Penzi shubiri :2
MTUNZI: JOSEPH SHALUWA ILIPOISHIA JANA... Baada ya kufanya mipango yote kwa siri, tuliamua tukapumzike Marangu Mtoni, twende huko siku ya week-end tukafurahie maisha! Kila nikiufikiria uzuri wa Linna nazidi kuchanganyikiwa, siyo siri Linna ni mrembo jamani! Tamaa ya mapenzi ilinizidi, mshawasha wa mapenzi ukanipanda nikaamua kumweleza hisia zilizoko katikati ya moyo wangu. Mwanzo niliogopa, lakini nijipa moyo nikamweleza. Cha ajabu sasa, wala hakukataa, alikuwa maharage ya Mbeya! Maji mara moja! Akadai eti alikuwa ananipenda mimi tu na alikuwa na Shams kwa sababu ya kitu kimoja tu; pesa! Si vinginevyo. Mh! Jamani nyie!!! SASA ENDELEA... KWANZA tulienda kushangaa maporomoko ya maji kwenye milima iliyokuwa jirani na hoteli tuliyofikia. Tulipata upepo na hewa safi ya mlima Kilimanjaro. Kaubaridi ka eneo hilo kalikuwa si mchezo! Baada ya hapo tukaingia maeneo ya chini kabisa ya maporomoko ya maji yale, ambapo kulikuwa na vijito vidogovidogo. Tukaanza kuchezea maji ambayo yalikuwa baridi kabisa. Tuliufurahia uumbaji wa Muumba wetu! Kweli ashukuriwe! Hapo tulipokuwepo hapakuwa mbali sana na geti la kuingilia mlima mrefu kuliko yote Afrika - Kilimanjaro. Tulikuwa kilomita chache sana karibu na mwanzo wa mlima maridadi ambao tunajivunia kuwa nao na unauingizia nchi yetu fedha za kigeni kila kukicha. Penyewe paliitwa Kilimanjaro National Park. Baada ya kuridhika na utalii feki wetu, tuliongozana moja kwa moja mpaka Marangu mtoni darajani; tukapanda barabara ya kuelekea Kilema. Kwa umbali kidogo tukaona jengo moja la ghorofa mbili, tukalipenda, baada ya kulichunguza kwa muda tuling’amua ilikuwa hoteli. Ilikuwa karibu na Chuo cha Ualimu cha Marangu. Sikumbuki vizuri jina la hoteli hiyo lakini tuliingia na kutafuta mahala pazuri patakapofaa kwa ajili ya mazungumzo. Macho yetu yalipata burudani ya kuangalia maua ya kila aina ya liyokuwa kila kona ya ile hoteli. Burudani ambayo hatukuilipia gharama yoyote. “Pazuri sana hapa, nadhani patatufaa sana kwa ajili ya mazungumzo au vipi?” nilimwambia Linna huku nikisogelea sofa moja kubwa lililokuwa karibu na pale tulipokuwa. ”Sawa mpenzi, hakuna tatizo,” aliniambia. Japo moyoni niliogopa! Kutembea na mchumba wa rafiki yangu tena kwa uhuru kiasi kile ilikuwa siyo haki hata kidogo. Kuna wakati nilikuwa najiuliza itakuwaje siku Shams akigundua kuwa namchukulia Linna wake. Niliamua kumshirikisha Linna suala lile kwa sababu ni wazi kuwa lilikuwa linamuhusu yeye na mimi. ”Hivi Linna, Shams akijua itakuwaje?” nilimwuliza. Unajua alinijibu nini? Alinisogelea na kuuchukua mguu wake mmoja akaubebanisha juu ya mguu wangu. Kutokana na kuvaa nguo laini iliyosababisha nihisi joto la mwili wake barabara, kisha akafungua kinywa chake, akaanza kuzungumza. “Labda umwambie wewe, na atajuaje? Hata akijua kwani atafanyaje? Shams kwangu haongei kitu na hata hivyo wala simpendi, mimi nakupenda wewe!” aliniambia. Jasho la woga likanitoka! Ni wazi kuwa sikuwa nahitaji jibu la aina ile. “Yaani hampendi Shams, kwa sababu yangu? Shams akijua si ataniua? Pesa ni kila kitu bwana! Shams ana uwezo wa kunipoteza kwa kutumia pesa zake,” niliwaza mwenyewe akilini mwangu. Nilikosa raha ghafla. Nikabadilisha mada, tukaanza kuzungumza mambo mengine. Tukamwita muhudumu atuletee vinywaji. Haikuchukua muda yule dada akaja na chano kilichobeba vinywaji. Alifungua zile bia kisha akamimina kwenye glasi zetu. Tukagonganisha na kunywa kwa furaha huku tukisubiri chakula ambacho tulikuwa tumeweka