H.J.M. Mwansoko
DAR ES SALAAM UNIVERSITY PRESS
DAR ES SALAAM
Dar es Salaam University Press
S.L.P. 35182
Dar es Salaam
© H.J.M. Mwansoko
Chapa ya Kwanza, 1991
ISBN 9976 60 161 1
Haki zote zinaehifadhiwa. Hairuhusiwi kuigiza, kunakili au kukitoa kwa njia yoyote ile bila idhini kwa maandishi ya Dar es Salaam University Press.Sura ya 1: Elunumitindo na mitindo
@masshele
Elimumitindo
Kabla hatujaeleza fasiri au maana ya elimumitindo ni muhimu kuanza kueleza taaluma hii inashughulikia nini. Jaribio dogo lifuatalo huenda litasaidia: Tuseme kwa mfano inatolewa tathmini ya maendeleo ya kazi ya mchunguzi (mtafiti) mmojawapo wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili katika mazingira mawili tofauti. Katika mazingira ya kwanza (1) tathmini htyo inatolewa na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo mbele ya Kamati ya Tathmini za wanataaluma na katika mazingira ya pili (2) tathmini hiyohiyo inatolewa na marafiki wawili wa mchunguzi huyo katika mazungumzo yao yasiyo rasmi, yaani maongezi ya kawaida ya kila siku yasiyotawaliwa na kanuni zozote maalum. Maelezo ya tathmini hiyo yanaweza kufanana na haya:
(1) Maendeleo ya utendaji kazi wa Ndugu X kwa kipindi cha mwaka uliopita yalikuwa mazuri sana. Ndugu huyo ameonyesha utanisi mkubwa wa kazi katika shughuli zake zote za kila siku, katika makala alizotoa na katika kushiriki kwenye majadiliano mbalimbali ya kitaaluma Taasisini na nje ya Taasisi (... n.k.).
(2) Unajua Ustadhi! Inaelekea Shekhe X ameamua kuisakama vikali taaluma mwaka huu. Kazi yake kwa ujumla si haba. Hata makala zake pamoja na machachari yake kwenye vikao vya wasomi yanasisimua ile ngumu (... n.k.)
Ulinganisho wa maelezo haya unatuonyesha kwamba kimsingimaudhui ya taarifa hizi yameHngana kabisa: kwamba kazi ya Ndugu X kwa mwaka uliopita ilikuwa nzun na ya kuridhisha katika vipengele vyake vyote. Lakini maelezo haya yanatofautiana katika matumizi yake ya zana za kiisimu, yaani msamiati na mpangilio wake katika sentensi Na utumiaji huu wa zana totauti za kiisimu wakati maudhui ya maelezo yanahaki yamelingana ndizo tunaziita totauti za kimtindo (zinazoletwa na mitindo mbalimbali ya lugha).
Kwa hali hii jaribio dogo la hapo juu limetuonyesha kwaipba kwa kutumia mada hiyomyo moja tunaweza kutoa maelezo yanayokaribiana sana kimaudhui lakini yakava yametofautiana kabisa katika zana za kiisimu yanazozitumia.
Swali linajitokeza: kwa nini watumiaji wa lugha wanalazimika (kwa kiwango fulani) kutumia zana mbalimbali za kiismu katika mawasiliano yao? Au kwa maneno mengine, inakuwaje zana mbalimbali za kiismu zijitokeze kwa mada moja katika mazingira yanayotofautiana na kwa watumiaji mbalimbali wa lugha moja?
Kuna sababu kadha wa kadha, kubwa kati ya sababu hizi ni hii ifuatayo. Kufuatana na utamaduni wa kila jamii, kwa wakati maalum, huwepo kawaida na taratibu fulani za zana za kiisimu zilizozoeleka na kujijenga kutokana na historia ndefu ya kukua kwa lugha hiyo ambazo kwazo hufanyika uchaguzi maalum wakati wa kuzitumia. Kwa kawaida uchaguzi wa zana hizo za kiisimu hutofautiana kufuatana hasa na mazingira mbalimbali ya utumiaji wa lugha.
Kulingana na maelezo haya Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ambaye tumemzungumzia hapo nyuma angeweza pia kuelezea tathmini ya kazi ya Ndugu X katika mazungumzo yake na ndugu pamoja na marafiki zake nyumbani (m.f. mkewe, mama yake, kaka yake... n.k.), ingawa kufanya hivyo kutakuwa ni kukiuka taratibu za kazi, na bila shaka uchaguzi wake wa zana za kiisimu ungetofautiana na ule wa kuhutubia kikao rasmi cha tathmini za wanataaluma.
Aidha uchaguzi wa zana mbalimbali za kiisimu unawcza kufanyika kwa kutegemea mambo yafuatayo:
(1) Lengo la mzungumzaji au mwandishi. Uchaguzi wa zana za kiismu kwa mada ya “matatizo ya miradi ya kiuchumi” utatofautiana sana kufuatana na malengo ya taarifa zitakazotolewa: linganisha k.m. mhadhara kwenye somo la Uchumi (lengo hapa ni kuelimisha) na mchezo wa Pwagu na Pwaguzi wa Redio Tanzania Dar es Salaam (wenye lengo la kuchekesha na kufunza).
