Nyakiiru Kibi pdf-2



Fasilu ya Tatu


Taswira
615
Habari ilienea
Watu wakaisikia
Kawamara wametua
Vijana wa kuvutia.
616
Wana mioyo ya wema
Wanagawa bure nyama
Na adabu na heshima
Na nguo wamevalia.
617
Kwa kasi ilisambaa
Habari ikazagaa
Watu wakaja manria
Wageni kuangalia.
618
Habari ikasaflri
Hadi katika kasiri
Ya Omukama amiri
Ntumwa akaisikia.
619
Akataka sulutani
Waitwe mara wageni
Kuwahoji atamani
Ajue walichojia.
620
Akapelekwa tarishi
Mwenye mbio mtumishi
Aupeleke utashi
Wa mkuu wa jamia.
621
Mithili ya mbayuwayu
Akenda mjumbe huyu
Anahema kama kuyu
Kwa mbio kuzidmua.
622
Kwake Nyakiru mgeni
Kabisha kangia ndani
Akisha subalherini
Amri kaitongoa.
623
“Mtukufu Omukama
Simba anayenguruma
Mume wa waume wema
Wageni awamkia.
624
“Mtukufu wajamala
Anasema halahala
Leo msende kulala
Kabula ya kumwendea.
625
“Mtukufu utashiwe
Leo mfike mpewe
Atakayo muambiwe
Na kisha mtarejea.”
626
Akaridhi muungwana
“Twashukuru maulana
Tu watumwa wake bwana
Wito twauitikia.”
627
Kamwita Kanyamaishwa
Kumwarifu alopashwa
Kuwa wameamrishwa
Kigarama kwelemea.
628
Wakawaita wenzao
Kuwapa ujumbe huo
Wafanye maandalio
Ikuluni kwelekea.
629
Wakavalia vizuri
Ngozi zisizo dosari
Wakisha kuwa tayari
Safari wakabandua.
630
Wakaenda kishujaa
Silaha zang'aang'aa
Kigarama wakangia
Mukama kawapokea.

Taswira
631
“Wapi mlikotokea
Wapi mnakokwendea
Kazi gani mwafanyia
Kujua natamania.”
632
Wakamjibu vijana
“Twasikia maulana
Nasi tu radhi kunena
Yote kukutobolea.
633
“Sisi, ewe Mtukufu
Tu wawindaji hafifu
Nasaba zetu dhaifu
Tu wanyonge twazagaa.
634
“Twazagaa e Jalali
Karibuni hata mbali
Tukitafuta fadhili
Nyakiru akatongoa.
635
“Kibumbiro ni nyumbani
Kiziba sisi wageni
Bali tunayo imani
Simba utatujalia.
636
“Kuwinda ni kazi yetu
Toka utotoni mwetu
Kuivinjari misitu
Ndiyo ya kwetu tabia.
637
“Twajua kila mnyama
Kila ndege mwenye nyama
Na misimu ya kuhama
Ya madege twaijua.
638
“Twajua misitu gani
Husitawisha kongoni
Kuro, swala hata nyani
Makazi yao twajua.
639
“Twajua kila kiumbe
Toka kwa simba kabambe
Hadi kwa fisi mzembe
Mahiri wa kudoea.
640
“Tunajua tamu nyama
Hutoka yupi mnyama
Na nyama ngumu kuuma
Mnyama gani hutoa.
641
“Tu mafundi wa kuvuta
Kila aina ya nyuta
Pia mapanga kufuta
Na mikuki kuinua.
642
“Japo tu watu hafifu
Sio watu wenye hofu
Japo sio watukufu
Uungwana twaujua.
643
“Tumezurura kutosha
Kadka yetu maisha
Twapenda kubahatisha
Maisha yalotulia.
644
“Kwa fadhilazo mwadhamu
Tu radhi kuishi humu
Tufanye masitakimu
Na kuwa zako raia.
645
“Tu radhi kutumikishwa
Tu radhi kuamrishwa
Hili litahakikishwa
Muda ukitupatia.
646
“Sisi na wetu vijana
Tuko radhi kupigana
Ili kudumisha jina
La enzi yako murua.
647
“Hatuogopi adui
Katika dunia hii
Madhali bado tu hai
Huna cha kukihofia.
648
“Vita ni chakula chetu
Damu ni kinywaji chetu
Adui zako ni zetu
Wajapo watatujua.
649
“Nchi hii ya Kiziba
Ni nchi yenye haiba
Wana bahati Baziba
Humu wanaolowea.
650
“Una bahad Mukama
Kutawala nchi njema
Yenye maziwa na nyama
Kama hii twakwambia.
651
“Kwa kuwa twaitamani
Tu radhi kuiauni
Ukikiri masikani
Yetu hapa kujengea.”
652
Akiyasikiya haya
Mukama kafurahiya
Kaona siyo wabaya
Hawa wawinda shujaa.
653
Kakuna upara wake
Na ndevu na mvi zake
Kasugua bongo zake
Kaona watamfaa.
654
Kaona watamfaa
Wataja mpigania
Nchini akiridhia
Kuwaruhusu kukaa.
655
Watoto wake wachanga
Wanaonyesha ujinga
Wataogopa mapanga
Hapo watakapokua.
656
Watakaposhika enzi
Watahitaji walinzi
Wapepezi na wakanzi
Ili kuwahudumia.
657
Kwani uzee balaa
Kaona unamtwaa
Ujana wamuambaa
Yazimika yake taa.
658
Na hivyo akatamka
“Ombi limekubalika
Mwaweza kujenga maka
Kizibani kulowea.
659
“Nawapenda wanaume
Wenye nyoyo za kiume
Na maungo ya kidume
Kuja kunitumikia.
660
“Napenda waume bora
Wasochelea madhara
Walo tayari kukera
Adui kuniulia.
661
“Mnaweza kwendelea
Makazi kujijengea
Kibali nimekitoa
Hamna cha kuhofia.”

