Viumbe watano wanaopewa heshima jeshini mbali na binadamu
Kwa kawaida wanyama hurahisisha maisha ya wanadamu kwakuwa walinzi wetu, chakula chetu na usafiri wetu lakini kuna baadhi ya wanyama na ndege walioweza kujiwekea heshima duniani hasa kwenye sekta maalum za kijeshi na wameweza kupata nafasi za juu jeshini.
1: Sir Nils Olav
Nils Olav ni ndege aina ya Penguinalipewa cheo mara ya kwanza mwaka1972 na kuwekwa kwenye timu ya walinzi wa mfalme Harald V Loudon wa Norwaykwa sasa Sir Nils Olav ni Brigediaanapewa heshima zote za kijeshi ikiwemo kupigiwa saluti na kukagua jeshi.
2: Treo
Ni mbwa aliyetumikia jeshi la Uingerezakuanzia mwaka 2001 mpaka 2015 , Trioana medali zisizopungua 63, alipewa medali hizo baada ya kufaya kazi kubwa ya kutegua mabomu na kutambua mahali mabomu yalipo fichwa.
3: William of Orange.
William ni njiwa aliyekuwa mwanajeshi wa jeshi la Uingereza mwenye namba MI14, mwaka 1944 William alipewa medali ya 21 baada ya kupeleka ujumbe uliyookoa vifo vya wanajeshi zaidi ya 2000 kwenye vita ya Arnhem wakati wa vita ya pili ya dunia.
4: Taffy IV.
Huyu ni mbuzi aliyetumikia jeshi laUingereza tangu mwaka 1775 Taffy IValichukuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1774 na kuingizwa kwenye jeshi maalum la Uingereza alipokutwa anarandaranda porini, alipewa medali ya 14 ambayo ni medali maalum waliyopewa wanajeshi wa Uingereza wakati wa vita ya kwanza ya dunia (ww1).
5: LIN WANG
Ni tembo aliyekuwa mwanajeshi wa jeshi la China kuanzia mwaka 1942 Lin Wangalitumika kujenga majengo marefu ya jeshini, kusafirisha chakula wakati wa vita na alitumika kama kivutio kwa ajili ya kukusanya fedha wakati wa njaa kipindi cha vita alipewa medali 12 za kijeshi.
SHERE POST
By EMANUEL MASHELE 0766605392
Comments
Post a Comment