(2) Sifa za mziuigumzaji au mwandishi (elimu yake, umri wake, utamaduni wake, tabaka lake katika jamii, ladha zake - yaani mambo gani hasa anayapendelea, hali yake kisaikolojia - amechukia? amefurahi? mcheshi?.... n.k.)
(3) Sifa za mtu unayewasiliana naye (elimu yake, umri wake, ujuzi wake, hali yake kisaikolojia - amechukia? ana majonzi? ana furaha?, uhusiano wako kwake - ndugu yako? rafiki yako? kiongozi wako kazini?... n.k.).
(4) Mada ya mawasiliano. Bila shaka kutakuwepo na tofauti kubwa katika uchaguzi wa zana za kiisimu baina ya mada ya kitaaluma k.m. juu ya fonolojia na mabishano ya washabiki wa mpira wanapozungumzia ubingwa wa timu zao, mathalani za Yanga na Simba.
(5) Jinsi mawasiliano yanavyotekelezwa - kwa mazungumzo au kwa maandishi. Inaeleweka na wengi wetu, kwa mfano, kuwa mawasiliano kwa mazungumzo yanaruhusu kutumia sentensi za mkato pamoja na ishara mbalimbali (k.v. kutikisa kichwa, kukonyeza, kupiga mluzi... n.k.) ambapo maumbo ya sentensi katika maandishi kwa kawaida si ya mkatomkato, bali yana taratibu zake maalum.
Baada ya kuonyesha jinsi maelezo mbalimbali yanavyoweza kutofautiana kutokana na zana za kiisimu zilizotumika, ingefaa sasa tujibu swali jingine muhimu: Je, tofauti hizi za zana za kiismu zinaletwa na nini hasa? Yaani ni mbinu gani za kiisimu zinazotumiwa ili kuonyesha tofauti hizi za zana za kiismu (ambazo kwa maneno mengine tunaweza kuziita tofauti za kimtindo).
Kwanza kabisa tofauti za kimtindo zinaweza kuletwa na msamiatiunaotumika katika mawasiliano. Majina (nomino) mengi yanayotumiwa kwa mfano, katika nfitindo ya kitaaluma na ya kirasimu kwa kawaida huwa yana maana pana na za kidhahania ambazo kwa desturi hazionyeshi hisia za mzungumzaji au mwandishi. Tena kwenye mtindo wa kitaaluma aghalabu majina hayo huwa ni istilahi. Kwa mfano, maendeleo, siasa, mapinduzi, uundaji, fonolojia, uhandisi, nazali, utamaduni, mkurugenzi, idara, data, masijala, makala, katiba, kumbukumbu, marejeo... n.k. Lakini kwa upande mwingine vihisishi, yaani maneno yanayoonyesha mshangao kama vile: loo!, ah!, lahaula! au tasfida (mf. “kujisaidia” badala ya “kukojoa” ama “kunya”, “makalio” badala ya “matako”) au nahau (mf. “ana mikono mirefu” badala ya “mwizi”), au misimu (mf. “chauchau”/“chai” badala ya “rushwa”) na pia maneno yenye mguso mkubwa (maneno hisishi) kama vile “masumbwi”, “ndondi” au “makonde” badala ya “ngumi” hutumika zaidi katika mtindo wa mawasiliano yasiyo rasmi na pengine katika mtindo wa magazetini.
Mitindo inaweza kutofautishwa vilevilekiortografia na kifonetiki. Kwa mfano, kwenye mtindo wa magazetini inaruhusiwa kutumia maneno yaliyofupishwa k.m. “KK” badala ya Rais Keneth Kaunda wa Zambia, “Dar” badala ya Dar es Salaam, “Moro” badala ya Morogoro n.k. ikiwa ni njia mojawapo ya kubana matumizi ya karatasi magazetini na pengine kuwavutia wasomaji na kuonyesha mapenzi na umuhimu auonao mwandishi juu ya jambo analolieleza. Hali kama hii kwa upande mwingine, hatuwezi kuiona kwenye mtindo wa kitaaluma. Hapa ni lazima kuandika na kutamka maneno yote kikamilifu kama ilivyo katika kanuni na taratibu za kisarufi. Kwa hali hii kwenye shughuli za kitaaluma k.m. wakati wa kujibu maswali ya mtihani, haiwezekani kuandika (na hata kusema) kuwa mji mkuu wa Tanzania ni Dar., au Rais wa Zambia ni KK. Haya yatakuwa makosa makubwa kimtindo ingawa majibu yake ni sawa. Hali kadhalika lafudhi inayotumika katika kipindi cha redio cha “Pwagu na Pwaguzi” na ile ya kikundi cha porojo cha Redio Tanzania Dar es Salaam katika kipindi cha “Klabu Raha Leo Shoo” lazima itofautiane na ile itakayotumika na mwalimu akiwa darasani. Na tofauti hizi zitakuwa za kifonetiki.
