Uhakiki wa Fonimu na Miundo ya Silabi za Kiswahili 10

Uhakiki wa Fonimu na Miundo ya Silabi za Kiswahili

Benard Odoyo Okal

Ikisiri

Fonimu ni kipashio kidogo cha sauti ya lugha chenye uwezo wa kubainisha maana na hudhihirika

kama irabu au konsonanti. Kama ilivyo katika lugha nyinginezo ulimwenguni, Kiswahili vilevile

kina fonimu za kategoria mbili yaani irabu na konsonanti. Hata hivyo, idadi ya fonimu konsonanti

za Kiswahili inaelekea kuainishwa tofautitofauti kwa mujibu wa wanaisimu mbalimbali wa

Kiswahili. Mathalani, wanaisimu wengine wanadokeza idadi ya fonimu konsonanti kuwa 24, 25,

26, 29, 32 au 33. Kwa upande mwingine, miundo ya silabi za Kiswahili pia hudokezwa kuwa

tofauti kama vile 4, 5, 6, 7 na 8. Idadi tofauti ya fonimu konsonanti za Kiswahili pamoja na idadi

tofauti ya miundo ya silabi za Kiswahili huelekea kuwakanganya wasomaji wa lugha ya Kiswahili.

Hivyo basi, makala hii inalenga kuhakiki fonimu na miundo mbalimbali ya silabi za Kiswahili. Ili

kufanikisha uhakiki huu, makala hii imehusisha katika upeo wake vijimada kama vile: dhana ya

fonimu, uhakiki wa idadi ya fonimu za Kiswahili pamoja na mifano ya fonimu zenyewe. Makala

imeshughulikia pia dhana ya silabi na uhakiki wa miundo ya silabi za Kiswahili. Uhakiki wa

miundo ya silabi umeshughulikiwa ili kuangazia tofauti zinazodhihirika baina ya wanaisimu wa

Kiswahili kuhusu idadi kamili ya miundo ya silabi za Kiswahili pamoja na mifano inayotolewa.

Katika kujaribu kutanzua mgogoro uliopo, makala imerejelea kanuni zifaazo zinazoweza kutumiwa

na mwanaisimu katika utambuzi wa fonimu na zinazotumiwa pia katika uundaji wa silabi.

1.0 Utangulizi

Makala hii imechochewa na swali la Mwangi (2007:93) alipouliza iwapo alofoni

zipo au hazipo katika Kiswahili. Katika utangulizi wa makala yake, anaibua

masuala mengine ambayo yanaonekana kuwa tata na huenda hayajapata kutatuliwa

na wanaisimu wa Kiswahili. Suala mojawapo ni kuhusu idadi kamili ya fonimu

konsonanti za Kiswahili na vilevile aina zake. Wanaisimu mbalimbali wanaelekea

kutambua idadi ya fonimu konsonanti za Kiswahili kwa namna tofautitofauti,

kama vile: 32 (Ashton, 1951), 33 (Whiteley, 1956), 29 (Polome, 1967), 29

(Nchimbi, 1995), 24 (Mgullu, 1999), 25 (Habwe na Karanja, 2004), 25 (Kihore,

Massamba na Msanjila, 2009), 25 (Obuchi na Mukhwana, 2010), 26 (TATAKI,

2013) na 25 (Akidah, 2013).

Tofauti katika idadi ya fonimu konsonanti za Kiswahili zinawakanganya

wasomaji na ndizo zinazoelekea vilevile kuchangia midhihiriko tofautitofauti ya

idadi ya miundo ya silabi za Kiswahili pamoja na mifano kinzani inayotolewa.

Ukinzani huo hutokea kwa sababu, msingi wa uundaji silabi aghalabu hutokana na

fonimu ambayo inaweza kuwa ya herufi moja ya kujisimamia pekee au

mwambatanisho wa herufi zinazoweza kutamkwa kwa pamoja kama sauti moja

(Mgullu, 1999: 72). Iwapo idadi ya fonimu inatofautiana kama tunavyoona katika

makala mbalimbali za wanaisimu wa Kiswahili basi maelezo kuhusu miundo ya

silabi za Kiswahili pia yatazidi kutofautiana kama tunavyoona katika kazi za 

104 Kioo cha Lugha Juz. 13

baadhi ya wanaisimu kama vile: silabi 4 (Nchimbi, 1995), 7 (Mgullu, 1995), 6

(Habwe na Karanja, 2004), 5 (Mwita, 2009) na 8 (Obuchi na Mukhwana, 2010).

Katika kufafanua ipasavyo mada hii kuhusu fonimu na miundo ya silabi za

Kiswahili, makala hii imeongozwa na madhumuni mawili makuu: kwanza,

kuhakiki maandishi mbalimbali kuhusu idadi na mifano faafu ya fonimu za

Kiswahili. Pili, kuhakiki maandishi kuhusu idadi ya miundo ya silabi za Kiswahili

na mifano yake. Madhumuni haya yamelengwa katika makala hii kwa sababu

maandishi mbalimbali ya kiisimu katika Kiswahili yanaelekea kuonyesha tofauti

nyingi katika idadi ya fonimu konsonanti na idadi ya miundo ya silabi za

Kiswahili. Aidha, mifano inayotolewa kuhusu fonimu na silabi pia huelekea

kuwakanganya wasomaji kila mara. Kwa hivyo, wanaisimu mbalimbali

wanaelekea kuwa na mitazamo inayotofautiana kuhusu dhana mbalimbali katika

fonetiki na fonolojia ya Kiswahili.

2.0 Dhana ya Fonimu

Istilahi fonimu imefafanuliwa na wanafonoloja mbalimbali. Trubetzkoy (1969:19)

anaieleza fonimu kama ishara ya kifonolojia yenye uamilifu. Vilevile, fonimu

huweza kurejelewa kama kundi la sauti katika lugha lenye sauti muhimu na sauti

zinazohusiana nayo na zinazoweza kutumiwa pahali pake katika miktadha mingine

maalum (Jones, 1975 akirejelewa na Mgullu, 1999: 51). Fonimu ni kipashio msingi

cha kifonolojia kinachotumiwa kubainisha maana za maneno katika lugha (Lyons,

1981: 84; Yule, 1996: 54; Batibo, 2000: 161). Kwa mfano, fonimu /a, e, i, o, u/

zina uwezo wa kubadilisha maana katika maneno. Mathalani, maneno pata na

peta yanatofautiana kimaana kwa sababu ya tofauti za fonimu /a/ katika pata na /e/

katika peta. Tunapotumia njia ya mlinganuo finyu ambapo mtindo wa nitoe

nikutoe hutumika, basi fonimu /p, t, a/ hutoana huku /a/ moja katika pata na /e/

katika peta husalia kama inavyojidhihirisha katika mifano ifuatayo:

Pata = pa t a = /a/

Peta = pe t a = /e/

Kwa kuwa fonimu /a/ na /e/ hazitoani, maana za maneno hayo huelekea

kutofautiana vilevile. Pata humaanisha ‘kuwa na jambo, hali au kitu’ (TUKI,

2004: 329) na peta humaanisha ‘rusharusha nafaka katika kitunga au ungo ili

kuondoa makapi na takataka’ (TUKI, 2004: 333).

Fonimu huwa akilini mwa mtu na aghalabu huhusiana na vivuli vyake au

alofoni zake kama vile fonimu /p/ ina kivuli chake /p

h

/ (Fromkin, Rodman na

Hyams, 2007: 261). Kwa jumla, fonimu humaanisha sauti ya lugha au kipashio

kidogo dhahania cha lugha chenye uwezo wa kubadilisha, kuvuruga au kuleta

maana kusudiwa ya neno (Batibo, 2000:161; Fromkin na wenz., 2007: 266).

Fonimu inapotumia alama ya mishazari miwili (/ /) kuonyesha???? mipaka yake, 

Uhakiki wa Fonimu na Miundo ya Silabi za Kiswahili 105

alama ya mabano mraba [ ] hutumiwa kuonyesha foni ya lugha au sauti zozote za

lugha ya binadamu (Mgullu, 1999: viii; Fromkin na wenz., 2007: 261).

Batibo (2000: 161-2) anaeleza dhima anuwai za fonimu kama vile: kwanza,

husaidia katika uundaji wa maneno ya lugha. Kwa mfano, fonimu irabu /a/ huweza

kutumiwa pamoja na fonimu konsonanti /p, t/ na hatimaye kuunda silabi {pa} na

{ta}. Silabi hizi za {pa} na {ta} huunda neno pata. Pili, fonimu huonyesha

ujumisia katika maana za maneno hasa katika matumizi ya onomatopeya na

vihisishi. Tatu, fonimu husaidia katika kubainisha maana za maneno ya lugha

kama tunavyoona katika kamusi za lugha husika.