Taswira
662
Wakamshukuru sana
Hilo alipolinena
Na kuhakikisha tena
Kuwa watamfalia.
663
Kwa furaha wakatoka
Waongea na kucheka
Kwani wamekubalika
Kadka nchi kukaa.
664
Wakirudi majumbani
Wakaweleza wandani
Mambo yote Kikaleni
Ambavyo yamewendea.
665
Pia wakawaambia
“Wake zetuni sikia
Mnaweza kupania
Mashamba kujilimia.
666
“Kama wanawake wote
Mabibi nchini popote
Mlime, maji mchote
Hamna cha kuhofia.
667
“Udongo mwanze kuchimba
Tupandikize migomba
Mpalilie mashamba
Na ndizi kujichumia.
668
“Utapofika msimu
Wa maharage matamu
Mpande ili kukimu
Wa'me zenu na jamaa.
669
“Sisi waume vijana
Kuwinda hatutakana
Tutazidi kupambana
Na nyang'au wa dunia.
670
“Tutazidisha usasi
Wa nyama bila kiasi
Tujiletee nemsi
Na kuwalisha raia.
671
“Pia tutajizoeza
Mishale kuipaaza
Na panga kuzipepeza
Na mikuki kurushia.
672
“Tufanye jeshi la nguvu
La wachache wa mabavu
Kuja kufuta maovu
Ambayo yamezagaa.”
673
Na kwa kwandalia hili
Mwendo hawakubadili
Raha hawakukubali
Tabu walivumilia.
674
Waendelea kuuwa
Wanyama wanaoliwa
Na nyama yao kugawa
Kwa wakulima raia.
675
Wauwapo kwa upanga
Nyama mmoja mjinga
Hukata na kumchonga
Watu wakawagawia.
676
Hivyo wakajulikana
Kwa wazee na vijana
Watumwa na waungwana
Wote wakawasifia.
677
Wakasema “Hawa watu
Ni kama wazazi wetu
Bahad kwa nchi yetu
Kuwa wameijilia.
678
“Hawa kwetu walishaji
Matumbo washibishaji
Wagawi si wafujaji
Mengi wastahilia.”
679
Nyama ikawa nchini
Kama ndizi za shambani
Watu wakawa rahani
Kwa nyama kuwazidia.
680
Mifugo haWakuchinja
Nyama yao kuionja
Ng'ombe mazizi wavunja
Jinsi walivyozidia.
681
Watu wakatajinka
Maziwa yakafurika
Nyama zikamiminika
Nchini zikaenea.
682
Ukanong'ozana umma
“Wameileta neema
Hawa wawindaji wema
Mizimu wawape dia.
683
Nyamuhanga wabariki
Waondokane na dhiki
Wape mali kwa malaki
Waitawale dunia.
684
“Wape faraja Mugasha
Uwaepushe rabusha
Nyakalembe wa maisha
Uwaepushe na njaa.
685
“Irungu wape salama
Washinde kila mnyama
Tuzidi kula minyama
Miungu twawalilia.”
686
Na huu wote wakad
Mutalala ameketi
Nyumbani kama hayati
Akila ha kujinywea.
687
Kachutama kama nguu
Ashindwa kwinuka juu
Au kwinua mguu
Unene wamzidia.
688
Unene wamzidia
Kama kameza dunia
Na bado ajipakia
Vyakula kwa magunia.
689
Ulezi vyungu na vyungu
Na matoke kwa mikungu
Vitamu hata vichungu
Kinywanimwe hupotea.
690
Maziwa yenye shahamu
Maji yenye chumvi tamu
Mapombe nayo dawamu
Huyanywa akibugia.
691
Dunia ina mizungu
Imewazua wazungu
Na Mutalala mwenzangu
Yu mzungu nakwambia.
692
Mzungu hawezi shiba
Japo angemeza mamba!
Nguruwe katika shamba
Zimwi kadka dunia.
693
Akisha kula bahau
Ngoma aliisahau
Ameshapata nafuu
Ya tumbo kujijazia.
694
Nafuu amesha pata
Kitambi kimeshaota
Kwani kuanza matata
Goma shinda kuwania?
695
Hajui kushika panga
Wala ngao kujikinga
Vita kwake ni ujinga
Kwani kuvifuatia?
696
Ndivyo alivyoamini
Mutalala ugenini
Na hii yake imani
Vema alishikilia.
697
Wenzake aliwacheka
Kuona wanatumika
Misuli yajisimika
Matumbo yawabonyea.
698
“Maisha ni kula sana
Na kunywa kulewa sana
Na kujizalia wana
Na mwishowe kujifia.
699
“Kamwe si kutangatanga
Kama nzige kwenye anga
Bila makazi kujenga
Na tumbo kujilelea.”
700
Ndivyo alivyowambia
Mutalala asojaa
Na sasa twamuachia
Yake tumeyasikia.
701
Yake tumeyasikia
Sasa tuzidi kujua
Nyama za wale shujaa
Nini zilichokizaa.
702
Kwanza na itambulike
Ile Ngoma ya makeke
Kachwankizi Ngoma pweke
Nyakiru aliitwaa.
703
Nyumbani kaisetiri
Aitunza kwa hadhari
Kuigusa ni hatari
Japo uwe Malikia.
704
Kachwankizi imetua
Hapo imejiketia
Kwa saburi yangojea
Siku yake ya kung'aa.
705
Sasa basi siku moja
Asubuhi ilikuja
Habari yenye faraja
Watu kuwaamkia.
706
Ikaingia habari
Mapema alifajiri
Habari kweli ya heri
“Senene wameingia.
707
“Senene wameingia
Mithili wingu la mvua
Kwa wingi wamezidia
Enyi Baziba sikia.
708
“Enyi Baziba wafane
Enyi walaji senene
Tokeni nje muone
Alichotuangushia.
709
“Alichotuangushia
Mugasha mwenye kujua
Asiyeogopa jua
Mweusi mleta mvua.
710
“Tokeni nje mabibi
Wanaume hawashibi
Leo hadi magharibi
Wajazie magunia.
711
“Tokeni nje madume
Uzembe wenu ukome
Senene muwaandame
Jioni watajendea.
712
“Tokeni nje watwana
Na mihi yenu vijana
Lete senene kwa bwana
Sulutani kujilia.
713
“Tokeni nje watoto
Acheni zenu topito
Kuna mlo motomoto
Washika na kujilia!”
714
Na watu wakaondoka
Kila hirimu na rika
Senene kwenda kusaka
Katika zogo la mvua.
715
Watu wakajifunika
Milumba yenye viraka
Na ngozi wakajivika
Manyuriyu kuyazuia.
716
Na maji yakaanguka
Kwa ghadhabu ya kizuka
Aridhi ikafurika
Mifuo yakachimbua.
717
Meme zinamemetuka
Radi nazo zapasuka
Nchi inatetemeka
Kama ukufi sikia!
718
Wasijali binadamu
Wenye shauku na hamu
Kupata senene tamu
Tumboni kujitilia.
719
Wakajitoma sharini
Kwa ari iso kifani
Na kuyalaza majani
Senene kujishikia.
720
Senene bila vitimbi
Wakaangnka kiwimbi
Wimbi baada ya wimbi
Watu wakajizolea.
721
Senene kawa senene
Kila mahali senene
Kushoto kwako senene
Mbele nyuma na kulia!
722
Kichwani pako senene
Nyayoni pako senene
Nguoni mwako senene
Senene wakazagaa!
723
Katika nyasi senene
Kadka miche senene
Na mitini ni senene
Senene wakaenea.
724
Senene kwenye mashamba
Senene kwenye miamba
Kwenye mapaa ya nyumba
Senene wakatambaa!
725
Senene miti kishika
Matawi yanavunjika
Matunda yanaanguka
Na mashina kupembea!