Aidha sarufimaumbo nayo inaweza kutumika kuonyesha tofauti mbalimbali za kimtindo. Kipengele cha sarufimaumbo kinajumlisha wakati, umoja au wingi wa watendaji, nafsi, ngeli, mofimu n.k. Hebu tutumie umoja au wingi wa watendaji pamoja na nafsi kuonyesha jinsi sarufi maumbo inavyoweza kutofautisha mitindo. Uchunguzi wa wataalam wengi wa elimumitindo, kwa mfano, umeonyesha kwamba ili kuficha “ubinafsi” wa mwandishi aghalabu tunatumia wingi wa watendaji na nafsi ya kwanza katika mtindo wa kitaaluma. Pengine hutumika (umoja wa mtendaji katika) nafsi ya tatu. Kwa mfano hatupendelei sana kusema:
- kutokana na jaribio nililolifanya...
- katika makala haya nimejaribukueleza...

Mashele blog
Badala yake tunasema: kutokana na uchunguzi tulioufanya... (hata kama mchunguzi ni mmoja tu), Wingi wa watendaji na nafsi ya kwanza katika wingi unaondoa ubinafsi na upendeleo wa mwandishi na kuifanya taarifa ionekane kuwa ni ya kweli na uhakika zaidi. Hali kadhalika umoja wa mtendaji katika nafsi ya tatu k.m. “mwandishi wa makala hii amejaribukuonyesha...” unatimiza lengo hili. Ubinafsi huu, kwa upande mwingine unakuwa ni jambo la kawaida kabisa kwenye mtindo wa mawasiliano yasiyo rasmi na ule wa shughuli za kisiasa. Kwa mfano, mara nyingi tunawasikia wabunge wakisema:
“Ndugu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Waziri mimi nina swali moja la nyongeza. Ningependakujua...”
“Ndugu Spika, ninamshauri Ndugu Naibu Waziri....” n.k.
Vilevile viambishi, vipashio na vijenzi hutumika kama vionyeshi vya mitindo tofauti. Kwa mfano, kiambishi “m-” (mchumi), kipashio “-a” (biolojia) na kijenzi “mwana-” (mwana-fonolojia) aghalabu huundaistilahi.
Tofauti za kimtindo zinaweza kuonyeshwa vilevile kwa sarufi miundo. Kwa mfano imedhihirika kwamba mara nyingi sentensi zinazotumika katika mtindo wa mawasiliano yasiyo rasmi ni za mkatomkato kwa sababu watu wanapozungumza ana kwa ana wanaweza kutumia ishara nyingine za nyongeza na, zaidi ya hapo, kwa kawaida jambo wanalolizungumzia huwa si geni (sana) kwao. Kwa upande mwingine sentensi za mkato si kawaida kutumika kwenye mtindo wa maelezo au maandishi ya shughuli za kitaaluma. Sentensi nyingi katika mtindo wa kitaaluma huwa kamilifu na zina kiima na prediketa.
Kutokana na yote tuliyoyajadili tunaweza kufanya mahitimisho yafuatayo:
1. kwamba elimumitindo inaambatana (inahusiana) na vipengele vyote vya muundo walugha
2. kwamba katika kutofautisha mitindo mbalimbali vipengele vyote vya isimu - yaani fonetiki, ortografia, sarufimaumbo, msamiati, miundo ya sentensi, n.k. hutumika.
Hii ina maana kwamba elimumitindo, kinyume na vipengele vingine vya taaluma ya lugha (kv. fonolojia, sarufimaumbo... n.k.) inahusisha nyanja zote za muundo wa lugha kwa pamoja. Katika elimumitindo tunajifunza uwezo wa lugha wa kuibua miguso mbalimbali na kanuni za utendaji kazi wa zana za kiisimu katika mazingira yanayotofautiana. Mtazamo wa utathmini kwa vipengele vya lugha ni sifa maalum ya elimumitindo. Elimumitindo inachagua - kutokana na fungu kubwa la zana na mbinu za kiisimu ni zana na mbinu zipi zitumike kufuatana na mazingira, mada, lengo/kusudi na njia za utekelezaji wa mawasiliano yanayohusika. Hususan elimumitindo ni taaluma inayotufundisha:
1. uwezo wa kuibua miguso wa zana na mbinu za kifonetiki, kimsamiati, kisarufimaumbo, kisarufi miundo;
2. zana zote za kiisimu kufiiatana na matumizi yake katika mazingira na malengo mbalimbali;
3. kanuni za utendaji kazi wa lugha katika mazingira mbalimbali ya mawasiliano;
4. mifumo mbalimbali ya zana za kiisimu kwa kufuatana na jinsi inavyotumiwa katika nyanja tofauti za shughuli za jamii.
Baada ya kupata madokezo haya machache kuhusu taaluma hii ya elununutindo na masuala inayoyashughulikia sasa tunaweza kutoa fasiri yake:
Elimumitindo ni taaluma ihusuyo lugha inayojifunza zana zote za kiisimu katika vipengele vyake vyote kwa kuangalia hasa kufaa na kukubaliwa kwake na wanajamii walio wengi wakati wanapozitumia kufuatana na malengo na mazingira ya mawasiliano. (taz. Turner, 1973:7 Krilova, 1979:17).
