Vigezo AJIRA mpya za ualimu na afya 2023
SERIKALI imesema inatambua uwepo wa walimu katika shule za Msingi na Sekondari wanaojitolea hata hivyo imesisitiza itazingatia vigezo katika kutoa ajira mpya zilizotangazwa wiki iliyopita.
Waziri wa TAMISEMI, Angellah Kairuki ametaja vigezo vitakavyo zingatiwa kuwa ni pamoja na wale waliomaliza elimu mwaka 2015, masomo waliohitimu (Fizikia, Biolojia, Kemia, Lugha ya Kingereza na wataalamu wa ufundi katika maabara za sayansi).
Waziri Kairuki ametaka wananchi kutowalaumu viongozi hususani wabunge ikiwa watakosa nafasi hizo kwa kuwa utaratibu uliowekwa na Wizara ni wa huru na haki. “Hakutakuwa na nafasi ya upendeleo na mimi nitakuwa nafuatilia kwenye mfumo kuhakikisha wale tu wanaostahili wanaajiriwa,” amesema.
“Tutahakikisha zoezi hili linaenda kwa haki. Viongozi mnaonitumia ujumbe wa simu sita jibu sita angalia nani ni nani kwa kuwa mtu asiyemjua mtu atapata shida wanaoomba nafasi hizi waende kwenye mfumo.” Waziri Kairuki ametahadharisha kuwa viongozi watakaoenda kinyume wataadhibiwa ikiwa ni pamoja na kufunguliwa mashtaka ya jinai.
Kwa mujibu wa Waziri Wizara haina mfumo uliorasmi unaotambulika na kutumiwa kuwatambua walimu wanaojitolea. Tatizo hilo pia lipo katika vituo vya afya kote nchini. Waziri amesema Serikali inaandaa utaratibu mahususi wa kielektroniki kuwafuatilia walimu na watumishi wa afya wanaojitolea.
Amesema uwepo wa walimu wa kujitolea umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la upungufu wa walimu katika shule za Msingi na Sekondari.
Soma zaidi www.masshele.co.tz
Comments
Post a Comment