Taswira
726
Nyumba wakiikalia
Hubonyeza lake paa
Na ndani wakiingia
Nyumba wanairarua!
727
Ndivyo walivyoanguka
Hao senene wa mwaka
Wakazidisha mpaka
Jinsi walivyoenea.
728
Kabula ya siku hio
Senene kwa wingi huo
Hawajakumbana nao
Kiziba kuangukia.
729
Pia tangu siku hio
Watu wanakiri leo
Senene wengi ja hao
Katu hawajatokea.
730
Ntumwa katika nyumbaye
Kuona senene naye
Katamani ajiliye
Utamu kufaidia.
731
Kaamuru watumwaze
Wazanaze na wakeze
Nao wakajitokeze
Senene kumletea.
732
Kaamuru watu wote
Ikuluni mwake mwote
Wapigwe mvua watote
Senene kumshikia.
733
Wakampinga wahenga
Wakamba: “Twahofu janga
Utabaki bila kinga
Sote tukikuachia.”
734
Akasema bila hofu
“Enyi viumbe dhaifu
Mukama ni mtukufu
Siye mfungwa sikia!
735
“Hahitaji asikari
Daima kumsetiri
Kama kwamba yu kauri
Wezi watamvamia.
736
“Semeni yu wapi mtu
Ambaye angethubutu
Kuja Ikuluni mwetu
Mukama kushambulia?
737
“Nendeni enyi wavivu
Toa hapa upumbavu
Lete senene wabivu
Ninataka kujilia.
738
“Senene waliofana
Wa matumbo yalotuna
Na vichwa vilivyonona
Ndio ninahitajia.
739
“Bali si yenu maneno
Na rangi ya yenu meno
Nendeni kwenye mavuno
Wazee mlopumbaa!”
740
Wakaondoka wahenga
Nyuso zimejiviringa
Kuona kawasimanga
Bwana wao kawashua.
741
Katika tufani kali
Manyunyu yenye ukali
Vipara vikahimili
Senene kufuatia.
742
Mukama kabaki hali
Na vijakazi wawili
Vikongwe viso amali
Vyangojea kujifia.
743
Na radi zikapasuka
Dhoruba ikacharuka
Na mvua ikaanguka
Nchi ikaogelea!
744
Nchi ikazamiana
Watu wakaloweana
Senene wafurikana
Kama nyasi wakajaa!
745
Na mvua ikawa mvua
Tufani ikazidia
Radi zikajilipua
Na mbingu zikaungua!
746
Kama panga la maud
Umeme wafuma nti
Na kufyeka katikati
Anga lote kwa sawia!
747
Na senene wajibwaga
Mabwawani na kuoga
Tayari kufanywa mboga
Watu kuwatowelea.
748
Watavunjwa zao mbawa
Na miguu kung'olewa
Na pembe kuchopolewa
Na hawatajitetea.
749
Watakongolewa wengi
Watiwe kwenye mitungi
Na kuchemshwa kwa wingi
Hadi wamejiivia.
750
Wengine watabugiwa
Chunguni wakitolewa
Na wengine watatiwa
Moshini kukaukia.
751
Wakazidia senene
Wanono wenye unene
Kutimia saa nne
Bado tu wanatokea!
752
Na watu wakawapata
Kwa wingi wakawachota
Mihi yote ikaputa
Ikajaa kuzidia.
753
Na kila mtu Kanyigo
Mkubwa hata mdogo
Alikusanya mzigo
Wa senene kujilia.
754
Na bado walendelea
Senene kuzoazoa
Furusa wakitambua
Haiwezi kurejea.
755
Hata Mutalala naye
Bila kujali haliye
Alichukua fimboye
Tufanini kuingia.
756
Akichupa kama chura
Kitumboche chamkera
Senene kiteka nyara
Aliowafumania.
757
Aliwashika mikia
Meno wasije mtia
Wakimuuma hulia
Kisha akawaachia.
758
Hatima aliwashinda
Vichwa alipowaponda
Akaweza kuyapinda
Meno yao ya udhia.
759
Watu wote kijijini
Walitoka majumbani
Hapakubakia ndani
Ila waliougua.
760
Ila waliougua
Na wachache mashujaa
Ambao walibakia
Mipango kujipangia.
761
Wakitengeza mipango
Ya kuingia ulingo
Kwa mikuki na magongo
Himaya kujitwalia.
762
Siku hii waliona
Kaileta Maulana
Kuwawezesha kukana
Wanaowasujudia.
763
Imeletwa na Mizimu
Kuwafanya mahakimu
Juu ya hii kaumu
Isiyo na mtetea.
764
Hivyo walitafakari
Kwa hamu tena kwa siri
Vipi wapate fahari
Ile waliyoijia.
765
Na wakisha kuamua
Silaha walichukua
Na kutoka kishujaa
Kigarama kwelekea.
766
Na mvua ilifuliza
Manyunyu kuyanyunyiza
Na pepo zilipuliza
Kwa shari ya kuzidia.
767
Senene wakianguka
Tokajuu kwa Mahoka
Juu, chini, wafurika
Mawindo ya kujiua.
768
Walikwenda kwa harara
Bila hata kudorora
Waenda kujipa kura
Kwa mikuki na jambia.
769
Senene walifuata
Nyuma yao kuwaita
Waende kuwakamata
Wao hawakusikia.
770
Manyunyu yakiwatosa
Pepo zikiwapapasa
Senene wakiwagusa
Wao wanaendelea.
771
Watu wakiwatazama
Huwafikiria wema
“Hawa wawinda wa nyama
Senene wafuatia.”
772
Nao wakasonga mbele
Bila kujali kelele
Ambazo ziwazingile
Za dhoruba na ghasia.
773
Walikwenda kwa shauku
Kwanyoyoza dukuduku
Kukabili lao juku
Walilojiamulia.
774
Mavazi yalilowana
Baridi iliwabana
Upepo uliwakuna
Bila wao kutambua.
775
Wakaenda, wakaenda
Kilima wakakipanda
Bila taabu na shida
Ikulu wakelemea.
776
Hapo njia ili pweke
Walikuwa wao peke
Raia wasioneke
Senene wajishikia.
777
Na radi zinarindima
Na dhoruba inavuma
Na baridi imeuma
Na inamwagika mvua.
778
Bali hawa wasijali
Waenda kwa nyoyo kali
Na nyuso zenye uvuli
Wa tamaa ya kuua.
779
Walipofika langoni
Langoni pa sulutani
Wakaingilia ndani
Wawili si kuzidia.
780
Nyakiru aliingia
Na Kanyamaishwa pia
Na kumi si kupungua
Langoni wakabakia.
781
Wakajiendea ndani
Na tazama sulutani
Yupo pale sebuleni
Salama kajikalia.
782
Katika enzi kazama
Ametarama kikama
Buni kavu anauma
Kwa raha ametulia.
783
Kakaa kama chuguu
Katulia kama nguu
Mikono hadi miguu
Vikuku amevalia.
784
Tumbole laning'inia
Ja boga lilokomaa
Ungedhani malikia
Ataka kujifungua.
785
Na vijakazi viwili
Vikongwe roho na mwili
Mukama vimekabili
Bwabwaja vyambwatia.
786
Akiwaona vijana
Sulutani akanena
“Karibuni wangu wana
Ili tupate ongea.
787
“Nimechoka na ukiwa
Kinywa sijakifunguwa
Vijakazi wangu hawa
Hawajui kuongea.
788
“Na wala siwalaumu
Ukabwela nao sumu
Wangakuwa na adhamu
Kusema wangalijua.
789
“Na maajuza kunena
Vilevile siyo sana
Meno vinywani hawana
Ni fizi zimebakia.
790
“Ni mkiwa mtawala
Anapokaa mahala
Patovu pa kabaila
Wawezao kuongea.
791
“Hivyo ninyi karibuni
Ijapo mu watu duni
Kujalisi ninadhani
Mwaweza kujaribia.”
792
Na mmoja mjakazi
Macho yake machunguzi
Aliyakodoa wazi
Kwake Kanyamaishua.
793
Kwake macho alikaza
Bila kope kupepeza
Kana kwamba anawaza
Huyu wapi katokea.
794
Akatamka Nyakiru
“Ni mwema wako udhuru
Nasi tunakushukuru
Udhuru kuutongoa.
795
“Bali sisi e dubwana
Hatuji kwa kupatana
Bali twaja kwa hiana
Mauti tumechukua!”
796
Vijakazi kusikia
Vilio wakaangua
Mmoja macho katia
Kwake Kanyamaishua.
797
Na Mukama akakaa
Amepigwa na butaa
Sauti hakuitoa
Macho aliwakazia.
798
Nyakiru akaongeza
“Hatuji kukutukuza
Tunakuja kukukuza
Enziyo kukuambua.
799
“Tunakuja kwa kisasi
Tunakuja kwa maasi
Ili kutakasa nsi
Ambayo umechafua.
800
“Twaja kukupatiliza
Kwa nguvu zake Muweza
Ukiona unaweza
Waweza kujiokoa!”
801
Na hapo Mukama Ntumwa
Tumbo akanza kuumwa
“Mbwa! Wana wa watumwa
Akili zimewapaa!
802
“Akili zimewapaa
Bila nyinyi kuelewa
Mwanena msichojua
Mwaja moto kuchezea!
803
“Watoto mnazo ndwele
Bongonimwenu zitele
Kuthubutu kama vile
Mukama kumtishia!
804
“Ntumwa katu si kabwela
Ntumwamtu kabaila
Kuguswa na mtu fala
Hilo halitatokea!
805
“Mngali wana wachanga
Mmezidiwa ujinga
Akili imewachenga
Nadhari imepungua.
806
“Angalia, angalia
Kuwaonya narudia
Haliwezi kutokea
Mnalolidhamiria!”
807
Nyakiru akatongowa
“Litatokea na kuwa!”
Na papo akainuwa
Mkuki na kumtia!
808
Akamfuma mkuki
Ukaingia kwa maki
Mambo yakawa mkiki
Mukama kamrukia!
809
Kanyamaishwa tazama
Naye pia kamfuma
Mkuki ukamzama
Na Ntumwa akaugua.
810
Akajiuma vidole
Na kupaaza kelele
“Ninakufa wangu ole
Vitwana vimeniua!”
811
Na Ntumwa akageuka
Kitamtn kimetoboka
Damu zampukutika
Akataka kukimbia.
812
Asiweze kaanguka
Hali amefadhaika
Macho yamemkodoka
Adui yamwangalia.
813
Macho akayakodoa
Kwake Kanyamaishua
Kisha akayashushia
Shingoni pake sikia.
814
Palepale kayakaza
Wala hakuyapepeza
Hirizi aichunguza
Kwani ameitambua!
815
Hirizi ni ya ukoo
Mwana wake siku hio
Walipomtoa kwao
Ali amejivalia.
816
Zamani hirizi hiyo
Mwanawe katupwa nayo
Na sasa karudi nayo
Ni leo ayangalia.