Ingawa neno “elimumitindo” limekuwa Ukitumika hapa na pale katika taaluma ya filolojia tangu zama za kale - tangu kame ya 18 na 19 - lakini taaluma yenyewe ya elunumitindo ilianza kujitokeza kwenye miaka ya 20 - 30 ya mwanzo wa karne ya 20. Uchunguzi mkubwa wa kipengele cha mitindo kufuatana na utendaji kazi wa lugha (functional styles) ambacho ni muhimu sana katika elimumitindo ulifanyika si muda mrefu uliopita, kwenye miaka ya 1950. Kwa hali hii ni dhahiri kwamba elimumitindo ni taaluma iliyo changa kabisa, na imejitokeza kama taaluma baada ya vipengele vingine vya lugha (k.m. fonolojia, sarufi maumbo,... n.k.) kufanyiwa utafiti wa kutosha na kujishamirisha kama taahuna kamili. Uchunguzi wa elimuniitindo, na hasa umuhimu wa mitindo unaambatana sana na matumizi ya lugha katika mawasiliano, yaani utendaji kazi wa lugha. Kusema kweli taaluma ya elimumitindo ni taaluma ya utendaji kazi wa lugha. Na huu ndio umekuwa mwelekeo wa uchunguzi mwingi wa taaluma ya lugha katika nchi nyingi za ulimwenguni katika karne yetu, yaani kuchunguza/kutafiti utumiaji wa lugha katika mawasiliano, na sio (tu) muundo (structure) wa lugha.
Kama tulivyosema, uchunguzi kamambe wa elimumitindo ulianza mwanzoni mwa kame tuliyo nayo. Skuli maarufu zilizojishughulisha sana na taaluma hii ni skuli ya Urusi (Boduene de Kurtene, I.A., Polivanova, E.D., Yakubinski, L.P., Vinogradov, V.V., Vinokur, G.O. n.k.) na ile ya Chekoslovakia. Vilevile kuna wanaisimu kadha wa Ulaya Magharibi wanaolishughulikia vya kutosha suala hili la elimumitindo (Enkvist, E.W., Hartmann, R.R.K., Tumer, G.... nk.).
Kumekuwa na mwitikio mkubwa kimataifa wa uchunguzi na upekuzi wa taaluma ya elimumitindo hasa baada ya nusu ya pili ya kame ya 20. Semina, warsha na makongamano, ya kimataifa juu somo hili yaliyokwishafanyika (New York - 1960, Warsaw - 1961, Moscow - 1961, 1969, Sofia - 1963, Prague - 1968, Bucharest - 1967) yanathibitisha kauli hii.
Mitindo
Dhana inayowakilishwa sasa na neno “mtindo” haikujitokeza wala kujengeka kwa ghafla tu. Dhana hii ina historia ndefu. Hapo zama za kale Wagiriki na Warumi waliuelewa mtindo kuwa ni balagha (rhetory), yaani utaalamu wa kutumia maneno mengi na yaliyo mazuri lakini yasiyo na maudhui makubwa. Mtindo ulichukuliwa kuwa ndio nyenzo au mbinu za kuwashawishi wasikilizaji wavutiwe, wasadiki na wayakubali yasemwayo na mzungumzaji. Kwa kifupi mtindo kwa Wagiriki na Warumi ulikuwa ni ufundi wa kusema.
Mtazamo huu una kasoro moja kubwa. Nayo ni kwamba unatuonyesha kuwa mzungumzaji alikuwa na uhuru wa kuzungumza apendavyo, yaani yeye ndiye aliyeitawala mitindo na sio kwamba mitindo ndiyo iliyomiazimisha kuzungumza kwa namna hiyo aliyofanya. Tena mtazamo huu ni finyu kwani unaihusisha mitindo na uzungumzaji tu.
Katika Uhindi ya kale mitindo ilichukuliwa kama mbinu za kupamba mazungumzo, kuyafanya yapendeze na yawe “matamu” sana yalifikiapo sikio. Hapa napo fasiri ya mtindo iriaonekana “imebanwabanwa” sana kwa sababu mtindo umehusishwa na upambaji tu wa lugha, tena sio katika hali zake zote, bali katika uzungumzaji tu.
Kwenye kame za kati (middle ages) mtindo uliambatishwa na tanzu za fasihi andishi na kulifanyika majaribio ya kulazimisha kuiona mitindo mbalimbali katika lugha kufuatana na tanzu zilizokuwepo wakati ule. Wakati huo istilahi “lugha ya maandiko”/“lugha ya vitabu” (literary language) ilichukuliwa kama kisawe cha istilahi “lugha ya fasihi”. Ni kutokana na hali hii ndio maana mitindo ya lugha ilihusishwa na tabia za lugha zilizokuwa zikijitokeza zaidi katika tanzu mbalimbali za fasihi.
Mmoja kati ya wafuasi wa mtazamo huu wa mitindo ni mwanataaluma wa zama za kale wa Kirusi Lomonosov, M.V. (1711 - 1765, yaani kame ya 18) aliyetofautisha mitindo mitatu na tanzu zinazoambatana na mitindo hiyo: (Krilova 1979:28)
1) “Mtindo wa juu” [kwa ajili ya kumbukizi (ode) - aina ya ushauri ambayo haisimulii hadithi, yenye urefu wa kiasi, dhamira moja, usanii wa hali ya juu na inayokusudiwa mtu, kitu au tukio maalumu; mashairi, tenzi na nyimbo za kishujaa; tanzia(tragedy); na hotuba kuhusu mada muhimu kitaifa k.m. dhifa za taifa, mazishi ya kiserikali, ulaji wa viapo... n.k.]