2.1 Hatua za Kufafanua Fonimu Kifonolojia

Fonimu hufafanuliwa kifonolojia kupitia hatua mbalimbali (Batibo, 2000: 182-8)

kama vile: kwanza, kuwa na hifadhi maalum ya sauti zilizokusanywa na

kuziandika kwa kutumia hati ya unukuzi makinifu ya kimataifa kama vile /ʧ (ch), ɲ

(ny), ɳ (ng’), θ (th), ʃ (sh), ð (dh), ɤ (gh)/. Pili ni kutambua familia za fonimu kwa

kuziweka pamoja fonimu irabu na konsonanti na aina zake. Tatu ni kuainisha

fonimu kwa mujibu wa sifa bainifu za kifonetiki na kuwasilisha aina zake katika

majedwali au mpangilio maalum. Vilevile, kuna kufafanua fonimu husika kwa

mujibu wa sifa bainifu za kiarudhi kama vile mkazo, silabi na toni.

2.2 Miainisho mbalimbali ya Fonimu za Kiswahili

Mgullu (1999: 69) anadokeza kuwa lipo tatizo la ufumbuzi wa idadi kamili ya

fonimu konsonanti za Kiswahili hasa lile tatizo la mwambatanisho wa sauti.

Anaongeza pia kuwa kuna wanaodai kwamba sauti kama vile [n] na [d] zikifuatana

huunda fonimu moja /nd/. Chimbuko la dai kama hili ni ile hali inayodhihirika

miongoni mwa fonimu kama vile /t/ na /h/ zinazotamkwa kama sauti moja na

hatimaye kuchukuliwa kama fonimu mwambatano /th/. Aidha, inadhihirika wazi

katika fonolojia ya Kiswahili kuwa kuna kutofautiana baina ya wanaisimu kuhusu

idadi sahihi na kamili ya vipandesauti vya Kiswahili (Mwangi, 2007:93). Hivyo

basi, wanaisimu mbalimbali wa Kiswahili wanaelekea kutoa idadi na pia mifano

tofautitofauti kuhusu fonimu konsonanti za Kiswahili kama vile:

Ashton (1951:3-4): /p, b, m, w, mb, f, v, mv, th, dh, j, t, d, s, z, n, r, l, nd, nz, ch, sh, nj, ny, y, k, g,

kh, gh, ng’, ng, h/ = 32

Whiteley (1956:9): / , , , , , , , , , t, t


, d, n, r, l, s, , nt, nd, ch, ch


, j, sh, n , ny, y, k,

k


, g, ng’, nk, ng, h/ =33

Polome (1967:38-9): /p, ph

, , t, th, d, c, ch, Ɉ, k, kh

, g, , , θ, ð, s, , š, ɤ, h, , n, ɲ, ɳ, l, r, , /

=29

Nchimbi (1995:35): / , t, ʗ (ʧ), k, , d, Ɉ, g, , ɲ, ɳ, n, , θ, s, ʃ, h, , ð, , r, l, , , ɤ, , nd, ng,

nj/ =29

106 Kioo cha Lugha Juz. 13

Mgullu (1999:67): / , ʧ (ch), d, ð (dh), , g, ɤ (gh), h, k, l, , n, ɲ (ny), ɳ (ng’), , r, s, ʃ (sh), t, θ

(th), Ɉ ( ), , , x (kh)/ =24

Habwe & Karanja (2004:49): / , , , , ƒ, , θ, ð, t, d, l, r, n, s, , Ɉ, ɲ, , ʃ, ʧ, k, g, ɳ, ɤ, h/ =25

Kihore na wenz. (2009:16): / , ch, d, ð, ƒ, g, ɤ, h, , k, l, , n, ɲ, ɳ, , r, s, sh, t, θ, v, w, y, z/ = 25

Obuchi na Mukhwana (2010:84): / , , , θ, t, l, n, , ɲ, ʃ, k, ɳ, h, , , , ð, d, r, s, , y, ʧ, g, ɤ/

=25

TATAKI (2013: xvi): / , ʧ, d, ð, f, g, ɤ, h, Ɉ, k, x, l, , n, ɳ, ɲ, , r, s, ʃ, t, θ, , , , / = 26

Akidah (2013: 3-4): /p, b, m, f, v, θ, ð, t, d, n, ɲ, s, z, l, r, j, ʃ, k, g, tʃ, ŋ, ɣ, h, w, y/ = 25

Wanaisimu hawa waliorejelewa wanakubaliana kuwapo kwa fonimu irabu 5

msingi za Kiswahili yaani /a, e, i, o, u/. Hata hivyo, wanatofautiana katika idadi ya

fonimu konsonanti. Ashton (1951) na Whiteley (1956:9), wanaainisha jumla ya

fonimu konsonanti za Kiswahili 32 na 33 mtawalia. Ingawa Polome (1967:38-9)

anaainisha fonimu konsonanti 29 za Kiswahili, idadi inayolandana na ya Nchimbi

(1995:35), kazi yake haitambui sauti [mb, ng, nj, nd] kama fonimu za Kiswahili

ambazo zinatambuliwa na Nchimbi.

Kwa mujibu wa Polome (1967), sauti [mb, ng, nj, nd] si fonimu licha ya

kwamba zinaundwa na fonimu konsonanti /m, n/. Hata hivyo, anaendelea

kudokeza kuwa fonimu hizi za /m, n/ aghalabu huambatana na konsonanti /b, g, j,

d/ katika uundaji wa silabi. Badala yake Polome anaongeza hoja ya kuwapo kwa

fonimu nyingine hasa /ph

, c, kh

, š/ katika msururu wa idadi ya fonimu za Kiswahili.

Kwa kweli [p

h

, kh

, š] si fonimu bali ni alofoni, na sauti [c] haipo katika msururu wa

fonimu za Kiswahili sanifu. Ile fonimu inayodhihirika katika Kiswahili ni /ch/

inayoonyeshwa kifonetiki kama /ʧ/. Vilevile, wanazuoni wengine wanazungumzia

idadi tofauti ya fonimu konsonanti kama vile fonimu 24 (Mgullu, 1999), fonimu 25

(Habwe na Karanja, 2004; Kihore na wenz., 2009; Obuchi na Mukhwana, 2010;

Akidah, 2013), na fonimu 26 (TATAKI, 2013).

Makala hii inaegemea mtazamo wa skuli ya Nchimbi (1995:35) na wafuasi

wake kwamba kuna fonimu konsonanti 29 za Kiswahili zikiwemo sauti ng’ong’o

[mb, ng, nj, nd]. Mtazamo huu unaungwa mkono na Simala (1995:48). Aidha, sauti

hizi ziliwahi kutambuliwa na Ashton (1951) na Whiteley (1956). Ingawa Obuchi

na Mukhwana (2010:84) hawaorodheshi [mb, ng, nj, nd] kama fonimu konsonanti

za Kiswahili, kwa upande mwingine wanatambua kuwapo kwa dai kwamba sauti

hizi hutumika licha ya kwamba hazijawakilishwa kwa ishara maalum za kifonetiki.

Hata hivyo, zile alama za kifonetiki wanazodokeza kuwa hazijabuniwa zipo kama

vile [ ƅ ( ), Ŋ (nd), N (ng), Ɲ(n )] (Nchimbi,1995:35). Vilevile, fonimu hizi 

Uhakiki wa Fonimu na Miundo ya Silabi za Kiswahili 107

tayari zimetambulika na alama za kuziwakilisha kupendekezwa kama vile: /nd/ =

/

n

d/, /mb/ = /

m

b/, /ng/ = /

n

g/ na /nj/ = /

n

j/ (Mwita, 2007:65).

Utambuzi wa fonimu za Kiswahili ungali unaendelea na fonimu zenyewe

hufaa kurekodiwa mara kwa mara zinapotambuliwa (Choge, 2009:64). Iwapo

hakuna alama katika orodha ya alama za unukuzi makinifu ya kimataifa basi alama

mpya au alama saidizi huweza kubuniwa na wanaisimu wa lugha husika (Lyons,

1981:69). Alama saidizi hutumika hata katika lugha nyinginezo za Afrika,

Amerika Kusini, Asia Kusini na Pasifika kuwakilisha fungu fonimu zilizokubalika

kama vile fonimu /᷇mb, ᷇nd/ zinazotamkwa kama sauti moja (Anderson, 1976

akirejelewa na Mwita, 2007:65).

Isitoshe, utambuzi wa fonimu za lugha hauna kikomo. Hii ndiyo sababu

Choge (2009:64) anasema kuwa utambuzi na uwekaji rekodi za fonimu za

Kiswahili ungali unaendelea. Utambuzi huo wa fonimu za Kiswahili huonekana

katika sauti kama vile /Ɲ, Ŋ, <b, N/ (Nchimbi, 1992 akirejelewa na Choge,

2009:64). Katika kuonyesha kuwa utambuzi wa fonimu ungali unaendelea, Choge

(2009:64) anatambua fonimu irabu nyingine za Kiswahili kama vile irabu ndefu /i:,

ɛ:, a:, u: & כ /:na irabuunganifu /au & כa/ na kuzidhihirisha katika data maalumu.

2.3 Kanuni za Utambuzi wa Fonimu

Kuna kanuni maalum zilizoangaziwa na Trubetzkoy (1969:56-58) za kufafanua na

kutambua sauti mahususi na sauti mwambatano zinazopaswa kurejelewa kama

fonimu moja. Kanuni hizo ni:

i. ‘Mwambatanisho tu wa sauti ambazo vijenzi vyake katika lugha

havijasambaa hadi silabi nyingine ya pili zichukuliwe kama fonimu moja

inayotambulika’ (Tafsiri yetu).