Taswira
817
Na hili alipoona
Kajua huyu ni mwana
Mwana wake wa laana
Kashiriki kumuua!
818
Kamba kwa sauti chungu
“Enyi vijakazi wangu
Elezeni ulimwengu
Mwanangu ameniua!”
819
Na hapo akaanguka
Rohoye ikamtoka
Machoye yakafumbika
Na shingo likalegea.
820
Nao vijakazi hao
Wakatoka mbio mbio
Wakalia “Yoo! Yoo!
Mukama wamemuua!”
821
Na wale wakaingia
Nje waliobakia
Wakakuta analia
Kanyamaishwa sikia.
822
Kanyamaishwa kasema
“Moyo wangu una homa
Sikutenda jambo jema
Mtima waniambia.
823
“Maneno nimesikia
Hayati akitongoa
Ati mwana kamuua
Mwana aliyemzaa!
824
“Babangu simfahamu
Mamangu simfahamu
Walakini nafahamu
Kiziba nilitokea.
825
“Na hii hirizi yangu
Tangu utotoni mwangu
Havaa shingoni mwangu
Sijapata kuitoa.
826
“Na mama alinambia
Yule aliyenilea
'Hirizi uliyovaa
Si ya kabwela tambua!'
827
“Nikitazama usoni
Mwake huyu sulutani
Ninaanza kuamini
Yale niliyoambiwa.
828
Nimekufuru hakika
Nimekosea Mahoka
O! Niliyelaanika
Sisitahili afua!”
829
Nyakiiru kampoza
“Kaka wacha kujisoza
Vipi kosa lakuliza
Usilolikusudia?
830
“Na wala huna hakika
Kwamba aliyotamka
Mfu yamethibitika
Ni kweli mia kwa mia.
831
“Tulia tutauliza
Wazee na maajuza
Mambo yote kueleza
Kabula ya kuamua.
832
“Mengl tumesha yatenda
Kukoma hapa ni shida
Tutafululiza kwenda
Hadi mwisho kufikia.”
833
Na vijana kawambia
Maiti kumuinua
Waende kumfukia
Kaburini kumtia.
834
Ndivyo alivyofariki
Huyu dhalimu wa haki
Akilia kwenye dhiki
Hana wa kumtetea.
835
Ndivyo alivyofanki
Akaiacha miliki
Akaacha halaiki
Aliyoiatamia.
836
Ndivyo alivyofariki
Akenda bila rafiki
Kwenenda akadiriki
Kusiko na kurejea.
837
Nayo mvua ikanyesha
Na umeme ukawasha
Dhoruba ikajirusha
Kwa nguvu za kuzidia!
838
Na Nyakiru akasema
“Siwezi kuwa Mukama
Na kuutawala umma
Peke yangu nakwambia.
839
“Kanyamaishwa sikiza
Acha sasa kujiliza
Kitini ninakukweza
Sote tutakikalia.”
840
Kanyamaishwa kakana
Akasema “Haja sina
Sitayakubali tena
Ambayo wanipangia.”
841
Wakabishana kwa nguvu
Saud zikawa kavu
Kila mmoja mvivu
Ufumbuzi kufikia.
842
Nyakiru kasisitiza
Mwenzie kubembeleza
“Mpenzi nakueleza
Vema kiti kukalia.
843
“Tumesafiri pamoja
Tumeteseka pamoja
Na tumeua pamoja
Vipi sasa wanachia?
844
“Tutakalia kwa zamu
Hiki kid cha adhamu
Sote tuwe mahakimu
Watawala wa raia!”
845
Mwishowe bila kutaka
Mwenzie akaitika
Ukafikiwa mwafaka
Wote Bakama wakawa.
846
Kanyamaishwa lakini
Hakutulia moyoni
Mateseko na huzuni
Rohoni vilibakia.
847
Na habari zikafika
Huko nje kwenye nyika
“Mukama kesha ondoka
Mambo yamesha timia!”
848
Watu wote wakatoka
Nyikani wamejitwika
Senene walioshika
Makuu kujionea.
849
Walipofika tazama
Nyakiiru ni Mukama
Na Kanyamaishwa mwema
Kandoye kajikalia.
850
Nyumao wamejikita
Asikari wa matata
Silaha zametameta
Kivita wamekalia.
851
Wenyeji wakauliza
“Ewe mgeni eleza
Nani amekutawaza
Ukama kukupatia?”
852
Nyakiiru kaeleza
“Watukufu sikiliza
Sisi tumejitokeza
Haki zenu kutetea.
853
“Tumeiona dhuluma
Aliyotenda Mukama
Tukashikwa na huruma
Ndipo tulipomuua.
854
“Mwaweza kutuhukumu
Bali hili lifahamu
Hatuji kuwadhulumu
Tujile kuwakomboa.
855
“Kama baya tumetenda
Kwa nyoka kichwa kuponda
Mnaweza kutukinda
Kwani tu wenye hatia.
856
“Chukueni misu yenu
Noeni mikuki yenu
Sisi tu halali zenu
Mnaweza kutuua.”
857
Akimaliza Nyakiru
Kuwaeleza udhuru
Raia wakashukuru
Shangwe wakampigia.
858
Bila kufanya udhia
Wakasujudu raia
Nyakiru wakamwambia
“Nchi umeiokoa.”

