Serikali imezima matangazo ya Television Kenya

Wakati wafuasi wa Muungano wa upinzani nchini Kenya (NASA) wanaendelea na shughuli ya kuapishwa kwa Raila Odinga kuwa ‘Rais’ serikali nchini humo imepiga marufuku TV za Kenya kurusha LIVE matangazo hayo kutoka katika uwanja wa Uhuru Park TV hizo ni Citizen, KTN na NTV.

Wafuasi wa Upinzani tayari wamekwisha fika katika uwanja wa Uhuru Park kushuhudia tukio hilo

Inaelezwa kuwa serikali nchini Kenya ilikuwa imekwisha tahadharisha kuhusu vyombo vya habari nchini humo kurusha live matangazo hayo ya Odinga kuapishwa ambapo ni kinyumme cha sheria.

Hata hivyo vyombo vya habari vya kimataifa havijafungiwa na vinaendelea kurusha matangazo hayo kama kawaida.

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?