KWA KAULI HII YA HANS POPPE TAYARI WACHEZAJI 10 SIMBA SAFARI IMEWAKUTA
Klabu ya Simba imepanga kuwabakiza wachezaji 15 pekee kati ya 25 iliowasajili msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho (FA). Timu hiyo, inataka kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (Caf) watakayoshiriki mwakani. Wakati wakipanga kusajili na kuwaacha wachezaji hao, tayari baadhi ya nyota muhimu wa Simba wameshaanza kuaga kwenye timu hiyo akiwemo Abdi Banda ambaye mkataba wake umemalizika, wengine ni Jonas Mkude na Ibrahim Ajibu ambao wanaelezwa kuwa wanaweza kuondoka kwenye timu hiyo. Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, alisema kuwa bado hawajapokea rasmi ripoti ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mcameroon, Joseph Omog lakini tayari Kamati ya Utendaji ilikutana kufanya tathmini ya kikosi chao kwa ajili ya usajili. Hans Poppe alisema katika kikao hicho wameona wachezaji kumi ambao hawana mchango na kupanga kuwaondoa katika mipango yao ya msimu ujao wa ligi na michuano ya...