2) “Mtindo wa kati” [kwa ajili ya drama; bama za kirafiki zilizoandikwa katika ushairi, kejeli(satire); ushairi wa makiwa (elegy); na mashairi mafupi, yanayosimulia hasa habari za maisha ya shambani(idyll)].
3) “Mtindo wa chini” [kwa ajili ya futuhi (comedy); nyimbo za utani; barua za kawaida (zisizo za kishairi) za kirafiki; na maandiko yasiyo rasmi].
Mtazamo huu vile vile ni finyu kwani unaiambatisha mitindo na fasihi andishi tu.
Kunako mwanzoni mwa kame ya 20 wanaisimu mamboleo walieneza mtazamo wa mitindo kama tabia pekee za uzungumzaji wa kila mtu, kila mwanajainii. Kufuatana na mtazamo huu idadi ya mitindo katika lugha ni sawa na idadi ya watu katika jamii wanayoitumia lugha hiyo. Tatizo la mtazamo huu ni kwamba idadi ya mitindo inakuwa kubwa mno na inaweza kuendelea kukua kadiri idadi ya watu inavyoongezeka.
Wakati mwingine mitindo hueleweka kama kisawe cha njia za kutekeleza mawasiliano, kwa maandiko au kwa mazungumzo. Hivyo twapata, kwa mfano, “mtindo wa maandiko”, “mtindo wa mazungumzo”. Kulingana na fasiri hii patakuwepo na nutindo miwili tu katika lugha.
Pengine mitindo huchukuliwa kuwa ni kionyeshi cha vivuli mbalimbali vya miguso (emotions) na maono (feelings), kwa mfano maono ya furaha, huzuni, upendo, hasira... n.k. Kulingana na mtazamo huu twaweza kupata kwa mfano, “mtindo wa huzuni”, “mtindo wa kejeli”... n.k.
Njia hii pia inaruhusu kuwa na idadi kubwa (mno) ya mitindo kulugana na wingi wa miguso na maono hayo.
Pamoja na mitazamo hii ya mitindo na utofautishaji wa aina mbalimbali za mitindo kama tulivyokwisha onyesha kwa nutazamo na fasiri zaidi za nutindo angalia pia Enkvist na wengineo (1964) na Hartman (1981) ulikuwepo pia mtazamo wa mitindo kufuatana na utendaji kazi wa lugha, yaani matumizi ya lugha katika jamii. Mwelekeo huu wa kuiona mitindo kwa kulingana na matumizi ya lugha ulielekea kuleta mategemeo makubwa na yaliyo sahihi zaidi ya kupata ufumbuzi wa fasiri ya mitindo. Vidokezo vya mwelekeo huu ambavyo vilianza kutolewa tangu zama za kale (k.m. na mseniaji mashuhuri Cicero) na kuendelezwa zaidi na wanaisimu wa kame ya 19 (hasa Wilhelm Humboldt) ulipata msukumo mkubwa wa kuchunguzwa katika kame yetu ya 20.
Wanaisimu mashuhuri waliojishughulisha na uchambuzi wa mitindo kufuatana na utendaji kazi wa lugha ni wale wa skuli ya Urusi na ya Chekoslovakia, akina: Pishkovskii, A.M., Sherba, L.V., Vinokur, G.O., Kozhina, M.N., Krilova, O.A. na wengineo. Mtazamo huu unaungwa mkono pia na mwandishi wa kitabu hiki.
Katika kufasiri mitindo na kuigawa mitindo hiyo katika makundi mbalimbali kwa kufuata mtazamo huu ni lazima kwanza kuyatilia maanani mazingira ya utendaji kazi wa lugha, ambayo ndiyo yanayoashiria mitindo katika lugha. Na hii ina maana kwamba kunahaja ya kuziangalia zile sababu zinazoathiri maumbo ya maneno katika mawasiliano na uchaguzi wa zana za kiisimu zitakazotumiwa na mwandishi au mzungumzaji. Sababu hizi hugawanyika katika mafungu mawili makubwa.:
1. sababu dhahania (subjective factors)
2. sababu yakini (objective factors)
Baadhi ya sababu dhahania ni:
1. hali za kiuchumi na kijamii za washiriki wa mawasiliano (kazi zao, elimu yao, tabaka lao katika jamii... n.k.)
2. hali ya kisaikolojia ya wawasilianao (k.m. tabia zao)
3. jinsi mtu anavyojisikia (mood)wakati wa mawasiliano (mwenye furaha? huzuni? majonzi? wasiwasi?)
4. rika (umri) la washiriki katika mawasiliano.
Ni kweli kabisa kwamba namna ya uzungumzaji wa mtu akiwa katika hali ya mshituko wa furaha huwa ya maneno mengi yenye maumbo yanayoonyesha furaha hiyo, ambapo katika hali ya kawaida kabisa maneno na maumbo haya hayawezi kujitokeza. Hali kadhalika hali ya kisaikolojia (mf. tabia), kiwango cha maendeleo ya kiutamaduni na kielimu cha mtu... n.k. huathiri kwa hali fulani namna ya uzungumzaji (na uandishi) wake.