Kwa mujibu wa kanuni hii, sauti mwambatano (sauti yenye herufi mbili au zaidi)

hufaa kudhukuriwa kama fonimu iwapo sauti zenyewe hazijasambaa katika silabi

nyingine ya neno. Kama vile neno ngoma lina fonimu nne /᷇ng, o, m, a/ zinazounda

silabi mbili za /$᷇ngo$ma$/. Kinachodhihirika hapa ni kuwa sauti mwambatano /᷇ng/

huunda silabi ya kwanza $᷇ngo$ na hakuna sehemu yake nyingine inayosambaa

hadi silabi ya pili $ma$.

ii. ‘Sauti mwambatano huweza kufasiriwa kama fonimu moja iwapo

imetamkwa katika sehemu moja ya utamkaji au kutokana na urahisishaji wa

utamkaji changamano’ (Tafsiri yetu).

Kanuni hii ndiyo inachangia ubunaji wa alama moja ya kuwakilisha fonimu kama

vile /ʧ (ch), ɲ (ny), ɳ (ng’), θ (th), ʃ (sh), ð (dh), ɤ (gh). Fonimu hizi mwambatano

hudhihirika hata katika lugha nyinginezo za kigeni kama vile Kiingereza (Lyons,

1981; 79). Tukumbuke kuwa licha ya kwamba fonimu hizi zinalandana katika 

108 Kioo cha Lugha Juz. 13

takriban lugha zote ulimwenguni ikiwemo Kiswahili na lugha nyinginezo, hakuna

kosa iwapo lugha nyingine mahususi zitadhihirisha vilevile fonimu za ziada zenye

herufi mwambatano tofauti hata hivyo zinazotamkwa kama sauti moja.

Labda kile kinachopaswa kuelezwa kwanza ni kwa namna gani sauti /ch, ny,

ng’, th, dh, gh/ zichukuliwe kama fonimu moja licha ya kuwa na herufi mbili na

sauti [nd, nj, ng, mb] ambazo pia huundwa na herufi mbili zisidhukuriwe kama

fonimu moja. Mathalani, katika Kiswahili, fonimu [h] huweza kuungana na fonimu

nyingine ili kuunda fungu fonimu kama vile /θ (th), ʃ (sh), ð (dh)/ (Ontieri, 2015:

2525). Muungano huu hutakona na hali ya utamkaji na pia mahali pa kutamkia

sauti hizi iwapo zinapatikana katika mazingira yaleyale. Mathalani, sauti ng’ong’o

hutamkika kwa kung’ong’oeshwa katika sehemu ya utamkaji inayojulikana kama

chemba ya pua (Coxhead, 2006:3).

Utamkaji wa sauti kama hizi umeangaziwa na Lyons (1981:74) anapodokeza

kuwa sauti [b, p, m], [d, t, n], na [g, k, ɳ (ng’)] zinahusiana kifonetiki au

kimatamshi kwa namna inayolingana. Sauti [b, p, m] hutamkika mdomoni huku [b,

m] zikiwa ghuna na [p] sighuna. Hivyo basi, ni rahisi kwa sauti ghuna [m, b]

kutamkika kama sauti moja na hatimaye kuunda fonimu moja /mb/. Kwa upande

mwingine, sauti [d, t, n] hutamkika kwenye ufizi hata hivyo [n, d] ni sauti ghuna

na [t] sighuna. Hivyo basi, sauti [n, d] huweza kufuatana na kutamkika kama sauti

moja na hatimaye kuunda fonimu moja /nd/ kama katika neno nda-ma. Aidha,

sauti [g, k, ɳ (ng’)] hutamkika kwenye kaakaa laini hata hivyo sauti /g, ɳ (ng’)/ ni

ghuna ilhali sauti [k] sighuna. Sauti hizi aghalabu hukubali mfuatano na sauti [n]

inayotamkika kwenye ufizi na hatimaye kuunda sauti moja kama vile [ng] kama

tunavyoona katika neno ngo-ma. Fafanuzi hizi huweza kuonyeshwa kwa njia

ifuatayo:

Sauti za midomo: [b, m] ghuna [p] sighuna

Sauti za ufizi: [d, n] ghuna [t] sighuna

Sauti za kaakaa laini: [g, ɳ (ng’)] ghuna [k] sighuna

Kutokana na fafanuzi hizi, imebainika kuwa sifa ya sighuna ndiyo hufanya sauti

[p] ikitanguliwa na sauti [m] kutounda fonimu moja bali hudhihirisha fonimu mbili

tofauti kama vile /m/ na /p/ zinazodhihirika katika maneno kama vile: m-pa-ka.

Katika mfano huu, /m/ husalia kama fonimu ya kipekee iliyo na sauti yake maalum

huku fonimu /p/ ikiambatana na /a/ ili kuunda silabi {pa}. Aidha, sifa ya sighuna

ya sauti [t] ikitanguliwa na sauti [n] ndiyo huchangia kuundwa kwa fonimu mbili

kama vile /n/ na /t/ kama katika neno n-ta.

Kihore na wenz. (2009: 26-7) wanaeleza kuwa kule kuathiriana

kunakotokea baina ya sauti nazali [m, n] zenye maumbo tofauti na sauti nyinginezo

zisizo za nazali kama vile [b, d, g] aghalabu huchangia uundaji wa maneno kama

vile mbawa, ndugu na ngoma. Tunachoweza kujifunza kutokana na maelezo ya

Kihore na wenzie ni kwamba nazali hizi kimsingi zinaathiriwa na konsonanti 

Uhakiki wa Fonimu na Miundo ya Silabi za Kiswahili 109

fuatilizi kama vile [m] huathiriwa na [b], na [n] huathiriwa na [d, g]. Kihore na

wenz. (2009: 32) wanaendelea kueleza kuwa kwa vile sauti [b] hutamkika kwa

kufunga mdomo, nazali [m] vilevile huathirika kwa kutamkwa kwa kufunga

mdomo. Hivyo basi, umbo tofauti linaloundwa kwa maoni yetu bila shaka litakuwa

[mb]. Kwa upande mwingine, sauti [d] inayotamkika kwenye ufizi huathiriana na

[n] ya ufizi na hatimaye kuunda umbo jipya tunaloita [nd]. Konsonanti [g] ya

kaakaa laini hulazimisha sauti [n] ya ufizi kutamkika kwenye kaakaa laini na

hatimaye kuunda sauti [ng]. Mifanyiko hii yote hurejelewa kama usilimishwaji wa

konsonanti.

Isitoshe, Kihore na wenz. (2009:32) wanatuhadharisha kuwa ingawa sauti

hizi za [m, n] zinaathiriana na sauti [b, d, g], isichukuliwe kuwa zinawakilisha sauti

moja bali zinawakilisha sauti mbili tofauti. Hata hivyo, wanajipinga wenyewe

wanaposema kwingine kuwa sauti hizi mwambatano yaani [mb, nd, ng] hutamkwa

kwa pamoja kama sauti moja kama tunavyoona katika dondoo lifuatalo:

‘Ingawa mfuatano huu wa herufi hufanana na mfuatano

tuliouelezea hapo juu lakini kila moja ya herufi zinazoandamana

hapa ni sauti inayojitegemea kwa dhati yake ingawa hutamkwa

kwa pamoja’ (Kihore na wenz., 2009:32).

Kimsingi, sauti hizi ng’ong’o za [mb, nd] huundwa kutokana na mchakato wa

usilimishwaji unaoitwa kama unazalishaji. Unazalishaji hurejelewa kama utamkaji

ambapo kitamkwa kisichokuwa nazali hupata sifa za unazali (TUKI, 1990:41).

Utafiti unadhihirsiha kuwa sauti zinazoundwa kutokana na usilimishwaji hufaa

kurejelewa kama sauti moja japo huundwa na sauti mbalimbali. Ithibati zinatolewa

na Mwita (2007:64) kuwa: kwanza, sauti hizi mwambatano zinafanana na

vikwamizwa katika muundo wa ndani. Pili, sauti hizi ni vitamkwa pamwe

vinavyotamkwa katika pahali pamoja. Tatu, sauti hizi hufanya kazi katika uundaji

wa silabi moja husika yaani hushiriki katika uundaji wa silabi moja maalum.

Aidha, Higgins (2012: 48) anadhihirisha unazalishaji wa sauti ng’ong’o

kuwa iwapo nazali [m] imetanguliza [b] basi unazalishaji wa [b] hutokea na

kuunda fungu fonimu /mb/. Kwa upande mwingine, iwapo nazali [n] imetanguliza

[d] basi unazalishaji wa [d] hutokea na hatimaye kuunda fungu fonimu /nd/. Hata

hivyo, tunatahadharishwa kuwa sauti zenye herufi mbili zinaweza kudhukuriwa

kuwa sauti tofauti iwapo matamshi yake yanasambaa katika silabi nyingine na hali

hiyo huweza kutambuliwa (Mwita, 2007:65).

iii.‘Sauti mwambatano huweza kudhukuriwa kama fonimu moja iwapo

haichukui muda zaidi kutambulika kuliko fonimu nyingine zinazojitokeza

katika lugha hiyo husika’ (Tafsiri yetu).