oda awali. Dakika chache baadaye yule dada aliyetuhudumia mara ya kwanza akatokeza na chano kilichobeba chakula. Tulikula na kulishana kwa furaha. Kuna wakati mwingine nilikuwa natoa chakula nilichotafuna kinywani mwangu na kumlisha Linna! Hata yeye alifanya hivyo hivyo. Hatukuona kinyaa tena! Tulijua kitu kimoja tu! Mapenzi! Ndiyo kitu kilichokuwa vichwani mwetu muda huo. Roho ya usaliti ilikuwa imeshanivaa, sikujali wala kukumbuka tena fadhila ambazo amenifanyia rafiki yangu Shams. Kweli binadamu tunasahau haraka. Nilijihalalishia penzi kwa mpenzi wa rafiki yangu bila kujali chochote, sasa sijui nd’o kusema nimetumia ule msemo wa ‘kizuri kula na ndugu yako hata kama kidogo’ hata hivyo sifahamu kama shabaha ya msemo huu wa Kiswahili ni kwa mambo maovu kama haya ninayomfanyia rafiki yangu Shams. Ngoja niwaambie kitu kimoja; Linna alikuwa mzuri jamani, kama ungefanikiwa kumuona naamini ungekubaliana na mimi. Hata kama ni wewe lazima uzalendo ungekushinda! Kwa hiyo tusilaumiane. “Naomba utuongeze bia mbili!” nilimwambia mhudumu mara baada ya kuja kuchukua vyombo. “Sawa!”aliitika kwa sauti laini ambayo inayoshtua. Kweli ilinishtua hata mimi kiasi nikalazimika kumsindikiza na macho yangu mawili kuangalia makalio yake yakipishana wakati akitembea. Hata Linna alinishtukia! Akaanza kunibadilikia, akaniuliza: “Mbona unamwangalia sana huyo dada?” ungemwona usoni sasa amevimba huyo! “Kivipi?” nikamdunga swali jipya badala ya kumjibu aliloniuliza. “Kama mambo yenyewe nd’o haya aka! Mimi naondoka!” ndivyo alivyoniambia. Hivi kama ni wewe ungemjibu nini? Unajua kuna mambo mengine yanahitaji akili mpaka zile za akiba! Ninachoamini ni kwamba; hawa viumbe wametoka kwenye ubavu wetu, sasa kwa nini watushinde? Kwa maana hiyo sasa inamaanisha bila mwanaume, mwanamke asingekuwepo! Ndivyo ilivyo! Sasa unajua nilichokifanya? Nilimsogelea na kumlaza kifuani mwangu nikampigapiga mgongoni taratibu sana kana kwamba nilikuwa namkuna hivi, halafu nikautoa ulimi wangu nikautumbukiza sikioni mwake! Ilikuwa balaa! Alilalama huyo, nikafungua kinywa changu nikamwambia: “Mimi nakupenda mpenzi, nakupenda sana na kamwe siwezi kukulingalisha na wanawake wa baa hata siku moja. Naomba uniamini, ni macho tu yalikuwa yameteleza, naomba tuchukue chumba nikakuenzi mpenzi,” ndivyo nilivyomwambia, japokuwa sijui hata hayo maneno yalitokea wapi. Kweli wanaume wanajua kuimbisha! “Kweli?” aliniuliza. “Niamini! Linna,” nilimwambia. “Nakuamini Masumbuko.” Nikamwondoa mikononi mwangu nikaelekea mapokezi, huko nikapokelewa na tabasamu pana lililojaa bashasha. Alikuwa ni mrembo haswa, sijui maana halisi ya jina la Masumbuko, sifahamu kwa nini wazazi wangu waliamua kuniita jina hilo na siyo lingine lolote kwa sababu duniani kuna majina chungu nzima. Hata hivyo sikuwahi kuwauliza wazazi wangu maana halisi ya jina langu la MASUMBUKO! Lakini najishangaa kwa nini nasumbuka hivi. Kumbuka nimekuja na Linna kutoka Moshi, nikamtamani mhudumu aliyetuhudumia, huku mapokezi napo nakutana na kimwana mwingine mrembo na wala hajasingiwa urembo wenyewe! Sijui kwa nini sijatulia kiasi hiki! Nadhani natakiwa kupepewa! Nilionyesha ushirikiano wangu japo kwa kumwonyesha tabasamu langu, baada ya kusalimiana na kunihakikishia kuwa nitapata chumba aliniuliza maswali kadhaa huku yeye akiwa anaandika katika kitabu cha wageni. “Jina lako?” “Masumbuko!” nilimwambia, badala ya kuandika alinikodolea macho kwa nukta kadhaa akaniuliza tena: “Masumbuko nani?” “Sumbuo.” “Kabila