MAFURIKO YAUA WATU 7
Watu 7 wamefariki dunia na wengine 21 hawana mahali pa kuishi kutokana na mto Talanda katika kijiji cha Talanda Kata ya Milepa wilayani Sumbawanga kujaa na kufurika katika makazi ya watu.
Mwenyekiti wa Kijiji ch Talanda Oscar Denya amesema waliofariki dunia ni wanaume watatu na wanawake wanne wote wa familia mbili tofauti.
Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Sixtus Mapunda akiwa ameongoza na wajumbe wa kamati ya USALAMA ya Wilaya ametoa Pole kwa maafa hayo na serikali imewahamisha wananchi wa Kaya 10 ambao nyumba zao zote zimesombwa na maji na kuanza kuwajengea nyumba sehemu nyingine.
Comments
Post a Comment