UGONJWA WA KUKOJOA DAMU (HAEMATURIA)
HAEMATURIA ni ugonjwa wa kukojoa damu
ambapo kwenye mkojo kunakuwepo chembechembe za damu nyekundu (Red blood cells).
Kukojoa damu ni dalili ya kuonyesha kuwa mtu anayekojoa ana
magonjwa katika mfumo wa mkojo kama vile magonjwa ya kichocho au magonjwa
mengine yanayoshambulia kibofu cha mkojo au kwenye figo.
SABABU
Magonjwa yanayoshambulia mfumo wa mkojo kama vile UTI, magonjwa
ya zinaa hasa kwa wanawake, vijidudu kama staphylococcus saprophyticus, mawe
kwenye figo (kidney stone) kuvimba kwa tezi zinazozalisha manii kwa wanaume
ambao umri umeenda yaani wazee.
Sababu nyingine ni kama kupata ajali na kuumia sehemu za mfumo
wa mkojo (trauma), kupata magonjwa kama kansa ya kibofu cha mkojo, hii
hutokea mara nyingi hasa vijijini ambapo watu wanacheza au
kuogelea kwenye madimbwi ya maji yasiyotembea.
Sababu zingine ni mtu kuugua magonjwa ya sickle cell
anemia na magonjwa mengine ya figo kama vile nephotic syndrome na mengine
mengi ambayo yanajulikana kwa kitaalamu na siyo rahisi kuyafafanua kwa
Kiswahili.
AINA
YA UGONJWA WA KUKOJOA DAMU
Kuna aina mbili za damu kutoka kwenye mkojo, moja ni ile
ambayo damu huchuruzika na kuonekana vizuri kwenye mkojo. Hii
hujulikana kama macroscopic haematuria au gross haematuria ambayo hutokea
kwa wagonjwa wa kichocho au waliopata ajali.
Nyingine ni ile inayoonekana kwa mbali na mara
nyingine huonekana wakati mgonjwa anapopimwa mkojo, aina hii hujulikana
kama microscopic haematuria.
JINSI YA KUGUNDUA TATIZO (diagnosis)
Mara nyingi tatizo la kukojoa damu hugundulika baada ya mgonjwa
kwenda hospitalini na kuonana na daktari na akachukua maelezo
yake vizuri na kuagiza mgonjwa akapime mkojo.
Kipimo cha Ultrasound pia husaidia kujua tatizo
linalosababisha mgonjwa akojoe damu.
Mashine ya X- ray husaidia
kugundua kama mgonjwa ana mawe kwenye figo. Kipimo kingine cha
kisasa ni CT scan hiki kina uhakika ila ni ghali sana na hupatikana
kwenye hospitali kubwa.
TIBA
Tiba ya uhakika ni kujua sababu
inayosababisha mgonjwa akojoe damu kama ni kichocho basi mgonjwa atapewa
dawa ya kichocho na kama ni UTI mgonjwa atapewa dawa husika na kama ni magonjwa
ya zinaa nayo yatatibiwa. Magonjwa mengine ni kama yale ya figo basi nayo
yakigundulika yatatibiwa.
USHAURI
Watoto wasichezee maji yaliyosimama hasa
kwenye mabwawa vijijini na mijini, wakigundulika kuwa walicheza basi haraka
wapelekwe hospitali kupimwa
Comments
Post a Comment