lako?” “Mngoni,” nikamwongopea. “Kazi yako?” “Dereva.” “Umetokea wapi?” “Moshi.” “Unaelekea wapi?” “Ndiyo nimefika!” “Utakaa siku ngapi?” “Moja tu!” Akanipa kitabu, akanionyesha mahala pa kutia sahihi, nikafanya hivyo. Nikamlipa haki yake... nikataka kuondoka akaniita...akaniuliza... “Samhani kaka upo peke yako?” aliniuliza kwa sauti legevu kama ndiyo alikuwa ametoka kulala. “Hapana nipo na wifi yako,” nilimwambia. Siyo siri jibu lile halikumpendeza kabisa. Mimi siyo mwanasaikolojia ila kwa uzoefu wangu wa kujua mambo, yule dada alikuwa tayari kashanizimikia kiana. Dakiaka chache baadaye tulikuwa tunapanda ngazi za kuelekea kwenye chumba chetu ambacho kilikuwa ni namba 502. Haikutuchukua muda tulikuwa chumbani mwetu. Chumba chenyewe sasa! Hutotamani kutoka ukiingia, kilikuwa na kila kitu ndani. Kitanda sita kwa sita, kilichobeba godoro nene lililofunikwa na mashuka meupe pee! Mito minne iliyotandazwa kila kona ya kitanda, feni pamoja na sofa kubwa ni baadhi ya vitu ambavyo vilipendezesha chumba na kuonekana nadhifu kabisa. Tuliingia bafuni tukaogeshana. Nilimsugua Linna mgongoni, naye akafanya hivyo. Tulifanya usafi wa jumla! Baada ya kuridhika na usafi wenyewe tulirudi chumbani tukiwa kama tulivyozaliwa. Tukakimbizana na kucheza michezo ya kila aina, baadaye tukaingia katikati ya dimbwi la bahari ya mapenzi. Jamani acheni! Mtoto alikuwa na kiuno kinazunguka kama feni! Nilizungushwa pale kitandani hadi nikahisi kama sikuwa na maandalizi kabla ya mchezo ule. Linna alikuwa anajua anachokifanya. Nadhani kama ni ngoma za unyago, yeye alikuwa mwalimu wao! Siyo siri Linna alinipagawisha sana. Nilihisi hakuna kufa tena. Niliona kama nilikuwa nimechelewa sana kupata furaha ya maisha. kama mchezo vile, dakika ishirini zikatosha kumaliza kazi iliyokuwa mbele yangu! Kazi ya kumfurahisha Linna. Haikuwa kazi ndogo kiukweli. Tukajiandaa ili tucheze raundi ya pili ya mchezo wenyewe. Purukushani zikaanza upya! Baada ya kuona kuwa tupo tayari kwa kuanza safari yetu ya mahaba. Tukavamiana! kiasi cha kama dakika moja tu kupita wakati wa mchezo huo, simu yangu ikaita. Ndiyo iliyosababisha tukakatisha safari yetu ya mahaba na hababi wangu Linna. Nikajitoa mikononi mwake! NILISHTUKA SANA! HADI NIKACHUKIA! Unajua ni nini? Eti nilikuwa naota. Ndoto ya pili sasa hii? Ndoto hizi ni za namna gani jamani? Huwezi kuamini nilikuwa kijiweni kwangu, tena ndani ya taksi yangu. Nikafumba macho na kuyafumbua kwa nguvu mara kadhaa, niligundua ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea. ni kweli ilikuwa ndoto! Tena ndoto za aninacha! “Mhh! Jamani ndoto gani hii tena jamani?” nikajiuliza tena. Sikuwa na kitu kingine zaidi ya kupokea ile simu. Alikuwa ni Shams, rafiki yangu, mteja wangu na sioni haya kumwita bosi wangu! Kweli kwagu alikuwa bosi! Baada ya kuzungumza naye tulikata simu zetu. Aliniambia kuwa ikifika saa 12:00 jioni niende Majengo nikamchukue Halima kisha nimpeleke hotelini. Alinitaka nivae nguo nzuri za kupendeza kwa ajili ya kwenda club jioni hiyo. Sijui huyu jamaa hachoki, yaani nimemwacha na Linna na bado anamtaka tena Halima. Kweli ilikuwa mchaka…mchaka! Sikuwa nimejikagua vizuri, baada ya muda nikaamua kuiangalia suruali yangu vizuri. Daaah! Mambo yalikuwa mengine! Nilikuwa nimemaliza saa nyingi! Niliharibikiwa! Nilijionea huruma mwenyewe, masikini nikaamua kuchomolea shati langu kisha nikawasha gari langu na kuelekea nyumbani kwangu Oysterbay. *** Niliingia bafuni na kufungulia bomba la mvua, maji