110 Kioo cha Lugha Juz. 13

Sauti mwambatano ni fonimu iwapo muda unaochukuliwa kuitambua unalingana

na sauti nyingine katika lugha husika. Kanuni hii inaonyesha kuwa fonimu za

lugha zinaelekea kuchukua muda unaolingana hata hivyo ule wa kutamkwa kwa

fonimu huweza kuathirika kutokana na mkazo. Kanuni hii hudhihirika hata katika

kila silabi ambayo hupimwa kwa kutumia sehemu moja ya mia ya sekunde (1/100)

inapotamkwa na huchukua muda mrefu kutamkwa inapowekewa mkazo

(Mwansoko, 1995:16). Mathalani, mfuatano wa fonimu katika Kiingereza kama

vile /mp, mb/ huchukua muda sawa wa kutamkwa ukilinganisha na kutamkwa kwa

fonimu /p, b, m/ (Ladefoged na Maddieson, 1996 katika Mwita, 2007:62). Hata

hivyo, silabi yenye shadda hutumia nguvu zaidi kutamkwa ikilinganishwa na zile

zisizo na mkazo (Mgullu, 1999:36).

2.4 Je, Mtazamo wa Nchimbi kuhusu Fonimu Konsonanti za Kiswahili

 Unafaa?

Iwapo, tutafuata kikamilifu mtazamo wa skuli ya Nchimbi (1995) na wafuasi wake

na pia kanuni kuhusu fonimu zilizodokezwa na Trubetzkoy (1969), basi kwa jumla

kunafaa kuwa na fonimu irabu tano msingi (5) kama vile /i, e, a, o, u/. Aidha,

kunafaa kuwa na fonimu konsonanti 29 /p, t, ʧ, k, , d, Ɉ, g, , ɲ, ɳ, n, , θ, s, ʃ, h,

v, ð, z, r, l, j, w, ɤ/ zikiwemo fonimu nyingine za ziada / ᷇ , ᷇nd, ᷇ng, ᷇n / za

Kiswahili.

Japo fonimu hizi za /᷇mb, ᷇nd, ᷇ng, ᷇nj/ zinazodhihirika katika Kiswahili

hazitambuliwi na baadhi ya wanaisimu wa Kiswahili, fonimu zenyewe zinaelekea

kutambulika moja kwa moja katika lugha nyinginezo za Kiafrika zinazotumia

mfumo wa matamshi unaolingana na wa Kiswahili. Kama vile, Kiluo kina fonimu

(/ , ch, d, dh, , g, h, , k, l, , n, ng’, ny, , r, s, t, th, , y, mb, nd, ndh, ng, nj/)

(Okombo, 1982; Tucker, 1994: 31; Owino, 2003; de Lacy, 2009: 5; Cable,

2009:4). Kuna pia lugha za Kibantu ambazo zina sauti ng’ong’o zilizotambuliwa

na kurekodiwa kama fungu fonimu zenye uwezo wa kutamkwa kama sauti moja.

Mathalani, Kikongo kina /mb, nd, ng, mv, nz/, Kikuria kina / , nd, ɳk, ɳg, nt, ns/

na Kiluganda kina / , nd, ɳ , ɳg, mp, nt/ (Mwita, 2007:58-60). Aidha, lugha ya

Ki-Chagga hudhihirisha fonimu /mb/ inayotamkwa kama sauti moja (Mwita,

2007:62).

Lugha nyingine ya Kibantu inayoitwa Ikoma inayozungumzwa katika eneo

la Mara kule Tanzania vilevile ina fonimu /mb, nd/ (Higgins, 2012:48), Kimeru na

Kiembu zina fungu fonimu /mb, nd, ng, nj/ (Starzmann, 2014: 5) na Kikuyu pia

kina /mb, nd, ng/ (Mwaniki, 2013:10). Katika Kikuyu, /mb, nd, nj, ng/ hudhihirika

katika maneno kama vile: ‘mbembe’, ‘nduma’, ‘njira’ na ‘ngoro’ (Cable, 2010:4-

5). Fonimu hizi zina alama maalum zinazotumiwa kuziwakilisha kifonetiki katika

Kikuyu kama vile: /mb/ = /

m

b/, /nd/ = /

n

d/, /nj/ = /

n

ɟ/, na /ng/ = /

n

g/ (Cable, 2010:4-

5).

Uhakiki wa Fonimu na Miundo ya Silabi za Kiswahili 111

Isitoshe, lahaja ya Kiswahili inayoitwa Kikae vilevile ina fonimu ng’ong’o

/mb, nd, nj, ng/ (Furumoto, 2015:20). Hivyo basi, utamkaji na utambuzi wa sauti

hizi nne za [mb, nd, ng, nj] hufaa kutafitiwa zaidi na wanaisimu ili tuwe na taarifa

inayojitosheleza kuhusu idadi kamili ya fonimu na aina za fonimu katika Kiswahili

bila kuwapo na idadi tofautitofauti na mifano mbalimbali inayochanganya wasomi

wa Kiswahili.

3.0 Dhana ya Silabi

Silabi imefafanuliwa na wanaisimu kwa namna mbalimbali. Mathalani, Fudge

(1990) akirejelewa na Mgullu (1999:72) anaifafanua silabi kama kipashio cha

kifonolojia ambacho ukubwa wake upo kati ya fonimu na neno, na ndefu zaidi

kuliko fonimu lakini ndogo ikilinganishwa na neno kamili. Naye, Batibo

(2000:175) anaifasili silabi kama kipashio katika neno chenye uwezo wa

kuathiriwa na mkazo au toni. Aghalabu, silabi huwa na konsonanti yenye

usonoranti kama vile nazali au likwidi na vokali yenye usonoranti ambayo wakati

mwingine hurejelewa kama kiini.

Juu ya hayo, kwa mujibu wa TATAKI (2013:512), silabi hurejelewa kama

sehemu ya neno inayoundwa na konsonanti na irabu au irabu pekee na hutamkwa

pamoja kama fungu moja la sauti linalojisimamia. Vilevile, silabi hufafanuliwa

kama sehemu ya neno inayoweza kutamkwa mara moja kama fungu moja la sauti

(Kihore na wenzake 2009:18). Huweza kurejelewa pia kama kipashio cha

matamshi ambacho sauti za lugha hutamkwa mara moja kama fungu maalum

linalojitegemea (Obuchi na Mukhwana, 2010: 91). Sauti hizi za lugha

zinazotamkwa mara moja aghalabu huunda mapigo ya sauti kwenye neno husika

na kuweza kusikika (Longhorn, 2011: 464).

Kwa jumla, silabi ni tamko au kipashio kidogo au mapigo ya sauti

yanayotamkwa mara moja katika neno kama fungu moja. Aghalabu, silabi ni

kubwa kuliko fonimu hata hivyo ni ndogo ikilinganishwa na neno. Aidha, silabi

huweza kuathirika kutokana na mkazo na toni na huwa na konsonanti na irabu

zenye usonoranti mkubwa. Wanaisimu wa kifonolojia wanaafiki kuwa aghalabu

silabi moja huweza kuwa na sehemu tatu kama vile mwanzo, kiini/kitovu na

koda/mwisho/kifungio (Yule, 1996:57; Batibo, 2000:176; Fromkin na wenzake

2007: 287).

Sehemu ya mwanzo aghalabu huwa na konsonanti. Hata hivyo, wakati

mwingine konsonanti inakuwa haipo ikiwa neno limeanza na irabu inayosimama

peke yake kama silabi (Yule, 1996:58). Kiini au kitovu aghalabu huwa irabu na

husikika zaidi kuliko konsonanti inayoambatana nayo. Aidha,

koda/mwisho/kifungio huwa konsonanti kama tunavyoona katika Kiingereza

kilicho na silabi funge. Yaani silabi inayoishia na konsonanti. Kimsingi, sehemu za

mwanzo na mwisho husaidia kuweka mipaka kati ya silabi zinazofuatana.

112 Kioo cha Lugha Juz. 13

3.1 Aina za Silabi

Kuna aina kuu mbili za silabi yaani silabi wazi au huru na silabi funge (Yule,

1996: 57; Batibo, 2000: 176; Fromkin na wenz., 2007: 286-7; Kihore na wenz.,

2009:18; Obuchi na Mukhwana, 2010:92). Silabi wazi huishia na irabu kama

katika neno kata kuna silabi mbili yaani /$ka$ta$/ zinazoishia na irabu. Aidha,

silabi wazi hudhihirika zaidi katika lugha ya Kiswahili na lugha nyinginezo kadha

za Kiafrika. Nayo, silabi funge huishia na konsonanti na aina hii aghalabu

hudhihirika mno katika lugha kama vile Kiingereza. Mathalani, neno good lina

silabi mbili, yaani /gʊ:d/ huku silabi ya mwisho ikiishia na konsonanti pekee.