Lakini sifa hizi haziwezi kuathiri ujenzi na ujipambanushaji wa mitindo ya lugha. Zinachoweza kufanya ni kuathiri tu uzungumzaji wa mtu. Mitindo ya lugha haijengwi na sifa dhahania, bali huletwa na sifa/sababu yakini, ambazo ni pamoja na:
1. njia za kutekeleza mawasiliano (kwa maandiko au kwa mazungumzo);
2. aina/namna ya mazungumzo [mazungumzo ya mtu mmoja akisema pekee (monologue); mazungumzo ya watu wawili(dialogue); mazungumzo ya watu wengi (polilogue)];
3. nyenzo za mawasiliano (za umma k.m. redio, magazeti, vitabu, simu, n.k. au za kibinafisi k.v. barua ya mtu binafsi);
4. tanzu (genre) ya mawasiliano (hotuba mkutanoni, kushiriki katika semina/mjadala, barua, tangazo, hati ya mkataba... n.k.);
5. kazi au shughuli muhimu za jamii.
Hebu sasa tuangalie jinsi sifa hizi yakini zinavyoathiri uundaji wa nutindo katika lugha. Moja ya sifa hizi ni ile ya njia za utekelezaji wa mawasiliano. Ni dhahiri kabisa kwamba uchaguzi wa zana za kiisimu kwa ajili ya mawasiliano ya kimaandiko uhatofautiana sana na ule wa mawasiliano kwa njia ya kuzungumza. Na tena utofautiano huo wa maumbo ya maneno haujitokezi kutokana na matakwa ya mwandishi au sifa fulani maalum za mwandishi huyo, bali unatokana na mahitaji maalum ya kiisimu ambayo ni lazima yajitokeze katika mawasiliano ya kimaandiko.
Ukweli umeonyesha kwamba wakati wowote tuandikapo kitu chochote kama barua za kirafiki, barua za kiofisi au makala kwa ajili ya majarida ya kitaaluma... n.k. hujikuta tunalazimika kufikiria zaidi juu ya sura au miundo ya sentensi tutakazoziandika, mpangilio wake wa maneno utakavyokuwa n.k.... kuliko tnambo yanavyokuwa katika mawasiliano ya kuzungumza. Kwa kifupi, wakati wowote mtu anapotarajia kuandika, lazima kujitokeza “hali fulani ya kujitayarisha” ili kupanga mawazo, maneno na miundo ya sentensi. Kwa upande mwingine mambo haya hayatiliwi maanani au mkazo sana wakati wa kuzungumza. Na hii inaeieweka: mazungumzo yanaruhusu utumiaji wa mbinu nyingi zisizo za kiisimu (m.f. mazingira, kutoa ishara mbalimbali kwa kutumia viungo vya mwilini k.v. vidole, macho n.k., kiimbo) katika kuyafanya mawasiliano yaeleweke, wakati ambapo mawasiliano kwa maandiko hayana nafasi hii. Mawasiliano kwa maandiko yanahitaji mpangilio maalum wa maneno ambao ndio unaweza kubashiri intonesheni itakavyokuwa. Tena uandikapo lazima utilie maanani uwezo wa unayemwandikia wa kuuelewa muundo wa sentensi zako, ama sivyo lengo lako la mawasiliano linaweza lisieleweke vizuri na yule unayewasiliana naye.
Nyenzo za mawasiliano vilevile humlazimisha mtu “kurekebisha” ipasavyo maandiko au nzungumzaji wake. Kwa mfano, mtu (mzima) akikaribishwa kuzungumza kwenye redio uzungumzaji wake utatofautiana kwa hali fulani na jinsi anavyoongea k.m. na familia yake nyumbani. Na “kujirekebisha” huku hakutegemei umri wala tabia ya mtu, bali kunaletwa na urasmi wa chombo hicho na labda pia uzito na umuhimu wa mambo yanayojadiliwa.
Sifa nyingine yakini ni tanzu za mawasiliano na namna ya mazungumzo. Ni ukweli ulio bayana kabisa kwamba bila kutegemea hali ya kisaikolojia au jinsi mtu anavyojisikia au rika lake uandishi wake wa makala ya kitaaluma utatofautiana na ule wa barua ya kibinafsi. Ndio maana mtindo wa makala ya kitaaluma yanayotolewa, kwa mfano, katika semina za Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili na wataalam mbalimbali una hali fulani ya ufanano licha ya kwamba wataalam hao wanatofautiana (sana) katika rika, elimu, tabia zao na kadhalika. Hali kadhalika mazungumzo ya mtu mmoja (k.m. hotuba mkutanoni au mhadhara darasani) bila shaka yatatofautiana na mazungumzo ya watu wawili au wengi zaidi juu ya mada hiyohiyo. Katika kuzungumza watu wengi lazima kutajitokeza kufupisha/kukatisha kwa sentensi, kurudiarudia mambo na sifa nyinginezo za mazungumzo ya hali hii.
