JELA MIAKA 20 KWAKUKUTWA NA PEMBE ZA NDOVU

 


Watu wanne wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 kwenda jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kukutwa na vipande vipande vya pembe za ndovu, kinyume cha sheria ya wanyama pori ya mwaka 2005 iliyofanyiwa wanawake mwaka 2016 wakiwa katika hatua za mauzo ya nyara hizo za serikali.


Hukumu hiyo imetolewa katika mahakama ya hakimu mkazi wa Mkoa wa Shinyanga na hakimu mkazi Yusuph Zahoro, baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili na kuwatia hatiani watakiwa wote wanne wa nyimbo na Kesi ya uhujumu uchumi namba 1 ya mwaka 2022.


Washitakiwa hao walikutwa na vipande 9 vya pembe za ndovu thamani ya milioni 6921 ambapo watakiwa walikamatwa wakiwa katika hatua za kuuza nyara hizo kata ya Solwa wilaya ya Shinyanga.


Waliohukumiwa kifungo cha miaka 20 jela ni Emanuel Shija Basu, Shija Kaswahili, Revocatus Mtara na Daud Ndizu ambao walitenda kosa hilo July 13 , 2022 baada ya kukutwa na nyara za serikali kinyume cha sheria.

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?