Posts

Showing posts from April, 2023

Asimamishwa kwa kupeleka Mganga shuleni

Image
   Vitendo vya ushirikina na kupiga ramli chonganishi vimesababisha mkuu wa shule ya Sekondari Imenya Kata ya Itwangi Halmashauri ya Shinyanga Seleman Karavina  kusimamishwa kazi  kutokana na kupeleka mganga wa kienyeji shuleni na kupiga  ramli chonganishi. Akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani cha robo ya tatu ya mwaka, Diwani wa Kata ya Itwangi Sonya Jilala alisema baadhi ya wanafunzi walikuwa wakianguka mapepo hovyo na kupiga kelele.  Alisema hali hiyo ilizuwa taharuki shuleni baada ya mwalimu kupeleka mganga wa kienyeji shuleni na kupiga ramli chonganishi ambayo iliwatuhumu baadhi ya wazazi wanahusika kufanya vitendo vya kishirikina na kusababisha taharuki. “Haya mambo yametokea hivi karibuni ambapo mwanafunzi mmoja wa kidato cha pili aliandikiwa barua na watu wasiojulikana akituhumiwa yeye na wazazi wake ni washirikina watauawa” alisema Mhela.  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Shinyanga Nice Munissy amekiri kupokea taarifa ya mwa...

WASHINDI TUZO ZA TMA 2022

Image
  Wafuatao ni washindi wa Tuzo za muziki Tanzania (TMA) zilizoandaliwa na Basata usiku wa kumakia leo Aprili 30, 2023 katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki, Dar. 1. WIMBO BORA WA FLEVA Upo Nyonyo – Phina Tamu – Barnaba Dunia – Harmonize Kwikwi – Zuchu Dear Ex – Marioo   2. MWANAMUZIKI BORA WA KIUME BONGO FLAVA Amelowa – Harmonize Huyu hapa – Mbosso Do Do – Dully Sykes Naogopa – Marioo ft. Harmonize Asali – Ali Kiba   3. MWANAMUZIKI BORA WA KIKE BONGO FLEVA Sitaki Mazoea – Shilole Siwezi – Nandy Kwikwi – Zuchu Tai Chi – Ruby Nishazoea – Malkia Karen   4.  MWANAMUZIKI BORA WA KIUME HIP HOP Kumbuka –Kala Jeremiah Puuh – Billnass ft. Jaymelody One Call Away – Country Wizzy Tawile – Fid Q ft. Rich Mavoko Tanzanite – Joh Makini ft. Jay Rox   5. MWANAMUZIKI BORA WA KIKE HIP HOP Witirialdo – Witness Kibonge Mwepesi Bibi Titi Vol. 1 – Trixy Tonic Hapa – Ge2 New Material – Chemical Blue Print – Rosa Ree   6. WIMBO BORA WA HIP HOP Blue Print – Rosa Ree New Mate...

Bosi BBC ajiuzulu

Image
  Mwenyekiti wa shirika la utangazaji la BBC Richard Sharp. Mwenyekiti wa shirika la utangazaji la BBC Richard Sharp alijiuzulu Ijumaa baada ya ripoti huru kubaini kuwa alikiuka kanuni kuhusiana na mkopo wa dola milioni moja aliochukua waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, Boris Johnson, akiwa madarakani. Kuondoka kwake madarakani kunakuja wakati wa uchunguzi wa kisiasa katika shirika hilo la utangazaji la Uingereza. Mzozo wa mkubwa sana unaomhusu mtangazaji ayelipwa mshahara mkubwa zaidi Gary Lineker, katika mzozo huo wa kutoegemea upande wowote ulitawala vichwa vya habari nchini Uingereza mwezi uliopita. Sharp, ambaye aliwahi kufanya kazi katika benki ya Goldman Sachs alichukua nafasi ya mwenyekiti wa BBC mwaka 2021, alikuwa katika shinikizo tangu mwezi Februari wakati kamati ya wabunge iliposema kuwa alifanya “makosa makubwa katika maamuzi” kwa kushindwa kutangaza kuhusika kwake katika mkopo huo. Sharp alisema amekubali kuendelea kuwepo kazini hadi mwisho wa Juni ili kuipa serikal...