3.2 Uhakiki wa Miundo ya Silabi za Kiswahili

Kimsingi, silabi zozote za lugha huelekea kuchukua mfumo wa konsonanti (K) na

irabu (I) (Yule, 1996:58; Aswani, 1995 akirejelewa katika Oduma na Odhiambo,

2008: 170; Fromkin na wenzake 2007:287). Vilevile, silabi za Kiswahili huchukua

mfumo kama huo. Hata hivyo, idadi ya miundo ya silabi za Kiswahili hudhihirisha

mkinzano mkubwa baina ya wanaisimu mbalimbali wa Kiswahili kama

tunavyoona katika Nchimbi (1995), Mgullu (1999), Habwe na Karanja (2004),

Mwita (2009), na Obuchi na Mukhwana (2010) miongoni mwa wengine. Katika

kuonyesha mifano ya miundo ya silabi katika neno, hati mlazo iliyo na wino mzito

imetumiwa:

Nchimbi (1995:36) anafafanua miundo minne ifuatayo ya silabi za Kiswahili:

1. Silabi ya irabu pekee (I): ua = ua

2. Silabi ya konsonanti pekee (K): nta = nta

3. Silabi ya konsonanti na irabu (KI): maji = maɈi, washa = waʃa

4. Silabi ya konsonanti, konsonanti na irabu (KKI): mpya = mpja, mgonjwa =

mgo᷇njwa

Uhakiki wa Fonimu na Miundo ya Silabi za Kiswahili 113

Mgullu (1999:73) anafafanua miundo saba ya silabi za Kiswahili kama ifuatayo:

1. Silabi ya irabu pekee (I): adui = a-du-i

2. Silabi ya konsonanti pekee (K): mtu = m-tu

3. Silabi ya konsonanti na irabu (KI): kitabu = ki-ta-bu

4. Silabi ya konsonanti, konsonanti na irabu (KKI): ndama = nda-ma.

5. Silabi ya konsonanti, nusu irabu na irabu (K½II): afya = a-fya

6. Silabi ya konsonanti, konsonanti, nusu irabu na irabu (KK½II): mbweha =

mbwe-ha

7. Silabi funge inayoishia na konsonanti na inayohusiana vilevile na maneno

yenye mkopo: labda = lab-da

Habwe na Karanja (2004:67-8) wanaainisha miundo sita ifuatayo ya silabi za

Kiswahili:

1. Silabi ya vokali pekee (V): iga = i-ga

2. Silabi ya konsonanti vokali (KV): panga = pa-nga

3. Silabi ya konsonanti pekee (K): mtu = m-tu

4. Silabi ya konsonanti, nusu vokali na vokali (K½VV): pigwa = pi-gwa

5. Silabi ya konsonanti, konsonanti, nusu vokali, vokali (KK½VV): bingwa =

bi-ngwa

6. Silabi ya konsonanti nazali, konsonanti na vokali (KKV): pinga = pi-nga

Mwita (2009:49) anaainisha miundo mitano ya silabi za Kiswahili kama vile:

1. Silabi ya konsonanti na irabu (KI): kiti = ki.ti

2. Silabi ya irabu (I) moja pekee: oa =o.a

3. Silabi ya konsonanti pekee (K) hasa konsonanti nazali: mtu, nne = m.tu,

n.ne

4. Silabi ya konsonanti, konsonanti na irabu (KKI): mwezi = mwe.zi

5. Silabi ya konsonanti, konsonanti, konsonanti na irabu (KKKI): chungwa =

cu.ɳgwa

Obuchi na Mukhwana (2010:93-5) wanaeleza kuwa kuna miundo minane ya silabi

za Kiswahili:

1. Muundo wa konsonanti na irabu (KI): wivu = wi-vu

2. Muundo wa konsonanti, konsonanti na Irabu (KKI): njama = nja-ma

3. Muundo wa konsonanti, nusu irabu na irabu (K½II): bweka = bwe-ka

4. Muundo wa konsonanti, konsonanti, nusu irabu, irabu (KK½II): mbweha =

mbwe-ha

5. Muundo wa irabu pekee (I): oa = o-a

6. Muundo wa konsonanti pekee (K): mtu = m-tu

7. Muundo wa konsonanti, irabu, irabu (KII): kaakaa = kaa-kaa

114 Kioo cha Lugha Juz. 13

8. Muundo wa konsonanti, konsonanti, konsonanti, irabu (KKKI): skrubu =

skru-bu

Kutokana na wanaisimu hao, imebainika kuwa wanaisimu wote wanakubaliana

kuwapo kwa miundo minne msingi ya silabi kama vile I, K, KI, KKI licha ya kutoa

mifano tofauti inayokinzana na kukanganya wanaisimu. Hata hivyo, kuna baadhi

yao wanaoongeza miundo mingine zaidi kama vile (K½II, KK½II, na silabi funge)

(Mgullu, 1999), (K½VV, KK½VV) (Habwe na Karanja, 2004), (KKKI) (Mwita,

2009) na pia (K½II, KK½II, KII, KKKI) (Obuchi na Mukhwana, 2010).

Wanaisimu hawa wanaelekea kutofautiana hasa katika orodha ya idadi ya

silabi za Kiswahili na mifano yake. Labda hali hii imetokea kwa sababu ya tofauti

katika idadi na miundo ya fonimu na maneno mengine ya Kiswahili sanifu yenye

sauti ambazo kiotografia huandikwa kwa kuwakilishwa na herufi zaidi ya moja.

Vilevile, imebainika kuwa baadhi ya sauti hizi zinajitokeza katika maneno ya

kukopwa kutoka lugha ya Kiarabu na kurasimishwa katika mfumo wa Kiswahili

kama ulivyo lugha nyinginezo za Kibantu.

Aidha, tunadhani shida inayokanganya wapenzi wa Kiswahili kuhusu

miundo ya silabi za Kiswahili inaweza kutatuliwa iwapo fonimu katika kila neno

itaandikwa kwa kutumia alama au hati za unukuzi makinifu ya kimataifa hata

katika kiwango cha silabi. Hivyo basi, hati hizi za unukuzi makinifu zinaweza

kudhihirika katika uchanganuzi wa muundo wa silabi hasa {KI} kama tunavyoona

katika mifano ifuatayo iliyoandikwa kwa kutumia chapa iliyokoza na kwa italiki:

Chakula = /$ʧa$ku$la$/ sio /$cha$ku$la$/

 KI KKI

Washa = /$wa$ʃa/ sio /$wa$sha/

 KI KKI

Thamani = /$θa$ma$ni$/ sio /$tha$ma$ni$/

 KI KKI

Dhana = /$ða$na$/ sio /$dha$na$/

 KI KKI

Uhakiki wa Fonimu na Miundo ya Silabi za Kiswahili 115

Ng’oa = /$ɳɔ$a$/ sio /$ng’o$a$/

 KI KK I


Lugha = /$lu$ɤa$/ sio /$lu$gha$/

 KI KKI

Kimsingi, fonimu zilizochanganuliwa na kuandikwa kwa herufi zaidi ya moja

zinaweza kushughulikiwa kwa kutumia hati ya unukuzi makinifu ama kwa

kurejelea alama zilizopendekezwa na Nchimbi (1995:36) yaani / ƅ (mb), Ŋ (nd), N

(ng), Ɲ (nj)/ au kutumia visaidizi kama vile /᷇mb, ᷇nd, ᷇ng, ᷇nj/ au /

n

d, m

b, n

g,

n

j/

(Mwita, 2007: 65). Tunajua kuwa sehemu hii huzua utata na kutokubaliana

miongoni mwa wanaisimu wengi wa Kiswahili. Utata huu hutokea kwa sababu

kuna baadhi ya wanazuoni wanaoshikilia kwamba sauti ng’ong’o hasa [mb, nd, ng,

nj] si fonimu. Hata hivyo, ithibati zinaonyesha kuwa fonimu mbili zinaweza

kutamkwa kama sauti moja kama tunavyoona miongoni mwa fonimu vikwamizwa

hasa /th, dh/.

Kulingana na Mwita (2007:60-61), ithibati zifuatazo zimetolewa kufafanua

kuwa sauti ng’ong’o zinazounda fonimu moja hutamkwa kama sauti moja:

i. Unazalishaji hutokea iwapo sauti nazali itafuatwa na sauti nyingine isiyo

nazali kama tunavyoona baina ya /n/ na /d/:

 Fonimu Fonimu

[+nazali] [-nazali] = n [+nazali] d [-nzali] = [nd]

ii. Fonimu ng’ong’o huundwa kutokana na sauti pamwe hasa zinapotokea

mwanzoni mwa silabi na aghalabu hutajwa hivyo zinapochukua muda ulio

sawa ukilinganishwa na fonimu nyingine katika lugha hiyo moja husika

(Ewen, 1982 akirejelewa na Mwita, 2007:61). Hii inamaanisha kwa mfano,

katika neno kama vile mboga, fonimu ng’ong’o /mb/ huja mwanzo kabla ya

irabu /a/ hivyo basi hutokea mwanzoni mwa silabi.

iii.Sauti ng’ong’o huunda silabi moja na hutamkwa kama sauti moja kama

tunavyoona katika maneno kama vile: shamba = /sha.mba/ na kenda =

/ke.nda/.