Taswira
859
Na wote makabaila
Wakichelea madhila
Wakondoka halahala
Bugandika kwelemea.
860
Huko wakajikusanya
Tayari vita kufanya
Wageni kuwanyang'anya
Enzi waliyochukua.
861
Nyakiiru akatoka
Na jeshi lilopanuka
Akaenda Bugandika
Adui kushambulia.
862
Majeshi yakakutana
Ikawa bimbirishana
Wakatana, wauana
Maid zikazagaa.
863
Maid zalaliana
Damu zafurikiana
Waume wanapambana
Wengine waangamia.

Taswira
864
Na ikifika jioni
Ikadhihiri yakini
Maadui wako chini
Nguvu zimewaishia.
865
Vitani wakajitoa
Na kuanza kukimbia
Hima wakafuatiwa
Wengi wakaangamia.
866
Hapo vita vikakoma
Naye Nyakiru Mukama
Akarudi Kigarama
Mukama kampokea.
867
Na pamoja kwa sawia
Kiti wakakikalia
Watu wakasujudia
Na kuwatii kwa nia.
868
Na wakaitwa wazee
Waje wawaelezee
Ili siri waijue
Yake Kanyamaishua.
869
Na wakiisha tamka
Ikawa hakuna shaka
Mambo yakadhihirika
Jinsi walivyodhania.
870
Kanyamaishwa kalia
Na matanga kukalia
Babaye kukumbukia
Na tendole kutubia.
871
Na matanga yakapita
Kanyamaishwa kapata
Maradhi yenye matata
Asiweze kujinua.
872
Nyakiru akasumbuka
Daima ashughulika
Waganga akiwasaka
Mwenzie kumtibia.
873
Mwisho kaona kijana
Dawa hazina maana
Sahibu azidi sana
Mwilini kudidimia.
874
Na muda ulipopita
Mauti yakamuita
Kifo kikamkamata
Mgonjwa akajifia.
875
Akafa Kanyamaishwa
Kakoma kutaabishwa
Shimoni kateremshwa
Watu wakamlilia.
876
Ndivyo alivyofariki
Huyu kijana wa dhiki
Bila kuacha kisiki
Katika hii dunia.
877
Nyakiru kamlilia
Akalia, akalia
Akamuombolezea
Mwenzi aliyemfaa.
878
Myezi miwili Nyakiru
Katu hakuona nuru
Kijiji hakukizuru
Nyumbani alitulia.
879
Nyumbani alitulia
Matanga kumkalia
Rafikiye wa dunia
Ambaye hatarejea.
880
Na matanga yakiisha
Nyakiru akajikosha
Nyumbani kajiondoshi
Nuru kuiangalia.
881
Akabaki peke yake
Mtawalaji mpweke
Akawa Mukama peke
Kiziba kuangalia.

Taswira
882
Kisha akajenga nyumba
Akaikata na vyumba
Halafu akaipamba
Mapambo ya kuvutia.
883
Akamaliza ujenzi
Akaleta Kachwankizi
Kaiingiza kwa enzi
Iketi na kulowea.
884
Ndoto ikakamilika
Kachwankizi ikatika
Di! di! di! di! kutamka
Enzi mpya kwa raia.
885
Na mjumbe akatoka
Kibumbiro akafika
Moto mpya akateka
Kiziba akarejea.
886
Huu moto wa ukama
Uliwashwa kwa heshima
Ngoma ilipochutama
Usiachwe kuzimia.
887
Mambo yalipotuliya
Nyakiru wakamtiya
Jina la Kibi - Kibaya
Kwani watu ameua.
888
Akalikubali jina
Kwa moyo wa kiungwana
Na ndivyo ajulikana
Katika historia.

Taswira
889
Hapa sasa nakomea
Kituo nimefikia
Nyuma yaliyotokea
Hapa sitasimulia.
890
Nimesema ya kutosha
Na wala sikupotosha
Na hadithi imekwisha
Tamati tumefikia.
891
Mtunzi ni chipukizi
Mugyabuso Mulokozi
Mulokozi ni mzazi
Baba aliyemzaa.
892
Ni kijana atokea
Upeo hajafikia
Makosa ukimtoa
Sana atafurahia.

Maneno ya Kihaya na lugha nyingine za asili
Ubeti
Neno
Maelezo
13
Ruhanga
Mungu Mkuu, Muumba.
27
Kintu
Mwanamume wa kwanza kwa mujibu wa imani za baadhi ya watu waishio mkoa wa Kagera na Uganda ya Kusini.
28
Kikazi
Mwanamke wa kwanza, mke wake Kintu.
31
Mugasha
Muungu wa Ziwa Viktoria, na mtawala wa tufani, mvua, kwa mujibu wadini zajadi katika mikoa ya Kagera, Mwanza na Kusini mwa Uganda. Wasukuma humwita Nyangassa, Wakerewe humwita Mugasa na Waganda humwita Mukasa.
32
Ngassa
(Kisukuma) Nyangassa, Mugasha.
Mukasa
(Kiganda) Mugasha.
33
Nyanja
Nyanza, Ziwa au mto.
Lweru
Ziwa Viktoria.
35
Nyakalembe
Mke wa Mugasha na Muungu wa kilimo kadka dini za jadi.
36
Kasana
Muungu wa uwindaji.
37
Irungu
Muungu wa mapori na uwindaji.
38
Lyangombe
Muungu wa wafugaji.
39
Kaihura-Nkuba
Muungu waradi, mwanawe Mugasha.
40
Wamala
Muungu Kiongozi wa Wachwezi.
Wachwezi
Kundi la Miungu na Mizimu, hususan lile linalohusishwa na Wamala kiukoo.
Huyamala
Huyamaliza.
41
Kagoro
Mtoto wa Wamala, Muungu wa vita.
42
Kilo
Muungu wa usiku.
43
Kasi
Muungu wa kike anayehusika na kilimo.