Sasa tuangalie jinsi sifa, kazi au shughuli muhimu za jamii, inavyoathiri ujenzi wa mitindo kwa kutumia mfano ufuatao:
Iwapo shughuli yajamii itahusu mambo ya kitaaluma au kisayansi, basi mawasiliano katika shughuli hii yatahitaji kueleza mambo kama yalivyo, kwa kweli tupu bila kuonyesha upendeleo wa wazi au maono ya wawasilianao. Na ili kukidhi haja hii itabidi zichaguliwe oa kutumika zile zana za kiisimu ambazo hazionyeshi upendeleo na maono ya mwandishi au mzungumzaji. Yaani kwenye shughuli za kisayansi kunahitajika utumizi wa lugha bayana (referential language), lugha inayotoa sifa na maelezo yaliyo halisi na ya waziwazi. Kwa mfano, mhadhara darasani juu ya matatizo ya ulevi hauwezi kubadilishwa kichwa cha habari na kutumia nahau - matatizo ya kuvaa miwani kwa sababu nahau hailengi kweoye dhana inayokusudiwa mara moja, ina utata katika kuielewa. Hapa tunataka lugha iliyo bayana na wazi kabisa.
Kwa upande mwingine hali ya uchaguzi wa zana za kiisimu inabadilika kabisa iwapo mawasiliano yanahusu shnghuli za kisiasa. Tuangalie kwa mfano mwanasiasa mashuhuri anapohutubia mkutano. Hapa itambidi atumie lugha ya kuvutia sana na iliyopambwa vizuri kwa nahau, methali, mafumbo, misimu, maelezo kwa kutumia mifano na ulinganisho mbalimbali, tasfida, sitiari... n.k. ili kuwafanya wasikilizaji wavutiwe na waifurahie hotuba na kuisikiliza kwa makini. Isitpshe lazima mhutubiaji aonyeshe maono na msimamo wake kuhusu jambo analolizungumzia, upande anaouunga mkono na kujaribu kadiri awezavyo kuwavutia wasikilizaji upande wake. Kwa hali hii uchaguzi wa msamiati na mpangilio wa maneno katika sentensi utatakiwa ukidhi haja zilizoorodheshwa hapo juu. Hii ina maana kwamba mfumo wa “muni” (ingawa “muni” hiyo inaweza kuwa kwa niaba ya kundi fulani la watu au chama) unatumika sana katika shughuli za kisiasa. Rejea, kwa mfano, hotuba zinazotolewa na wagombea viti vya ubunge wakati wa kampeni za uchaguzi. Wanasiasa wengi hntumia mtindo huu, k.m.
Wananchi! kama mtanichaguamimi, basi nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu kuyatatua matatizo yetu. Shida zetu nazijua kwani nami ni mkazi wa wilaya hii...
Sasa ingefaa tuzitaje kazi au shughuli muhimu za jamii. Kusema kweli shughuH za jamii zinaweza kuwa nyingi sana, laldni wataalam weagi wa elimumitindo (k.m. Kozhina 1977:37, Krilova 1979:36) wamejaribu kuziunganisha shughuli hm katika mafungu matano makubwa:
1. taaluma/sayansi,
2. sheria na utawala,
3. shughuli za kijamii na kisiasa(social and political activities),
4. sanaa na fasihi,
5. shughuli (za nyumbani) za kawaida za kila siku.
Kuna swali moja muhimu linalojitokeza hapa. Je, ni sifa gani kati ya zile zilizo yakini ambayo tunaweza kusema ni muhimu knzidi nyingine zote katika ujenzi wa mitindo? Jibu la swali hili lina umuhunu mkubwa sana kwani litatusaidia kujua idadi ya initindo katika lugha.
Iwapo tutasema kuwa njia za utekelezaji wa mawasiliano ndiyo sifa iliyo muhimu zaidi, basi itabidi tukubali kwamba katika lugha idadi ya mitindo iko sawa na idadi ya njia za kutekeleza mawasiliano - yaani mlrili: “mtindo wa maandiko” na “mtindo wa mazungnmzo”. Kama namna ya mazungumzo tutaichukulia kuwa sifa yenye uzito zaidi kuliko sifa yakini nyinginezo na kwamba sifa hii ndio inayojenga mitindo, basi tutakuwa na mitindo mitatu na sio miwili na itakuwa tofauti kabisa na ile miwili ya mwanzo. Yaani tutapata “mtindo wa mazungumzo ya mtu nunoja”, “mtindo wa mazungumzo ya watu, wawili” na “mdndo wa mazungumzo ya watu wengi”.
Hivyo ili kuipata mitindo iliyomo katika lugha sharti tupate uamuzi juu ya sifa iliyo muhimu zaidi inayoathiri ujena wa nutindo hiyo. Sifa hiyo, kwa kulingana na maoni ya wanamitindo wengi wa mtazamo wa mitindo kufuatana na utendaji wa lugha, ni kazi au shughuli za jamii.
Kusema kweli nutindo ni nufumo ya zana za kiisimu inayoambatana na kazi au shughuli muhiniu za jamii - kila mtindo ukiihudumia kazi au shughuli moja maalum ya jamii:
1. shughuli za kisayansi - mtindo wa mambo ya kitaaluma,
2. shughuli za kisheria na kiutawala - mtindo wa kirasimu,
3. shughuli za kijamii na kisiasa - mtindo wa magazetini na shughuli za kisiasa,
4. shughuli za kawaida za kila siku - mtmdo wa mawasiliano yasiyo rasmi.
