya ni kwamba podkasti inaweza kusikilizwa popote, wakati umetulia, uko njiani au hata ndani ya gari.
Miaka 15 tangu podkasti kuanza, sasa imefufuka na kuzidi kupendwa.
Teknolojia na matangazo (yaani sauti na maoni yanayotolewa) yameumana pamoja. Mtiririko wa filamu kama vile zinazotolewa na kampuni ya Netflix umewafanya watu wanunue filamu kuangalia kwa nafasi yao. Na teknolojia mpya piya imezidisha hamu ya kusikiliza unachotaka upendapo na kwa wasaa wako.