Rugila
Muungu wa kike anayehusika na uzazi.
59
Mukama
Mfalme, sultani.

Bike
Mtawala wajadi wa Kiziba aliyeuawa na Ntumwa, labda kwenye karne ya 15.
78
Nanga
Ala ya muziki yenye nyuzi saba na umbo kama la mtumbwi.
89
Ngisha
Hirizi.
96
Katonda
Mungu, Muumba.
104
Ukama
Ufalme.
129
Mshonge
Nyumba ya jadi ya Wahaya, Wachaga, naWaganda, ambayo paa lake huteremka mpaka ardhini; haina kuta za udongo au matofali.
133
Kanwa
Mdomo, kinywa.
Matoke
Ndizi zilizopikwa.
139
Kukaga
Kuhisi, kutambua.
144
Ugino
Ufizi.
171
Wazana
Abazana, watumwa wa kike. Mmoja ni muzana.
175
Bami
Machifu au wazee wenye heshima. Mmojani mwami.
178
Habuka
Neno litumikalo kumsalimu mfalme, maana yake kama dhihirika au tokea hadharani.
Lugaba
Mtoaji wa fadhila, mkarimu.
181
Wakazi
Bakazi, wanawake. Mmoja ni mukazi.
199
Ukazi
Hali ya kuwa mwanamke.
203
Mizio
Miziro, miiko.
230
Kanyamaishwa
Jina lenye maana yamtoto aliyeokotwa porini kama mnyama.
247
Kachwankizi
Jina la ngoma ya utawala wa Kiziba ambayo Nyakiiru alikuja nayo kutoka Bunyoro.
249
Kyezailwe
Jina la ngoma lenye maana ya Kilichozaliwa.
250
Kalemaitalula
Ngoma ya utawala. Maana yake haibebeki.
251
Nyabatama
Jina la ngoma, maana yake haikupatikana.

Matama
Mashavu.
252
Tabamulibi
Jina la ngoma ya utawala lenye maana ya Asiyekosa Soko, Anayehitajika Wakati Wote.
261
Mihango
Amri za mfalme au Mungu.
286
Balangila
Wana wa mfalme. Mmoja ni Mulangila.
302
Katikiro
Waziri Mkuu.
357
Anakomaga
Anatengeneza nguo za milumba.
Nyumanju
Nyuma ya nyumba.
361
Mbugu
Milumba, nguo za magamba ya miti.
371
Kukama
Kukamua.
520
Zinajipogoa
Vichane vya ndizi vinakongoloka vyenyewe.
526
Saza
(Kiganda) Jimbo.
529
Mbito
Wa Ukoo wa Babito. Watawala wa ufalme wa Bunyoro na Kiziba.
543
Mtelele
Tambarare.
597
Nsi
Nchi kavu.
602
Wanyamahanga
Wageni kutoka mbali.
621
Kuyu (nkuyu)
Aina ya samaki wa ziwani.
658
Maka
Kaya.
664
Kikaleni
Katika Kikale, yaani Ikulu.
683
Nyamuhanga
Mungu - Jua.
712
Mihi
Vifaa vya ukili vya kubebea senene wakisha kamatwa. Kimoja ni muhi.
713
Topito
Manati.
732
Watote
Walowe.
798
Kukukuza
Kukuua hutumika kwa mfalme tu.
855
Kutukinda
Kutuchinja, kutuua.
Maneno magumu au matumizi magumu ya maneno
Ubeti
Neno
Maelezo
0
Fasilu
Sehemu, sura.
1
Hisitoria
Historia.
3
Wahenga
Wazee wa kale, watangulizi.
6
Wavyele
Wazazi.
7
Pasina
Pasipo.
Jadi
Asili ya mtu.
8
Ufalume
Ufalme.
9
Elufu
Elfu.
10
Walisakini
Walikaa, waliishi.
12
Wali
Walikuwa.
Miungu
Mizimu.
Mizimu
Pepo za watu waliokwisha kufa.
Mahoka
Pepo za watu waliokwisha kufa.
15
Waafirika
Waafrika.

