Saa chache baada ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Vyuo Vikuu kukusanyika katika Ofisi za Bodi ya Mikopo wakidai kupewa mkopo kwa kudai kuwa wana na vigezo stahiki, Bodi ya mikopo imezungumzia suala hilo.
Meneja Mawasiliano wa bodi hiyo Omega Ngoli, ameeleza kuwa mpaka sasa wamekwisha toa mikopo kwa wanafunzi 29, 500 katika awamu ya kwanza na pesa hizo zimeshapelekwa vyuoni na awamu nyingine ya majina ya wanufaikaji wa mikopo hiyo itatolewa hivi karibuni.
Ameeleza pia kufikia Ijumaa November 10, 2017 Bodi hiyo ifungua dirisha la rufaa na hivyo wanafunzi ambao wanaona hawajatendewa haki watakata rufaa hiyo.