Iwapo alama za Nchimbi (1995) zinaelekea kutoungwa mkono na wanaisimu wa

Kiswahili basi alama zilizobuniwa na Mwita (2007: 65) hasa /

n

d,

m

b, n

g,

n

j/ na 

116 Kioo cha Lugha Juz. 13

zinazodhihirika pia miongoni mwa lugha nyinginezo za Kibantu huweza kutumiwa

au kutumia alama saidizi kama vile /᷇mb, ᷇nd/, ᷇ng, ᷇nj/. Hali hii inaweza kutupa

mifano ya silabi kama ifuatayo:

Mboga = /$᷇mbo$ga$/ au / $

m

bo$ga$/ sio /$mbo$ga$/

 KI KI KKI

Kanda = /$ka$᷇nda$/ au /$ka$ n

da$/ sio /$ka$nda$/

 KI KI KKI

Ngoma = /$᷇ngo$ma$/ au / $

n

go$ma$ / sio /$ngo$ma$/

 KI KI KKI

Kunja = /$ku$᷇nja$/ au /$ku$ n

ja$/ sio /$ku$nja$/

 KI KI KKI

Kutokana na mifano hii minne, imebainika kuwa sauti moja inawakilishwa na

alama moja. Kwa hivyo, {᷇mbo, ᷇nda, ᷇ngo, ᷇nja} ni silabi zilizoundwa na fungu

konsonanti na irabu. Hali hii inatukumbusha kuwa kimsingi muundo mojawapo wa

silabi ya Kiswahili ni konsonanti (K) na Irabu (I) yaani KI (Aswani, 1995

akirejelewa na Oduma na Odhiambo, 2008:170). Hivyo basi, {mbo} ni silabi moja

iliyoundwa na fungu fonimu moja ya /᷇mb/ pamoja na irabu /o/. Aidha, muundo

mwingine wa silabi ya Kiswahili huweza kuwa Konsonanti, Konsonanti na Irabu

yaani KKI ambapo konsonanti husika huweza kuwa nazali au viyeyusho (Aswani,

1995 akirejelewa Oduma na Odhiambo, 2008:170).

 Kwa hivyo, iwapo silabi huonyesha hali ambapo nazali hutangulia na

kufuatwa na konsonanti nyinginezo basi tunaweza kuwa pia na muundo wa silabi

KKI. Hiyo konsonanti inayofuata nazali husika huweza kuwa kiyeyusho /w/ na /y/.

Kwa mfano:

Kandwa /$ka$᷇ndwa$ au /$ka$ n

dwa$/

K K I KKI

Aidha, muundo wa silabi hasa wa KKI hudhihirika pia katika matumizi ya

kiyeyusho /y/ na /w/ hasa zinapofuata konsonanti nyingine isiyokuwa nazali katika 

Uhakiki wa Fonimu na Miundo ya Silabi za Kiswahili 117

silabi moja. Hivyo basi, tukawa na hali kama vile {pya} yaani /pja/ na vilevile

{pwa} yaani /pwa/. Silabi kama hizo hudhihirika katika mifano ifuatayo:

Mpya = /$m$pja$/ sio /$m$pya&/

 KKI K½II

Mpwa = /$m$pwa$/ sio /$m$pwa$/

 KKI K½I I

3.3 Je, kuna Uwezekano wa kuwa na Miundo mingine ya Silabi za Kiswahili?

Wanaisimu mbalimbali wa Kiswahili wanakubaliana kuwa kuna miundo minne

msingi ya silabi za Kiswahili kama vile I, K, KI, KKI. Hata hivyo, kuna wengine

wanaoendelea kushikilia kwamba kuna miundo mingine zaidi hasa ile inayotokea

katika baadhi ya maneno yaliyokopwa au kutoholewa na yenye silabi za mkopo.

Ijapokuwa pendekezo kama hili linaelekea kuungwa mkono na baadhi ya

wanaisimu, hatudhani kuwa neno linapokopwa na na kutoholewa na hatimaye

kuingizwa katika lugha pokezi basi huelekea kuwa na muundo wa silabi mkopo.

Ukopaji hujumuisha hali ya kuchukua moja kwa moja neno kutoka lugha chasili na

kuliingiza katika lugha pokezi jinsi lilivyo kimuundo. Mathalani, neno ugali la

Kiswahili limekopwa moja kwa moja kutoka Kiswahili hadi Kiingereza jinsi

lilivyo (Hornby, 2010:1613).

Utohozi humaanisha kuchukua neno la lugha chasili na kulinukuu kwa

kuzingatia fonolojia ya lugha pokezi (TUKI, 1990:2) na pia mofolojia ya neno

husika ili kuweza kulandana na kanuni za lugha pokezi. Mathalani, maneno

yaliyokopwa kwa kutoholewa kutoka Kiingereza ni kama vile springi, skrubu,

faksi na elektroni. Maneno kama haya ya kutoholewa yamezua hali kwamba kuna

uwezekano wa kuwa na muundo mwingine wa silabi za Kiswahili hasa KKKI.

Mathalani, neno skrubu hurejelewa kana kwamba lina muundo wa silabi KKKI

(Obuchi na Mukhwana, 2010:95). Neno hili linafafanuliwa kuwa lina silabi mbili

kama vile: {skru} inayoundwa na {KKKI} na {bu} inayoundwa na {KI}.

Tunadhani kuwa hali hii inazua utata mwingi tunapofafanua silabi za

maneno yaliyokopwa kwa kutoholewa. Inaelekea kuwa bado hakuna maafikiano

kamili kuhusu jinsi ya kutamka na kuandika baadhi ya maneno mengine

yaliyotoholewa kutoka lugha za kigeni hadi Kiswahili. Labda hii ndiyo sababu

Kiango (1995:50) alidokeza kuwa kuna utata katika matamshi ya maneno

yaliyotoholewa kama vile afisa na ofisa, na disemba na desemba. Anatamatisha

hoja hii kwa kusema kuwa kuna haja ya kuwapo na makubaliano kuhusu utamkaji 

118 Kioo cha Lugha Juz. 13

hata hivyo ana hofu kuwa matamshi hayo yatakayotolewa na yatakayokubaliwa

yatakuwa ya nani (Kiango, 1995:50). Tunakubaliana na maoni haya ya Kiango

kwa sababu, neno skrubu (TATAKI, 2013:517) hurejelewa pia kama skurubu

(TATAKI, 2013:517). Iwapo hali hizi mbili ni sahihi basi miundo ya silabi

itakayotokea itachukuliwa pia kuwa sahihi kama tunavyoona kati ya (a) na (b):

a). Skrubu /$skru $ bu$/

KKKI KI

b). Skurubu /$sku $ ru $bu/

KKI K I KI

Kutokana na mifano hii, neno (a) lina silabi ya mwanzo inayoundwa na KKKI na

neno la pili (b) lina silabi ya mwanzo inayoundwa na KKI. Swali tunaloweza

kujiuliza ni kuwa silabi gani basi ni sahihi? Aidha, tukifuata uzi huo huo wa kuwa

na vibadala katika matamshi katika maneno yaliyotoholewa basi mwanaisimu

mwingine anaweza kujitokeza na neno ‘sikurubu’ na kuainisha silabi zake kama

vile:

Sikurubu /$si &ku $ru &bu$

 KI K I KI KI

Kuna uwezekano wa kuwa na ‘sikurubu’ iwapo kwa kweli tunataka kuzingatia

kanuni za muundo wa maneno ya Kiswahili. Kama vile tunapopata mlolongo wa

konsonanti katika neno hatuna budi kuuvunjilia mbali mlolongo huo kwa kutumia

mbinu ya uchopekaji kama tunavyoona katika neno la Kiarabu ‘iblis’ yaani /ibli:s/

linalotoholewa katika Kiswahili kama ibilisi yaani /i.bi.li.si/ (Mwita, 2009:54).

Hali ikiwa hivyo basi tunaweza kuvunjilia mbali pia mlolongo wa konsonanti /skr/

katika skrubu na hatimaye kuwa na neno ‘sikurubu’. Hata hivyo, dai hili lingali

linahitaji mdahalo wa wanaisimu.

Kimsingi, maneno ya Kiswahili huundwa kutokana na silabi huru au wazi.

Hivyo basi, silabi hizi za maneno aghalabu huishia na irabu (Kihore na wenz.,

2009:18) isipokuwa maneno ya mkopo (Habwe na Karanja, 2004: 67). Hata hivyo,

si maneno yote ya mkopo huishia kwa konsonanti. Hii ni kwa sababu maneno ya

mkopo na hasa yaliyotoholewa hufaa kuchukua sifa za kifonolojia na kimofolojia

za lugha pokezi. Kama vile, neno la Kiarabu ‘sultan’ hutoholewa katika Kiswahili

kama sultani ambapo irabu /i/ huongezwa mwishoni (Mwita, 2009:54). 