SIMBA YATUPWA NJE KWA MIKWAJU YA PENATI

Image
  KLABU ya Simba imetolewa na Wydad Casablanca kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CAF CL). baada ya kupokea kichapo kwa mikwaju ya penati 4-3 mara baada ya matokeo kuwa 1-0 (agg 1-1) Katika mchezo huo ambao Simba alikuwa na faida ya bao moja mbele, waliingia uwanjani na kikosi kilekile kilichoanza mkondo wa kwanza Jijini Dar es Salaam ambacho kiliwasaidia kuondoka na ushindi wa bao 1-0. Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Mohamed V nchini Morocco Wyadad waliweza kumuanzisha mshambuliaji wao hatari raia wa Senegal Bouly Sambou ambaye alionesha uhatari wake na kuweza kupata bao dakika ya 24 ya mchezo.

WATANZANIA WALIOKWAMA SUDANI WAREJEA

Image
  Ndege iliyowabeba raia wa Tanzania waliokuwa wamekwama Sudan imewasili salama Jijini Dar es salaam. Watanzania hao waliookolewa waliondoka Sudan kwa mabasi kuelekea Addis Ababa kabla ya kuwasili nchini kwa ndege ya Shirika la Ndege ATCL. Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Dkt.Stergomena Tax amesema kufuatia siku tatu za kusitisha mapigano nchini Sudan,wameweza kuwasafirisha Watanzania 200, wanafunzi, watumishi wa Ubalozi na raia wengine.

MIILI YA WAKENYA 21 WALIOFUNGA HADI KUFARIKI YAFUKULIWA

Image
  Jeshi la Polisi nchini Kenya wamefukua miili ya watu 21 ambao ni waumini wa kanisa la News International Church, ambao inadaiwa wamefariki dunia kwa njaa baada ya kufuata maelekezo ya mchungaji wao ya kufunga mfululizo. Mchungaji Paul Makenzie Nthenge ndiye anayedaiwa kuwapa maelekezo hayo waumini wake, ikidaiwa kwamba aliwaambia wakifunga mfululizo, wataenda kuonana ana kwa ana na Yesu. Tayari mchungaji huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini humo huku taarifa zikieleza kwamba huenda makaburi mengine yakabainika. Credit: DW

Mwanachuo Amchinja Mwanae Na Kumla Utumbo

Image
Author:  Mwanafunzi wa chuo kimoja kikuu nchini Kenya amemuua kinyama bintiye mwenye umri wa miaka miwili na kula viungo vyake vya ndani. Msichana huyo mwenye umri wa miaka 24 alijifungia ndani ya chumba chake akiwa uchi wa mnyama na kumchinja kama mnyama bintiye “huku akinena kwa lugha na ndimi sisizoeleweka.” Majirani wa mwanafunzi huyo wa somo la biashara aliye na misuli mithili ya mwanaume walisema walishtushwa na makelele ya mtoto huyo aliyekuwa anaomba msaada. Majirani walidhania kwamba amevamiwa na majmbazi, ndipo wakamkuta mwanachuo huyo aliyetambuliwa kwa jina Olivia Kaserran akifanya kitendo hicho. Hadi wanafanikiwa kuvunja mlango tayari Olivia alikuwa amemuua bintiye. Baada ya muda Polisi walifika na kumtia nguvuni. Credit: mcshonde.com

Rais Ruto atoa wito wa kufunguliwa mashtaka kwa mhubiri tata nchini Kenya

Image
Rais wa Kenya William Ruto ametaka kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa mhubiri mwenye utata Paul Mackenzie ambaye aliwataka wafuasi wake kufunga hadi kufa Rais amemtaja mhubiri huyo kuwa gaidi. Matamshi yake yanakuja muda mfupi baada ya Polisi kupata mwili mmoja zaidi kutoka kwenye kaburi la pamoja karibu na mji wa pwani wa Malindi. Hii inafikisha 40, idadi ya waliofukuliwa, na idadi ya vifo ikifika 48. Polisi wameviambia vyombo vya habari kwamba miili miwili zaidi imeonekana na itafukuliwa katika muda mfupi ujao. Maafisa wakuu wa usalama wakiongozwa na Inspekta Jenerali wa Polisi, Japhet Koome na Mkuu wa Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mohamed Amin wanatarajiwa kujiunga na timu ya wachunguzi katika eneo Shahola palipopatikana makaburi ya kina kifupi

AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI MWANZA

Image
  Katika hali isiyokuwa ya kawaida  Mfanya biashara mmoja aliyejulikana kwa jina la  Emmanuel Nyambera Mkazi wa Bwiru Msikitini Wilayani Ilemela  jijini Mwanza  amejiua kwa kujipiga Risasi kifuani kutokana na Migogoro ya kifamilia. Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema Tarehe 16.04.2023 muda wa saa 21:45 usiku, huko maeneo ya Bwiru Msikitini, kata ya Pasiansi, Tarafa na Wilaya ya Ilemela, kuliripotiwa taarifa ya  Emmanuel Nyambera, miaka 40, mfanyabiahashara na mkazi wa Bwiru Msikitini  aliyejipiga risasi kifuani upande wa kushoto na kupelekea kifo chake.  Emmanuel  Nyambera  alikuwa akimiliki Bastola yenye namba za usajili  TZCAR80190  Model namba  79 KCAL 38  aina ya charter ambayo inauwezo wa kuchukua risasi tisa (9) na ndio aliyotumia kujifyatulia  risasi kifuani hali iliyopelekea kifo chake . Chanzo cha tukio hilo ni migogoro ya kifamilia iliyotokana na mgawanyo wa mali za fami...

Ubalozi wa marekani watoa mafunzo jeshi la polisi

Image
    Ubalozi wa Marekani umetoa mafunzo kwa askari wa Jeshi la Polisi Nchini ya namna ya kukabiliana na matukio ya kughushi nyaraka mbalimbali ikiwemo hati za kusafiria(Pass Port) ambapo mafunzo hayo yamehusisha wakufunzi kutoka chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA). Akiwapongeza na kuwapa vyeti vilivyotolewa na ubalozi wa marekani leo April 18.2023 Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi Daktari LAZARO MAMBOSASA amesema vyeti hivyo ni alama ya kile walichosoma kwa lengo la kusaidia Jeshi katika maswala ya kupambana na uhalifu wa kughushi nyaraka mbalimbali. Aidha Daktari mambosasa amewataka wahitimu hao kutumia mbinu walizopata katika mafunzo hayo yaliyotolewa na ubalozi wa marekani ambapo amesema kuwa taifa hilo liko mbele kiteknolojia nakuwaomba watoe mbinu hizo kikamilifu kwa askari ambao watakuja kupata elimu hiyo. Kwa upande wake kamishina msaidizi wa Polisi hamisi Msolo ambaye ni miongoni mwa walio hitimu elimu hi...

Vigezo AJIRA mpya za ualimu na afya 2023

Image
  SERIKALI imesema inatambua uwepo wa walimu katika shule za Msingi na Sekondari wanaojitolea hata hivyo imesisitiza itazingatia vigezo katika kutoa ajira mpya zilizotangazwa wiki iliyopita. Waziri wa TAMISEMI, Angellah Kairuki ametaja vigezo vitakavyo zingatiwa kuwa ni pamoja na wale waliomaliza elimu mwaka 2015, masomo waliohitimu (Fizikia, Biolojia, Kemia, Lugha ya Kingereza na wataalamu wa ufundi katika maabara za sayansi). Waziri Kairuki ametaka wananchi kutowalaumu viongozi hususani wabunge ikiwa watakosa nafasi hizo kwa kuwa utaratibu uliowekwa na Wizara ni wa huru na haki. “Hakutakuwa na nafasi ya upendeleo na mimi nitakuwa nafuatilia kwenye mfumo kuhakikisha wale tu wanaostahili wanaajiriwa,” amesema. “Tutahakikisha zoezi hili linaenda kwa haki. Viongozi mnaonitumia ujumbe wa simu sita jibu sita angalia nani ni nani kwa kuwa mtu asiyemjua mtu atapata shida wanaoomba nafasi hizi waende kwenye mfumo.” Waziri Kairuki ametahadharisha kuwa viongozi watakaoenda kinyume wataadhib...

AUDIO | ROMA Ft. Abiud – Nipeni Maua Yangu | Download

Image
  AUDIO | ROMA Ft. Abiud – Nipeni Maua Yangu | Download ROMA Ft. Abiud – Nipeni Maua Yangu Download Mp3 Audio Audio Player 00:00 00:00  