Kwangamia
Kuangamia.
16
Kuzimuni
Makao ya wafu au mizimu.
Auni
Misaada.
19
Hako
Hayuko.
22
Kwelezawe
Kueleza wake.
23
Umbile
Vilivyoumbwa.
24
Malikia
Malkia.
25
Tufani
Upepo unaovuma kwa nguvu sana.
26
Kuzawana
Kuzaliwa pamoja naye.
30
Ali
Alikuwa.
31
Anafurusha
Anarusha.
34
Mtetemo
Tetemeko la ardhi.
36
Aridhi
Ardhi.
41
Mahiri
Bingwa, mjuzi.
Chuku
Udanganyifu, ulaghai.
42
Humpiku
Humshindi.
44
Walihimidiwa
Waliabudiwa.
45
Ezi
Enzi.
46
Kutongoa
Kuimba, kusimulia.
Kunga
Siri za utunzi.
Mahadhi ya halua
Sauti tamu ya wimbo.
47
Kuhadithi
Kuhadithia.
Uhabithi
Uovu, ubaya.
50
Matetano mzomzo
Magomvi tele.
52
Kasheshe
Fujo, vurugu.
53
Waume wa miraba
Wanaume wakubwa, wenye nguvu.
54
Kuwanda
Kuwa na neema, kustawi.
Kutanda
Kuenea, kuzagaa.
Murua
Nzuri sana.
55
Sulutani
Sultani, mfalme.
56
Kumaizi
Kufahamu.
57
Uzinzani
Uzinza, nchi ya Wazinza.
58
Maliki
Mfalme.
Miliki
Utawala, ufalme.
59
Wadhifa
Cheo.
63
Yali
Ilikiwa.
64
Masogora
Mafundi wa kuwamba ngoma.
66
Tambo
Wakubwa.
Kiambo
Kitongoji, makazi.
68
Ziwa lahema
Ziwa lapandisha nakushusha mawimbi yake.
Kaskazi
Kaskazini.
70
Kufuma
Kutoboa kitu.
Husuma
Chuki.
Hujuma
Shambulizi, uharibifu.
72
Ngwamba
Kazi ngumu.
74
Mzito mja
Mjamzito.
76
Nadhifu
Mzuri, anayevutia.
78
Yakerereze
Yapigekwa msisitizo.
80
Zikatangaa
Zikaenea.
81
Pukupuku
Kwa wingi.
82
Aso makamu
Asiye na umri mkubwa.
84
Kwa tuwatuwa
Kwa kusitasita.
85
Akikita batobato
Akibamiza miguu kama bata.
87
Linayumkini
Linafaa, linastahili.
88
Janga
Maafa.
90
Afia
Afya.
Waa
Doa, dosari.
Asiyechelea
Asiyeogopa.
91
Ahodhi
Amiliki.
92
Zisilitindike
Zisipungue.
95
Myezi
Miezi.
102
Labuda
Labda.
104
Hadhari
Uangalifu.
Liso
Lisilo.
Dhila
Dhara, ubaya.
105
Wakanipalia
Wakinipa.
109
Katu
Kamwe, hata kidogo.
112
Kuzikoroga kwato
Kuja haraka haraka.
114
Mahiri
Hodari, mwenye ujuzi.
115
Hakuita
Nimekuita.
116
Kabula
Kabla
117
Kuikidhi
Kuitimiza.
120
Dhidi
Kupinga.
122
Mtokoto
Mkali, unaotokota.
125
Thawabu
Ahsante, shukrani, zawadi.
128
Tasihili
Kwa haraka.
Tunguri
Vibuyu vidogo vya uganga.
Kili
Ukindu.
131
Kasabahi
Kaamukia, katoa salamu ya asubuhi.
Afua
Uzima, uponaji.
132
Kanagiza
Kaniagizia.
Kuzinuizia
Kuzisalia, kuzisemea maneno ya uganga.
134
Yabisi
Ngumu.
135
Panyiza
Fanya.
137
Kishapo
Kisha hapo.
138
Makeke
Machachari, hekaheka, fujo.
141
Kudhalilisha
Kupunguza nguvu au hadhi.
142
Kutobanga
Kuvuruga.
144
Iso kifano
Isiyo kifani.
146
Kafanza
Kafanyiza, katengeneza.
148
Kutangaa
Kutajika kila mahali, kuzagaa.
149
Sudi
Bahati njema.
150
Kamuengeza
Kambembeleza.
151
Kajipangusha
Kajipangusa.
155
Mikiki
Tendo la kutumia nguvu.
157
Hayajangia
Hayajaingia, hayajaota.
160
Laana
Balaa inayotokana na kukosa radhiya Mungu.
Kitwana
Mtumishi wa kiume aliye kama nusu mtumwa.
Kwambua
Kuambulia; kukutwa najambo.
162
Kwangamia
Kuangamia.
163
Ulozi
Uchawi.
164
Kafi
Kasia la kuendeshea mtumbwi; Mugasha ni Muungu wa ziwa, hivyo inasemekana huonekana akitembea huku ameshika kasia.
Ghafi kanda
Mabaya, maovu, kenea.
Kuwanda
Kuwa nene.
166
Debe shinda
Debe tupu.
Panda
Parapanda, baragumu.
167
Baa
Balaa
168
Kasirini
Ikuluni.
170
Fadhaa
Mshtuko.
171
Kukongolewa
Kuopolewa, kukatwakatwa.
Kengewa
Aina ya mwewe.
172
Kulalama
Kulaani.
175
Harara
Mbio, haraka.
Ghera
Hamu, nia.
176
Ada
Desturi.
Jamala
Fadhila, wema.
177
Malika
Maliki, mfalme.
180
Nafusi
Nafsi.
183
Shari
Rabsha, vurugu.
Watakasiri
Watakasirika.