Uhakiki wa Fonimu na Miundo ya Silabi za Kiswahili 119

Kulingana na hoja tulizodokeza hapo juu kuhusu silabi za mkopo, hatudhani

kuwa kuna uwezekano wa kuwa na miundo mingine zaidi. Hali inayotokea ya

kuwa na KKKI kuashiria silabi mkopo ni jambo linalotokea kwa sababu ya shida

ya namna ya kutamka maneno ya mkopo kwa njia iliyo bora kutoka lugha

nyingine. Hata hivyo, tukizingatia kanuni ya utohozi ya kufuata fonolojia na

mofolojia ya lugha pokezi hatuwezi kuwa na hali kinzani kama tunavyoona baina

ya skrubu na skurubu ambayo yanaleta miundo miwili tofauti ya silabi yaani KKKI

katika /skru/ na pia KKI katika /sku/. Maneno yote mawili huchukuliwa kuwa

sanifu na kufasiliwa katika kamusi za Kiswahili. Hata hivyo, mwanazuoni wa

taaluma ya fonolojia atachukua muundo gani kuwa sahihi? Hivyo basi, makala hii

inashikilia kuwa kuna miundo minne ya silabi za Kiswahili na miundo mingine

zaidi inayodokezwa haina msingi. Mtazamo huo wa kuwa na miundo minne

hutokana na msingi wa Kanuni ya Alfabeti ya Kifonetiki ya Kimataifa ya kuwa

sauti moja iwakilishwe na alama moja. Sauti hiyo inaweza kuwa yenye herufi moja

au mwambatano wa herufi hata hivyo hutamkika kama sauti moja. Aidha, alama

hizo za kifonetiki ndizo hufaa kuzingatiwa katika udhihirishaji wa miundo ya

silabi za maneno ya Kiswahili ili kupunguza mikanganyo baina ya wanaisimu.

3.4 Je, Viyeyusho hufaa Kurejelewa kama Konsonanti au nusu irabu katika

 Uainishaji wa Miundo ya Silabi za Kiswahili?

Ikumbukwe kuwa kuelewa miundo ya silabi za Kiswahili kunahitaji ung’amuzi wa

dhana ya fonimu na pia idadi kamili ya fonimu za Kiswahili pamoja na sheria za

ufonimu. Maelezo yanayotolewa na Kihore na wenz. (2009:15) ya kuwapo kwa

konsonanti 23 na viyeyusho 2 huelekea kuwafanya wanaisimu wengine

kuvidhukuru fonimu viyeyusho kama aina nyingine za fonimu hivyo basi si aina

mojawapo ya konsonanti. Kwa hivyo, maelezo hayo huweza kudokeza maana

nyingine kwamba huenda kuna makundi matatu ya fonimu kama vile irabu,

konsonanti na viyeyusho.

Kwa upande mwingine, wanaisimu wengine hufafanua viyeyusho moja

kwa moja kama aina za konsonanti miongoni mwa makundi mengine kama vile

vipasuo, vikwamizo, vipasuo kwaruzo na likwidi (Habwe na Karanja, 2004:50).

Hata hivyo, swali linaloweza kuchipuka ni kwamba: kwa nini katika orodha ya

makundi ya konsonanti fonimu viyeyusho /w, j (y)/ hukubaliwa moja kwa moja

kama aina za konsonanti yenye jina jingine la viyeyusho? Hata hivyo, wakati wa

kuzitumia katika uainishaji wa miundo ya silabi konsonanti hizi huanza kurejelewa

kivingine kama nusu vokali (½V) au nusu irabu (½I). Mathalani, Mgullu (1999:76)

anarejelea fonimu /j (y)/ kama nusu irabu katika mfano ufuatao:

Afya = (a) + (f+y+a)

 I K+½I+I

120 Kioo cha Lugha Juz. 13

Habwe na Karanja (2004:68) hurejelea pia /w, j (y)/ kama nusu vokali katika

mfano ufuatao:

Pigwa = pi-gwa

 K+½V+V)

Obuchi na Mukhwana (2010:93) wanatoa pia mfano wa matumizi ya nusu irabu

kama vile:

 Mwizi = mwi -zi

 K ½I I + KI)

Mgullu (1999:67) anatambua kuwa kuna fonimu viyeyusho /w/ na pia /j(y)/ katika

orodha ya fonimu za lugha ya Kiswahili. Hata hivyo, katika ukurasa mwingine

hatambui kuwapo kwa viyeyusho miongoni mwa makundi mengine ya konsonanti

kama vile vikwamizwa, vizuiwa, nazali, vizuiwa kwamizwa, kitambazi na

kimadende. Aidha, tunadhani kuwa fonimu hizi /w, j(y)/ ni konsonanti kamili moja

kwa moja hata hivyo hupewa jina jingine kama viyeyusho kwa sababu huundwa

kutokana na mabadiliko ya kifonolojia ya vokali kuwa nusu vokali. Uundaji wa

viyeyusho hutokana na mchakato wa mabadiliko ya kifonolojia jinsi tunavyoona

fonimu /ch/ ikiundwa kutokana na mabadiliko ya kifonolojia yanayoitwa

ukaakaishaji. Licha ya kwamba /ch/ huundwa na mabadiliko yanayoitwa

ukaakaishaji, fonimu hii hairejelewi kama fonimu ukaakaishaji jinsi wanazuoni

wengine wanavyoita fonimu viyeyusho /w, y/ kama nusu irabu au nusu vokali.

Ili kujenga msingi imara wa mtindo wa kuandika miundo ya silabi za

Kiswahili, inafaa turejelee Alfabeti ya Kifonetiki ya Kimataifa (AKIKI). Ishara

hizi za AKIKI zikitumiwa basi mifano inayokanganya na inayotolewa katika

miainisho mbalimbali ya silabi za Kiswahili kama vile (K½VV, KK½VV)

itaepukwa. Naye, Lyons (1981:69) anatujuza kuwa kanuni msingi ya kuundwa

kwa AKIKI ilikuwa kwamba tuwe na alama moja ya kuwakilisha kila sauti na iwe

alama inayoweza kutambuliwa katika lugha husika na iwapo alama haipo basi

kuna haja ya kuongeza kisaidizi juu ya sauti hizo ili kuipa hadhi ya ufonimu.

Kama vile, fonimu /᷇nda/ yenye maana sawa na /Ŋa/ kwa mujibu wa Nchimbi

(1995:36) imeongezewa alama saidizi ili kuweza kuitambua kama fonimu.

Maelezo haya yanatusaidia kung’amua kwamba ingawa silabi aghalabu huundwa

kwa konsonanti na vokali au hata vokali pekee, kuna sauti zenye usonoranti kama

vile nazali, kimadende na kitambazi zinazoweza kuunda silabi zikiwa pekee

(Batibo, 2000:176). 

Uhakiki wa Fonimu na Miundo ya Silabi za Kiswahili 121

Hivyo basi, tunadhani kuwa anazorejelea Batibo ni zile fonimu ng’ong’o

kama vile /m, n/ pamoja na /ny, ng’, n , , ng, nd/ zinazoundwa kutokana na

usilimishwaji na pia fonimu /l/. Kwa hivyo, sauti ng’ong’o hasa zenye herufi mbili

zinafaa kuwakilishwa kwa alama moja ya kifonetiki kama tunavyoona baina ya

/th, dh, gh, sh, ch/ zenye alama maalum. Alama hizo tayari zinadokezwa na Mwita

(2007: 65) kama vile /n

d, m

b, n

g na n

j/ au tunaweza kutumia alama saidizi kama vile

/᷇ , ᷇nd/, ᷇ng, ᷇n /. Aidha, istilahi kama vile konsonanti au irabu zitumiwe badala ya

kutumia majina yanayodhihirisha aina za konsonanti au irabu. Hivyo basi, fonimu

husika hufaa kurejelewa moja kwa moja kama irabu au konsonanti na sio kwa

msingi wa utamkaji wake au mchakato wa uundaji wake kama tunavyoona katika

viyeyusho. Hii ni kwa sababu uainishaji wa fonimu aghalabu hufanywa kwa

kutumia alama kama vile I/V (irabu/vokali) na K (konsonanti) bila kujishughulisha

na aina zake.

4.0 Hitimisho

Kama zilivyo lugha nyinginezo, kuna fonimu za aina mbili za Kiswahili nazo ni

fonimu irabu na konsonanti. Aidha, makala inaunga mkono msimamo kuwa

Kiswahili kina fonimu irabu 5 msingi kama vile /a, e, i, o, u/ na fonimu konsonanti

29 kwa mtazamo wa skuli ya Nchimbi (1995). Fonimu hizo ni kama vile: / , t, ʧ, k,

 , d, Ɉ, g, , ɲ, ɳ, n, , θ, s, ʃ, h, , ð, , r, l, , , ɤ, , nd, ng, nj/. Iwapo alama za

fonimu hasa / ƅ (mb), Ŋ (nd), N (ng), Ɲ (nj)/ zilizopendekezwa na Nchimbi

(1995:35) au za Mwita (2007: 65) hasa /

n

d, m

b, n

g na n

j/ hazijakubaliwa na

wanaisimu wengi basi aghalabu tunahimizwa kufuata kanuni za wanafonetiki wa

kimataifa za kutumia alama kisaidizi kama alivyoeleza Trubetzkoy (1969) na

hatimaye kuwa na maumbo ya fonimu kama vile /᷇mb, ᷇nd, ᷇ng, ᷇nj/. Maumbo ya

fonimu kama vile /᷇ , ᷇nd, ᷇ng, ᷇n / au /n

d, m

b, n

g na

n

j/ huweza kutumiwa na

wanaisimu wa Kiswahili kwa kufuata msingi wa kanuni za Alfabeti ya Kifonetiki

ya Kimataifa. Kanuni mojawapo ni kuwa na alama moja ya kuwakilisha sauti

moja. Hiyo sauti moja inaweza kuwa irabu pekee, konsonanti pekee au

mwambatano wa konsonanti kama tunavyoona katika /ʧ (ch), ɲ (ny), ɳ (ng’), θ (th),

ʃ (sh), ð (dh), ɤ (gh)/.