AVUNJA NDOA YA MIAKA 20 KWA TABIA YA MKEWE KUPAKULIA CHAKULA MAJIRANI

Image
                  Image:  MARGARET WANJIRU           Mwanamume mmoja nchini Zambia amewaacha watu kwa mshangao kubwa baada ya kumpa mkewe talaka kwa sababu ya kuwa na mazoea ya kuwapakulia majirani chakula. George Phiri mwenye umri wa miaka 49 aliamua kumuacha mkewe Tanta Zulu mwenye umri wa miaka 34 ambaye walidumu naye kwa ndoa ya miaka 20, tovuti ya Zambian Observer iliripoti. Phiri aliamua kumshtaki mkewe mwishoni mwa juma katika mahakama ya Matero, akidai anatabia ya kugawa chakula, akiongeza kuwa amekua akiwapatia na watoto wa hao majirani. Akijitetea, Zulu aliiambia mahakama kuwa mumewe alikuwa ni bahili na mkali hadi anafikia hatua ya kupima chakula kilichopo ndani ya nyumba kabla ya kwenda kazini, tovuti hiyo ilisema. Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mfawidhi Harriet Mulenga, alibainisha kuwa sababu za kuachana kwa wanandoa hao hazina msingi. Lakini kwa sababu mlalamikaji alisisitiza kwamba hataki mke...

KENYA, WABUNGE CHAMA TAWALA KUKUTANA NA UPINZANI

Image
  Rais wa Kenya William Ruto. Serikali ya Rais wa Kenya William Ruto, Jumanne, imewatangaza wabunge saba wa Kenya Kwanza watakao shiriki katika mazungumzo na upinzani unaoongozwa Raila Odinga ili kumaliza uhasama wa kisiasa kati ya pande hizo mbili. Hata hivyo chama hicho tawala kimesema hakitashiriki mazungumzo yoyote yatakayohusu kurejeshwa kazini kwa makamishna wanne wa IEBC waliofutwa kazi na Rais Ruto pamoja na kushiriki katika harakati za ufunguaji wa seva za uchaguzi. Majadiliano hayo si ishara ya udhaifu wala njia ya kuishinikiza serikali kukubaliana na matakwa ya wapinzani wake. Mazungumzo hayo yanayotarajiwa kufanyika katika mfumo wa bunge, yatahudhuriwa na wabunge wa chama tawala ambao ni pamoja na Boni Khalwale, Hillary Sigei, Adan Keynan, Lydia Haika, George Murugara, Essy Okenyuri na Mwengi Mutuse. Mazungumzo hayo yatahusu hali ngumu ya maisha, ufufuaji wa uchumi na kuundwa kwa tume ya uchaguzi IEBC na kuwepo kwa makubaliano ya kisiasa. Kiongozi wa Shughuli za Serikal...

MAFURIKO YAUA WATU 7

Image
  Watu 7 wamefariki dunia na wengine 21 hawana mahali pa kuishi kutokana na mto Talanda katika kijiji cha Talanda Kata ya Milepa wilayani Sumbawanga kujaa na kufurika katika makazi ya watu. Mwenyekiti wa Kijiji ch Talanda Oscar Denya amesema  waliofariki dunia ni wanaume watatu na wanawake wanne wote wa familia mbili tofauti. Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Sixtus Mapunda akiwa ameongoza na wajumbe wa kamati ya USALAMA ya Wilaya ametoa Pole kwa maafa hayo na serikali imewahamisha wananchi wa Kaya 10 ambao nyumba zao zote zimesombwa na maji na kuanza kuwajengea nyumba sehemu nyingine.

AJIRA ZAIDI YA 20,000 KUTOLEWA 2023

Image
  Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kutoa kibali cha kuajiri watumishi 21,200. Katika ajira hizo, kada  ya walimu ni ajira 13,140 kwa shule za msingi na sekondari na kada ya afya ni ajira 8,070 kwenye halmashauri vituo vya afya na zahanati. Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI, utaratibu wa kuajiri unaanza leo Aprili 16, 2023.   UNATAFUTA KAZI BOFYA >HAPA>>

JELA MIAKA 20 KWAKUKUTWA NA PEMBE ZA NDOVU

Image
  Watu wanne wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 kwenda jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kukutwa na vipande vipande vya pembe za ndovu, kinyume cha sheria ya wanyama pori ya mwaka 2005 iliyofanyiwa wanawake mwaka 2016 wakiwa katika hatua za mauzo ya nyara hizo za serikali. Hukumu hiyo imetolewa katika mahakama ya hakimu mkazi wa Mkoa wa Shinyanga na hakimu mkazi Yusuph Zahoro, baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili na kuwatia hatiani watakiwa wote wanne wa nyimbo na Kesi ya uhujumu uchumi namba 1 ya mwaka 2022. Washitakiwa hao walikutwa na vipande 9 vya pembe za ndovu thamani ya milioni 6921 ambapo watakiwa walikamatwa wakiwa katika hatua za kuuza nyara hizo kata ya Solwa wilaya ya Shinyanga. Waliohukumiwa kifungo cha miaka 20 jela ni Emanuel Shija Basu, Shija Kaswahili, Revocatus Mtara na Daud Ndizu ambao walitenda kosa hilo July 13 , 2022 baada ya kukutwa na nyara za serikali kinyume cha sheria.