Wataihasiri
Wataiharibu.
184
Wajihi
Uso, sura.
Hutumika wakad wa kuzungumzia mfalme, mathalan kufika wajihi ni kufika mbele ya mfalme.
185
Pulikeni
Sikilizeni.
187
Naugulia
Nalilia.
Ulezi
Kulea.
Vijaluba
Vifuko.
188
Macho yanasinasina
Machozi yataka kutoka.
Wakajiondokelea
Wakaondoka.
191
Kungia
Kuingia.
194
Tunutu
Mtoto wa nyuki.
196
Huba
Hamu.
199
Ajizi
Usiri, ugumu wa kufanyajambo.
202
Midhana
Balaa.
204
Mwanondolea
Mwaniondolea.
206
Utuvu
Utulivu.
207
Kakata
Kwa mikiki.
Aguta
Anahema.
213
Wakamgura
Wakamuacha.
214
Msito
Kusita, kupumzika.
218
Magharibi
Jioni.
Amekwajuka
Amechakaa.
219
Gharighari la mauti
Karibu na kukata roho.
Siti
Mwanamke.
221
Mtima
Moyo, nadhiri au fikra ya ndani.
222
Tumai
Tumaini.
224
Wampapia
Unapiga.
227
Asikari
Askari.
228
Chepechepe
Dhaifu.
230
Azima
Kusudio, dhamira, nia.
233
Msasi
Mwindaji.
Podo
Kifuko cha kubebea mishale.
237
Nasabaye
Ukoo wake.
239
Karine
Kame.
241
Heba
Haiba, heshima na utukufu.
242
Wororo
Hali ya kuwa laini.
Mbaro
Kifungo.
244
Mziwanda
Kitmdamimba, mtoto wa mwisho.
246
Kakara
Kukurukakara, mapambano.
247
Alihozi
Alihodhi, alimiliki.
249
Iitilwe
Inaitwa.
Iwambilwe
Imewambwa.
251
Goma
Ngoma kubwa.
253
Wakifu
Takatifu.
257
Mtunzi
Mtunzaji.
258
Masikiyo
Masikio.
260
Majilisi
Baraza.
Wasiasi
Hawakuasi, walitii.
265
Inavyosinyaa
Inavyonyong'onyea, inavyopungua.
267
Mtanza
Mtaanza.
Kuteta
Kuzozana, kugombana.
272
Ukakasi
Kutumia nguvu, kulazimisha jambo.
276
Msasa
Laini.
277
Kumusia
Kumuusia.
279
Kamwagizila
Kamwagizia.
289
Lukuki
Wengisana.
292
Akahaha
Akahangaika.
Asiridhi
Asiridhike.
294
Wenzo
Wenzio.
297
Budi sina
Sina budi.
298
Tasihili
Haraka.
300
Jamala
Fadhila, matendo mazuri.
304
Tukiamiri
Tukiongoza.
306
Masurufu
Chakula cha safari.
309
Kuwajuza
Kuwapa habari, kuwafahamisha.
312
Dazani
Kumi na mbili.
Kani
Nguvu.
313
Pamwe
Pamoja.
314
Kiza kiliposhitadi
Kiza kiliposhtadi, giza lilipokoza, liliposhika sana.
315
Nyatunyatu
Kunyaria.
316
Milumba
Mbugu, nguo za magamba ya miti.
320
Nguu
Milima.
321
Ngisi
Aina ya samaki mweupe.
323
Pamba
Chakula cha safari.
325
Udhia
Tabu, usumbufu.
326
Ikawakeketa
Ikawauma.
327
Wanazivinjari
Wanazitembelea, wanazizunguka.
331
Jikusuru
Jihimu, jitahidi.
332
Kabarizi
Kazungumza.
Uchizi
Utukutu, upuuzi.
333
Kujinusuru
Kujiponya.
334
Itajulika
Itajulikana.
335
Litangia
Litaingia.
338
Konde
Shamba.
339
Wakona
Wakaona.
Azizi
Zuri.
345
Woto
Uoto, mazao.
347
Limemuumuka
Limemvimba.
348
Kudhukuru
Kueleza, kusema.
Mashukuru
Shukrani.
350
Garasha
Kitu cha ovyo kisicho na thamani.
352
Futa
Vuta.
353
Kitala
Vita.
361
Kitanga
Chombo cha udongo.
365
Iliyowasakamia
Diyowaandama.
369
Maridhawa
Vingi.
372
Usasini
Katika uwindaji.
375
Ndumba
Hirizi.
378
Walikozukia
Walipotokea.
383
Nyayu
Nyau, paka.
Halitaka
Hali takataka, hali uchafu.
386
Amiri
Mkuu, kiongozi
388
Sichi
Sichelei, siogopi.
390
Ghaidi
Jambazi.
398
Janadume
Kijana mkakamavu.
Mana
Maana.
399
Ukibalehe
Ukikomaa.
404
Kuutiringa
Kuurusha kasi.
Kumtindanga
Kumchinja.
405
Ugwe
Kamba ya upinde.
407
Tambo litajitambua
Fumbo litajifumbua.
408
Wakakirihi
Wakakinai.
410
Hari
Joto.
416
Walipojia
Walipokula chakula cha jioni.
419
Wakenda
Wakaenda.
420
Kamkabizi
Kamkabidhi.
421
Katukatu
Hata kidogo.
422
Miadini
Mahali pa kukutana.
425
Wahedi
Wa kwanza.
434
Wakamba
Wakasema.
Wa chaleni
Wa chanjo.
437
Tangua
Vunja.
440
Wakajizatiti
Wakajiandaa.
443
Suhubia
Fanyiana urafiki.
450
Nadhari
Uangalifu.
Kuzisasi
Kuzipeleleza.
452
Tamthili
Mfano wa.
453
Nyatunyatu
Tahadhari, nyatia.
Matumatu
Ghafla.
459
Akajitoma
Akajirusha.
462
Nduli
Dude, mnyama mkali.
Kibahaululi
Kijitu, kiumbe duni.
468
Bwabwa
Sauti za mbwa.
469
Rabusha
Rabsha.
470
Ananyapa
Ananyatia.
473
Usipombeze
Usitingishe.
476
Wakabwagika
Wakaanguka chini kama mzigo.
477
Yakangia
Yakaingia.
480
Lege
Legelege, mlegevu, dhaifu.
487
Nderemo
Vifijo, furaha kubwa.
489
Ahueni
Nafuu.
492
Ng'ombemwitu
Mbogo, nyati.
496
Tuu
Tu.
498
Halahala
Haraka haraka.
503
Anadhukuru
Anakumbuka.
508
Furifuri
Kwa wingi.
521
Kufura
Kufurika.
524
Nikakamke
Niwe mkakamavu.
532
Kuikita
Kuisimamisha.
535
Sahiba
Rafiki mkubwa.
537
Kaumu
Umma wa watu.
549
Nadhiri
Ahadi.
560
Twishi
Tuishi.
566
Majikalifu
Bila kutaka.
575
Miba
Miiba.
576
Alifajiri
Alfajiri.
584
Kuiegeza
Kuigesha.
586
Kuziratibu
Kuzishika (zamu).
587
Jia kijio
Kula chakula cha jioni.
Malalio
Virago vya kulalia.
589
Ja
Karpa.
Wameipambaja
Wameikumbatia.
592
Wakaishua
Wakaitia, wakaiteremsha.
595
Kafara
Sadakakwa Mizimu.
596
Kusi
Kusini.
599
Uliokoza
Wenye mwanga mkali.
622
Subalherini
Salimio la asubuhi.
624
Halahala
Himahima haraka.
627
Kwelemea
Kwenda, kuelekea.
634
Jalali
Mtukufu.
Fadhili
Hisani, msaada.
638
Kongoni
Aina ya mnyama kama nyumbu.
Kuro
Mnyama wa porini afananaye na ndama.
644
Fadhilazo
Hisani yako, msaada wako.

Mwadhamu
Mtukufu.

Masitakimu
Maslakimu, makazi.
651
Kuiauni
Kuilinda, kuitetea.
656
Wapepezi
Watu wanaowapepea watawala kwa vipepeo ili wasisumbuliwe na joto au wadudu warukao.
Wakanzi
Wakandaji.
660
Kukera
Kusumbua.
669
Nyang'au
Nduli, madude.
670
Nemsi
Ustawi.
682
Dia
Malipo mema, fidia.
690
Shahamu
Mafuta.
Dawamu
Bila kukoma, milele.
691
Mizungu
Maajabu.
693
Bahau
Mpumbavu.
694
Gomashinda
Gomatupu.
704
Saburi
Subira.
708
Wafane
Waliofana, wema, wazuri.
714
Hirimu
Kundi la umri fulani.
Rika
Watu wa uniri fulani.
716
Mifuo
Mitaro iliyochimbwa na maji.
717
Ukufi
Kitu kidogo.
719
Wakajitoma sharini
Wakajitosa katika pilikapilika.
720
Vitimbi
Hila, ujanja.
728
Hio
Hiyo.
733
Janga
Balaa, maafa.
735
Kauri
Chombo cha udongo.
740
Kawashua
Kawadharau, kuwashushia hadhi.
742
Amali
Matendo.
743
Ikacharuka
Ikalipuka.
746
Nti
Nchi, ardhi.
747
Kutowelea
Kufanya kitoweo.
752
Ikaputa
Ikavimba kama puto.
754
Furusa
Fursa, nafasi.
763
Kaumu
Umma wa watu.
764
Walitafakari
Waliwaza kwa makini.
768
Harara
Haraka.
772
Ziwazingile
Ziliwazunguka.
773
Juku
Jukumu.
776
Wasioneke
Wasionekane.
782
Ametarama
Amestarehe.
783
Vikuku
Mabangili,
785
Bwabwaja
Porojo.
788
Adhamu
Hadhi, heshima.
789
Maajuza
Wakongwe.
791
Kujalisi
Kuongea, kujadiliana.
795
Dubwana
Dude, nduli.
Hiana
Uhaini, uadui.
798
Kukuambua
Kukunyanganya.
803
Ndwele
Maradhs, ugonjwa.
804
Mtufala
Mtu duni, mjinga.
805
Nadhari
Akili, uangalifu.
808
Maki
Kina.
825
Havaa
Nilivaa.
828
Nimekufuru
Nimetenda mambo yenye kuwachukiza Miungu.
829
Kujisoza
Kujiumiza.
834
Dhalimu
Anayedhulumu.
835
Aliyoiatamia
Aliyoimilild.
850
Nyumao
Nyuma yao.
853
Dhuluma
Uonevu.
856
Misu
Majisu makubwa.
859
Madhila
Maafa.
862
Bimbirishana
Angushana.
873
Sahibu
Rafiki.

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?