OKWI BADO NI HATARI ANGALIA ALICHO WAFANYA HAWA WAFARANSA

KAMA ulidhani kiwango cha Emmanuel Okwi kimeshuka baada ya kusota sana benchi kwenye klabu ya Sonderjyske ya Denmark basi unajidanganya, nyota huyo aliyerejea Uganda na kujiunga na SC Villa ‘Jogoo’ yuko bado yuko juu na hashikiki kwa kutupia nyavuni.

Katika michezo sita tu aliyoichezea Villa, Okwi ametupia mabao saba huku akitisha kwenye timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’ alikokabidhiwa kitambaa cha unahodha pia.

Katika mchezo wa hisani kati ya Cranes na Jeshi la Ufaransa uliopigwa Jumamosi iliyopita Okwi alizidi kuuthibitishia umma juu ya uwezo wake pale alipopachika bao moja na kusaidia kupatikana kwa jingine katika ushindi wa mabao 3-1 walioupata.

Hizi hapa ni picha zinazoonyesha jinsi alivyosababisha penati iliyosaidia kupatikana kwa bao la kwanza lililofungwa na Geofrey Sserunkuma kabla yeye mwenyewe hajatupia la pili akiwa ndani ya sita na Martin Kizza kufunga kitabu cha mabao kwa upande wa Cranes kwa penati

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?