yakaanza kutiririka kila kona ya mwili ya wangu. Nikajipaka sabuni mwili mzima, nikachukua dodoki laini sana na kulitembeza mwilini mwangu. Nilitumia muda mwingi sana kuoga siku hiyo, nadhani ni kuliko siku zote. Sikufahamu sababu ya mimi kuchukua muda mrefu kiasi hicho. Nikaanza kurejewa na kumbukumbu za ile ndoto niliyoota. Nilibaki nimeduwaa, sikuwa na la kufanya. “Kwa nini nimeota ndoto ya namna ile lakini jamani mimi? Au itatokea hivyo nini? Ndoto nyingine unaweza ukaota kumbe ndivyo itakavyokuwa,” niliwaza akilini mwangu, peke yangu nikiwa bafuni. Ni kweli nilitamani sana ndoto ile iwe kweli. Nikajikausha na taulo safi, nikarudi chumbani kwangu kwa ajili ya mapumziko mafupi. Nikategesha kengele kwenye saa iliyokuwa kwenye simu yangu ili inishtue muda ule ambao mteja wangu alitaka nikamchukue. Haikuchukua muda mrefu, nilikuwa nimeshapotelea usingizini. *** Starehe kwake ilikuwa ni kila kitu! Kuliko asifanye starehe ilikuwa bora afe! Kazi yake mahususi sikuwa naifahamu. Wala yeye hakuwahi kunieleza. Hata hivyo sikutaka kumwuliza kwa kuogopa kuwa kuuliza kwangu kunaweza kumaanisha tamati ya ajira yangu kutoka kwake. Kwa kuhofia hayo sikutaka kabisa kumwuuliza ila aliwahi kuniambia kuwa yeye ni mfanyabiashara. Ila hakutaka kuniweka wazi kuwa ni biashara gani aliyokuwa anafanya. Baada ya mimi kuondoka nilimwacha na mpenzi wake Linna, binti mrembo, mtoto wa Kitanga. Siyo siri sioni haya kumsifia Linna jamani ni mzuri huyo usis’kie! Aliendelea kuufaidi uzuri wa Linna atakavyo. Baada ya kuridhika na mapenzi ya Linna alimkumbuka Halima. Ndiyo maana akanipigia simu ili nikamchukue Nakumbuka kuna wakati aliwahi kuniambia kuwa: “Mapenzi pesa bwana, mapenzi matamu na hayawezi kubadilika kuwa shubiri asilani abadani! Mbele ya pesa kila kitu ni kupeta tu! Hakuna raha nyingine duniani zaidi ya mapenzi, mapenzi matamu rafiki yangu!” Alichokifanya ni kummwagia minoti Linna kisha akamsindikiza na maneno matamu ya kimahaba: “Linna mpenzi, chukua hizi pesa, zitakusaidia kwa matumizi madogomadogo mpaka nitakaporudi kesho. Kwa sasa naelekea Arusha.” Ilikuwa uongo mtupu! Alisema hivyo ili apate fursa ya kujivinjari na Halima usiku kucha! Linna alionyesha furaha isiyo na kifani wakati akipokea zile fedha kutoka kwa Shams! Shams akamtulizia macho Linna kwa dakika na sekunde kadhaa, akagundua kitu. Macho ya Linna tayari yalikuwa yameshabadilika rangi na kuwa mekundu kama alikuwa alikuwa analia muda mrefu. Wakarukiana. Wakakumbatiana. Midomo yao iligusana, wakaanza kubadilishana mate. Haikuchukua muda mrefu tayari walikuwa kama walivyozaliwa kitandani wakicheza michezo ya kikubwa! Ndiyo maana nashawishika kusema kuna baadhi ya wanawake wanampenda mtu kutokana na pesa zake. Pesa zikiisha na mapenzi yanaisha. Purukushani hizo za mahaba ziliendelea kama ndiyo wamekutana siku ya kwanza. Kila mtu alikuwa haishwi hamu na mwenzake. *** Nilizinduka usingizini nusa saa kabla ya muda wa ahadi na Shams. Nikaingia bafuni kujiondoa uchovu kidogo. Kichwani mwangu nilishaingiwa na mawazo ya usaliti. Kitu nilichopanga ilikuwa ni kwenda kumchukua Halima, halafu baada ya hapo nimfuate Shams. Nikishahakikisha Shams yupo na Halima, nirudi kwa Linna nizungumze naye. Bado niliendelea kuteswa sana na ile ndoto niliyoota mchana kule kijiweni. Kwa kweli nilihisi nikijaribu zali, naweza nikampata. “Hebu nijaribu!” nikawaza. “Nitampata tu!” Nilizidi kuwaza. TOA MAONI YAKO TAFADHALI! ITAENDELEA JUMAPILI ASUBUHI..
Comments
Post a Comment