Kama inavyoonekana sifa ya “kazi au shughuli za jamii” si sifa ya kiisimu. Lakini katika kuigawa na kuipambanusha mitindo mbalunbali ya lugha ni muhimu na yatubidi kutafuta sifa za kiisunu ili kukidhi haja hiyo. Hii ina maana kwamba kama kuna mtindo mmoja ambao unaihudumia kazi au shughuli moja maalum ya jamii, basi katika mtindo huo kutajitokeza namna fulani ya maneno, msamiati, miundo ya sentensi, hali fulani ya lafudhi... n.k. ambayo hujikita (hujishamirisha) na kuanza kutumika zaidi katika mtindo huo. Yaani kunatokea kitu kama “mihuri” fulani ya kiisimu ambayo ni lazima itumike zaidi katika mawasiliano yahusuyo kazi au shughuli husika ya janui. “Mihuri” hii itajikuta kuwa si mahala pake iwapo itatumika katika mawasiliano yahusuyo nyanja nyingine za kazi za jamii.
Kwa mfano, miundo ya sentensi nyingi zinazotumika katika mtindo wa mawasiliano yasiyo rasmi ni ya mikato (yaani inaruhusu kukatiza sentensi) ambapo kwenye mtindo wa mambo ya kitaaluma kwa kawaida hutumika sentensi zilizo kamilifu - zenye kiima na prediketa. Hali kadhalika lafudhi ya kuchekesha ya akina “Pwagu na Pwaguzi” tunayoisikia kwenye redio itajikuta kuwa si mahala pake iwapo itatumiwa kwa mfano, na mtoa hoja bungeni. (Linganisha vile vile utofautiano wa lafudhi ya “uncle J. Nyaisanga” kwenye kipindi cha Klabu Raha Leo Shoo na ile ya “Julius Nyaisanga” wakati anaposoma Taarifa ya habari).
Zana maalum za kiisimu zinazotumika mara kwa mara katika mawasilaino yahusuyo shughuli fulani za jamii huonekana kama kwamba zina “kivuli” maalum kimtindo. Na kivuli hiki kinaweza kuhisika hata kama zafla hiyo itasimama peke yake (bila kutumika katika sentensi) au iwapo itatumika mahala pasipo pake kimtindo. Kwa mfano, ni wazi kabisa kwamba maneno kama “chauchau”, “daladala”, “sanyasanya”, “mitumba”, “so” n.k. yana hali fulani ya kivuli cha mtindo wa mawasiliano yasiyo rasmi, yawe yametumika katika sentensi au hata kama yamesimama pekee. Kwa hiyo itakuwa ni makosa kwa namna fulani kimtindo kuyakuta maneno haya katika mitindo mingine, mathalani mtindo wa kirasimu. Kwa mfano, hatuwezi kusema: “Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ameidhinisha Sehemu ya Kamusi kupewa so kumi (yaani shilingi elfu moja) kwa ajili ya kununua kamusi za marejeo” wakati wa kutoa ripoti kwenye mkutano wa Wakuu wa Sehemu. Vivyo hivyo neno “ndugu” lina kivuli cha mtindo wa kirasimu na si kawaida mtu nyumbani kwake, wakati wa maongezi na mke na watoto wake kulitumia. Kumwita mke nyumbani “Ndugu mama Zuberi!” ni kulitumia neno “ndugu” mahali pasipo pake kimtindo. Na hili ni kosa.
Hivyo basi kwa kuzingatia mambo yote tuliyoyajadili hapo juu tunaweza kuifasiri mitindo kama mifumo ya zana za kiisimu inayotokana na maendeleo ya kukua kwa lugha ambayo hutofautiana kufuatana na kutumiwa kwake katika mawasiliano yahusuyo nyanja mbalimbali za kazi au shughuli muhimu za jamii.
Kulingana na fasiri hii tunaweza kuigawa mitindo ya lugha ya Kiswahili (na lugha yoyote nyingine) katika makundi yafuatayo:
1. mtindo wa kitaaluma,
2. mtindo wa kirasimu,
3. mtindo wa magazetini na shughuli za kisiasa,
4. mtindo wa mawasiliano yasiyo rasmi.
Pamoja na hayo yote kuna suala moja ambalo limekuwa likileta kero na mabishano makali sana baina ya wataalam wengi wa elimumitindo, nalo linahusu kuwepo au kutokuwepo kwa mtindo maalum unaotumika katika fasihi (yaani maandishi ya kisanii kama vile riwaya, tamthilia, mashairi, tenzi, ngonjera, hadithi fupi... n.k.). Baadhi ya wataalam wanakubali kwamba mtindo wa shughuli za kifasihi upo kwa madai kwamba unahudumia nyanja maalum ya kazi za jamii - fasihi na sanaa. Lakini uchunguzi na upekuzi wa ndani zaidi wa suala hili umeonyesha kwamba iasihi haina mtindo maalum, bali hutumia mitindo yote minne tuliyoitaja hapo awali, tena kwa pamoja. Tena fasihi si lazima itumie kisanifu tu, bali hata lahaja, misimu na pengine hata lugha za kienyeji na za kigeni zinaweza kupenyezwa.
Sura hii imechanganua mambo mengi ikiwa ni pamoja na maana na umuhimu wa elimunutindo, dhana ya mitindo, mitazamo mbalimbali ya mitindo na historia ya nutindo hadi kufikia mgawanyo wa aina kuu nne za mitindo. Katika sura zinazofuata tutaijadili kwa undani zaidi mitindo tuliyoidhahinisha na kuonyesha nduni zinazoipambanua.