Kaburi alilozikwa yesu lafunguliwa tena Israel
Chumba kidogo kinachofunika kaburi ambako inaaminika Yesu Kristo alizikwa kimefunguliwa rasmi tena baada ya kufanyiwa ukarabati kwa miezi tisa katika Kanisa la Kaburi la Yesu Kristo katika maeneo ya mji wa zamani wa Jerusalem kilikuwa kimekuwa dhaifu sana kiufundi.
Aidha, kilikuwa limebadilika rangi na kuwa karibu rangi nyeusi kutokana na masizi ya mishumaa mingi ambayo huwashwa eneo hilo.
Kanisa takatifu lafunguliwa Israel
Mji wa kale sana wagunduliwa Misri
Mzozo kati ya madhehebu matatu ambayo kwa pamoja husimamia kanisa hilo - Kanisa la Kiothodoksi la Ugiriki, Kanisa la Kiarmenia na Kanisa Katoliki la Kirumi - ulichelewesha ukarabati huo kwa miongo mingi.
Antonia Moropoulou, aliyesimamia ukarabati, amesema chumba hicho sasa kimepata tena rangi yake asili inayokaribia hudhurungi.
Chumba hicho kilifanyiwa ukarabati
Comments
Post a Comment