DOWNLOAD QASWIDA MPYA, AUDIO | Abydad – RAMADAN Kareem | Download

Image
Abydad – RAMADAN Kareem Download Mp3 Audio Audio Player

Maneno mapya yakutongoza

Image
  Ili uweze kumpata kirahisi mwanamke unayemtaka unatakiwa kujifunza mbinu mpya za kutongoza. Wengi wanashindwa kuwapata watoto wanaowapenda kwa sababu ya kutumia maneno ya kawaida au ambayo yamepitwa na wakati. Hivyo ili uweze kumpata mwanamke unayempenda kwa dhati basi unatakiwa kujifunza kutumia maneno yafuatayo; 1. Nipe makinikia ya moyo wako. 2. Naahidi kulipa mirahaba yako na kodi zote za mapenzi. 3. Sitakudanganya kiwango cha madini kilichoko kwenye mchanga wa madini ya mapenzi kama acacia. 4. Please usizuie contena la mchanga wa madini ya penzi langu kwenye bandari ya moyo wako. 5. Usiniundie kamati za marafiki zako kufanya uchunguzi wa makanikia ya upendo wangu. 6. Usinitangaze kuwa naiba utajiri wa mgodi wa moyo wako hadharini mbele ya vyombo vya habari. 7. Nitakuomba ukae kwenye meza ya mazungumzo ili uniruhusu kuchimba sukari ya moyo wako. 8. Usiwahusishe viongozi wastaafu ma X wako katika katika ombi langu sababu wengine watakuwa walikusainisha mikataba mibovu ikakuumi...

Mhalifu wa mtandaoni akamatwa Tanzania

Image
  Thabo Bester, ni raia wa Afrika Kusini aliyekuwa akisakwa kwa udi na uvumba kutokana na tuhuma nzito za ubakaji, wizi na mauaji, alizozifanya na baadaye kutoroka gerezani alikokuwa akitumikia kifungo cha maisha, huku watu wote wakiamini kwamba amekufa. Taarifa mpya ni kwamba, mtuhumiwa huyo amekamatwa na Jeshi la Polisi nchini Tanzania na sasa taratibu za kumrudisha nyumbani kwao, Afrika Kusini kwa hatua zaidi za kisheria zinaendelea huku ikielezwa kwamba amekamatiwa jijini Arusha. Taarifa za kipolisi, zinaeleza kwamba Thabo alikuwa na mchezo wa kuwatongoza wanawake Facebook, akiwaahidi kuwatafutia kazi au kuwaunganisha na kampuni za kimataifa za mitindo na kuishia kuwabaka na kuwaibia huku wengine akiwaua. Ni tuhuma hizo ndizo zilizosababisha akakamatwa nchini Afrika Kusini na baada ya kukutwa na hatia, alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani katika Gereza la Hloko jijini Bloemfontein, Mei 2022. Hata hivyo, katika mazingira yaliyojawa na utata, ilikuja kuelezwa kwamba jamaa huyo...

LORI LAUA BODABODA 10 KIJIWENI

Image
  Watu kadhaa wamepoteza maisha baada ya lori lililokuwa likisafirisha changarawe kupoteza mwelekeo na kugonga kundi la bodaboda waliokuwa wameegesha eneo lao (kijiweni) mjini Migori nchini Kenya. Tukio hilo la asubuhi ya Jumamosi - Aprili 8,2023 limeshuhudia umati mkubwa wa watu ukimiminika eneo la tukio ili kuwanusuru majeruhi na kuwakimbiza hospitalini kwa matibabu.  Kwa mujibu wa raia mmoja aliyeshuhudia na kuzungumza na runinga ya TV47, breki za lori hilo zilifeli na kuingia katika kundi hilo la bodaboda ambao walikuwa wanasubiri abiria.  Ajali hiyo imefanyika karibu na shule ya msingi ya Migori. Eneo la tukio lilikuwa limejaa damu na miili.  Vyuma pia vilikuwa vimetapakaa eneo hilo. Eneo la tukio linaripotiwa kuwa na zaidi ya miili kumi huku ambulansi na wazima moto kutoka kwa serikali ya kaunti ya Migori wakifika eneo la ajali hiyo.