Breaking News: Mwanasiasa mkongwe, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia


Habari tulizozipokea hivi punde zinasema kuwa mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia leo alfajiri Ijumaa Februari 2,2018 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

Mzee Kingunge alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam takriban mwezi mmoja uliopita.

Mke wa Kingunge Peras Ngombalemwiru alifariki dunia mwanzoni mwa mwezi January kutokana na ugonjwa wa kupooza kipindi ambacho Mzee Kingunge alikuwa tayari anapatiwa matibabu ya majeraha hayo. 

Mzee Kingunge alikuwa kiongozi mwandamizi nchini Tanzania katika serikali za awamu nne zilizopita na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali  zikiwemo ukuu wa mikoa ya Tanga na Singida, Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi na Waziri katika wizara mbalimbali

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?