Iwapo, msingi wa uundaji silabi ni konsonanti na irabu, basi hatuna budi

kushikilia uzi huo huo mmoja na hatimaye kutambua miundo ya silabi za

Kiswahili kama alivyoeleza Nchimbi (1995:36) kama vile (I, K, KI, KKI) au (V,

K, KV, KKV). Aina nyingine ya muundo wa silabi kama vile KKKI inayodaiwa

kuwa hutokana na maneno ya kutoholewa ingali ina utata kwa sababu baadhi ya

maneno hayo huweza kudhihirisha mifumo miwili ya maandishi kama vile skrubu

na skurubu. Aidha, fonimu zinazounda silabi aghalabu hufaa kurejelewa kwa

kutumia alama au hati za unukuzi makinifu ya kimataifa kwa kufuata kanuni kuwa 

122 Kioo cha Lugha Juz. 13

kila sauti au kitamkwa kimoja kiwakilishwe na alama moja au kutumia alama

kisaidizi.

Marejeleo

Akidah, M. A. (2013). ‘Phonological and Semantic Change in Language Borrowing. The

Case of Arabic Words Borrowed into Kiswahili’, katika International Journal of

Education and Research, 1(4), 1-20. Kutoka www.ijern.com/images/April2013/42.pdf.

Ashton, E. O. (1951). Swahili Grammar. Kenya: Longman.

Batibo, H. (2000). ‘Systems in the Sounds of Africa’, katika African Voices. An

Introduction to the Languages and Linguistics of Africa. Southern Africa:

Oxford University Press, 160-196.

Cable, S. (2009). Some Basic Facts about the Dholuo Language. Kutoka

people.umass.edu/scable/LING748-FA09/Materials/Handouts/DholuoBasics.pdf.

Cable, F. (2010). Some Basic Facts about the Gikuyu Language. Kutoka

http://people.umass.edu/scable/LING404-FA10/Materials/Gikuyu_Basics.pdf.

Choge, S. (2009). ‘Understanding Kiswahili Vowels’, katika The Journal of Pan African

Studies, 2 (8), 62-77. Kutoka

http://www.jpanafrican.org/docs/vol2no8/2.8_UnderstandingKiswahiliVowels.p

df.

Coxhead, P. (2006). Natural Language Processing and Application: Phones and

Phonemes. Kutoka https://www.cs.bham.ac.uk/~pxc/nlp/NLPA-phon1.pdf.

De Lacy, P. (2009). Morpho – Phonological Polarity. Kutoka

www.paudelacynet/polarity/delacy-2009-Morphophologicalpolarity.pdf.

Fromkin, V., Rodman, R. na Hyams, N. (2007). An Introduction to Language. Boston:

Thomson Wadsworth.

Furumoto, M. (2015). ‘On the Copula in the Kikae Dialect of Swahili’, katika Swahili

Forum, 22, 20-41. Kutoka

http://afrikanistik.gko.uni_Leipzig.de/Swafo/images/documents/SF_22_Furumo

to.pdf.

Habwe, J. na Karanja, P. (2004). Misingi ya Sarufi. Nairobi: Phoenix Press.

Higgins, H. A. (2012). Ikoma Vowel Harmony: Phonetics and Phonology. Kutoka

http://www.sil.org/systems/files/reapdata/12/83/13/1283136465216248246553506

614061697303369/e_book_43_Higgins_Ikoma_Vowel_Harmony.pdf.

Hornby, A. S. (Mh.) (2010). Ox ord Ad anced Learner’s Dictionary (8th ed.). Oxford:

Oxford University Press.

Kiango, J. G. (1995). ‘Uundaji wa Msamiati Mpya katika Kiswahili: Zoezi Lenye Njia

Mbalimbali’, katika Kioo cha Lugha, 1 (1), 46-54. Dar es Salaam: Chuo Kikuu

cha Dar es Salaam.

Kihore, Y. M., Massamba, D. P. B. na Msanjila, Y.P. (2009). Sarufi Maumbo ya

Kiswahili Sanifu (SAMAKISA). Chuo Kikuu cha Dar es Salaam: TUKI.

Uhakiki wa Fonimu na Miundo ya Silabi za Kiswahili 123

Longhorn (2011). Kamusi ya Karne ya 21. Nairobi: Longhorn.

Lyons, J. (1981). Language and Linguistics: An Introduction. Cambridge: Cambridge

University Press.

Mgullu, R. S. (1999). Mtalaa wa Isimu. Nairobi: Longman.

Mwangi, I. (2007). ‘Swala la Alofoni (Zipo au Hazipo?) katika Ufundishaji wa Fonolojia

ya Kiswahili’, katika Kiswahili na Elimu Nchini Kenya, 93-102. Nairobi:

Twaweza Communications and CHAKITA-Kenya.

Mwangi, P. I. (2011). ‘Nasal Consonant Processes in Standard Kiswahili’, katika Baraton

Interdisciplinary Research Journal, 1 (1), 77-84. Kutoka

http://ueab.ac.ke/BIRJ/download/birj_volume_1_no_1/Nasal%20consonant

%20Processes%20inStd%20Kiswahili.pdf.

Mwaniki, I. N. (2013). ‘The Underlying Reality of Phonological Simplification of Loan

Words by Speakers of Gikuyu’, katika International Journal of Education and

Research, 1 (8), 1-8. Kutoka http://www.ijern.com/journal/August-2003/52.pdf.

Mwansoko, H. J. M. (1995). ‘Shadda Katika Kiswahili,’ katika Jarida la Kiswahili, 1 (1),

15-20, Dar es Salaam: E.S.C. Ltd.

Mwita, L. C. (2007). ‘Prenasalization and the IPA’, katika UCLA Working Papers in

Phonetics. 106, 58-67. Kutoka

http://www.ku.ac.ke/schools/humanities/images/stories/2016/scholarship.pdf.

Mwita, L. C. (2009). ‘The Adaptation of Swahili Loanwords from Arabic: A ConstraintBased Analysis’, katika The Journal of Pan African Studies, 2 (8), 46-61.

Kutoka

http://www.jpanafrican.com/docs/vol2no8/2.8_Adaptation_OfSwahiliLoanword

s.pdf.

Nchimbi, A. S. (1995). ‘Je, Mang’ong’o ni Fonimu au si Fonimu katika Kiswahili

Sanifu?’ katika Baragumu, 25-39. Maseno: Chuo Kikuu cha Maseno.

Obuchi, S. M. na Mukhwana, A. (2010). Muundo wa Kiswahili. Ngazi na Vipengele.

Nairobi: A~Frame Publishers.

Oduma, R. na Odhiambo, K. (2008). ‘The Adequacy of CV Phonololgy in Syllabifying

African Languages: The Case Study of Kiswahili Loanwords in Ateso’, katika

Nadharia katika Taaluma ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika, 167-174. Chuo

Kikuu cha Moi: Moi University Press.

Okombo, D. O. (1982). ‘Dholuo Morphophonemic. A Generative Framework’, katika The

Language and Dialect Atlas of Kenya Supplement 2. Berlin: Dietrich Reimer.

Ontieri, J. O. (2015). ‘Phonological Influences of First Language on Kiswahili: A Case

Study of Kenyan Bantu Languages’, katika International Journal of Science and

Research, 4 (1), 2522-2526. Kutoka

https://www.ijsr.net/archive/v4i1/SUB15856.pdf.

Owino, D. (2003). Phonological Nativization of Dholuo Loanwords. Doctor of

Philosophy Thesis, University of Pretoria, South Africa. Kutoka

www.upetd.up.ac.2a/thesis/available/etd-02092004-

112729/unrestricted/00thesis.pdf.

Polome, E. C. (1967). Swahili Language Handbook. Washington: Center for Applied

Linguistics.

124 Kioo cha Lugha Juz. 13

Simala, I. K. (1995). ‘Uziada wa Sauti (Alofoni) za Kiswahili Sanifu’, katika Baragumu,

41-49. Maseno: Chuo Kikuu cha Maseno.

Starzmann, P. (2014). A Dialectology of Central Kenyan Bantu: Quantitaive and

Qualitative Analysis. Kutoka

https://www.iaaw.hu_berlin.de/de/afrika/linguistik-undsprachen/veranstaltungen/afrikalinguisticscheskolloquium/papersunintersemester-2013-14/handout_starsmann_28_01_2014.pdf.

TATAKI (2013). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Toleo la 3. Nairobi: University of Dar es

Salaam and Oxford University Press.

TUKI (1990). Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha. Dar es Salaam: Chuo Kikuu cha Dar es

Salaam.

TUKI (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Toleo la 2. Nairobi: Oxford University Press.

Trubetzkoy, N. S. (1969). Principles of Phonology. Berkeley and Los Angeles: University

of California Press.

Tucker, A. N. (1994). A Grammar of Kenya Luo (Dholuo). Koln: Rudiger Koppe Verlag.

Whiteley, W. H. (1956). Studies in S ahili Dialect 1: Ki tang’ata. East African Swahili

Committee.

Yule, G. (1996). The Study of Language. 2

nd Ed. Cambridge: Cambridge University Press.