Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi la UNHCR, limedai kuwa jumla ya wakimbizi 1200,raia wa jamhuri ya Demokrasia ya Congo,wameyakimbia mapigano yanayoendelea Mashariki mwa nchi hiyo na kuingia Tanzania.

Aidha shirika hilo limedai Maelfu ya watoto, wanawake na wanaume, wameacha makazi yao kukimbia mapigano dhidi ya makundi yenye silaha ya Mai Mai yanayoendelea Kusini mwa Jimbo la Kivu.

Aidha shirika hilo la umoja wa mataifa limedai mbali na Tanzania,wakimbizi wengine wamekimbilia nchi za Burundi, na Uganda.

Wakati huo huo, inaamika kwamba, kuna wimbi kubwa zaidi la wakimbizi ambao wapo Kivu Kusini wakiwa katika hali mbaya ya kukosa chakula na makazi.