UMESIKIA HIKI ALICHOAMBIWA RAIS MAGUFULI,? A ---Z. IPO HAPA
Abdul Omar Nondo. *PONGEZI KWA MH.RAISI JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI*
Na
*Abdul Omar Nondo*.
Napenda kumpongeza Mh.Raisi kwa hatua alizochukua, na kwa namna alivyokasirishwa juu ya mapato makubwa ambayo tumekuwa tukiyapoteza.
Kampuni ya ACACIA ,ni kampuni ya uingereza ambayo viongozi wake wakuu ni *kelvin Dushnisky* Kama m/kiti,Bradly Gordon Kama *CEO* na imeanza kuwekeza tangu mwaka 1999,ikitambulika Kama BARRICKS GOLD COOPERATION LTD.kabla ya kubadilishwa jina tarehe 27.november 2014. ndio ikaitwa ACACIA ikimiliki mgodi wa Buzwagi na Bulyanhulu, baadaye north Mara,na tulawaki. hii ndio kampuni ya kimataifa ambayo imekuwa ikisafirisha mchanga tangu 1999.
Hivyo basi kwa ripoti ya kamati hiyo iliundwa kuchunguza kiwango cha madini katika makinikia (mchanga)chini ya DR MRUMA, niwazi nchi imekuwa ikiibiwa kwa muda saana na kwa muda mrefu saana,nakuamini kuwa TMAA (Tanzania minerals audit agency) /wakala wa serikali wa ukaguzi madini wamekuwa hawapo makini nakuishia kutoa ripoti ambazo zinamashaka ripoti yao ya 2011,february.
Lakini ripoti ya kamati na hotuba ya Mh. Raisi inatoa majibu na ujumbe mzito sio tuu kwa Tanzania tuu ila kwa nchi zote afrika namna gani mataifa makubwa na makampuni makubwa ya kimataifa yanayo binafsishiwa na kuwekeza katika sekta mbalimbali katika nchi zetu za ulimwengu wa tatu yanavyo didimiza nchi zetu kwa manufaa yao binafsi.
Katika kitabu cha festo mkenda *julius Nyerere's four ingredients for development*,mwalim anasema "foreign governments and multinational companies still lock Africa's potential as they syphon continent's wealth" kuwa mataifa ya kigeni ndio yanadidimiza Afrika.
Haya ni maneno ya Mwalimu, hii inaashiria dhahiri kuwa bado tuna mapambano makubwa ya kulinda rasilimali zetu kwa hali yote kwa maendeleo yetu.
Haya ni mapambano makubwa dhidi ya makampuni ya kimataifa ambayo yapo kwa faidi ya mataifa yao, haya ni mapambano yaliyokuwa yakipiganwa na waasisi wetu, JK Nyerere, kwame Nkurumah ,kamuzu banda, muamar Ghadaf, leopard Senghor, mnandi azikiwe, jomo Kenyatta ,leo Mh. Magufuli amekumbusha mapambano haya hivyo anahitaji kuungwa mkono.
Ukisoma kitabu kiitwacho "Tanzania under mwalimu Nyerere"cha Godfrey mwakikagile (2006).mwalimu anasema "condition which such private investers have in their minds is that the interprises into which they put their money should bring them Profit and they like countries whose policies they agree with for their economic interests" kwamba makampuni hayo yanafanya vitu kwa faida yao za kiuchumi na wanapenda nchi yenye Sheria na sera nyepesi ili wanufaike zaidi.
Katika hotuba ya Mh.Raisi Leo nimejifunza kuwa katika nchi yetu bado tuna watu wanaitwa *compradors*hawa ni watanzania ambao wanaweza kuwa ni viongozi,wanasiasa, wafanyabiashara,taasisi za serikali ambao wanasimama Kama mawakala wa kutetea na kuchunga maslahi ya makampuni ya kimataifa na maslahi yao binafsi kabla ya maslahi ya taifa lao.hawa baada ya huru walipigwa Vita Sana na mwalimu. Nchi hii ni yetu lazima ifike mahali wote katika masuala Kama haya tuwe wazalendo kwa maslahi mapana ya nchi yetu.na wala sio CCM, Chadema, ACT wazalendo, CUF, mfano, kabla ya mapinduzi ya China 1949, kulikuwa na civil kati wachina wenyewe 1921,kati ya *MAO TSETUNG*na *Chiang Kai Shek* lakini mwaka 1937 mjapani chini ya *General Hedek Tojo* aliivamia china,mao na Kai Shek waliungana, na kuondoa tofauti zao.(nimechomekea)
Hotuba ya leo ya Mh. Raisi imeonesha namna gani tunapaswa kuwa pamoja kwa maslahi mapana ya kitaifa, badala ya kuchukulia kila jambo katika sura ya kisiasa, mwalimu nyerere tarehe 16,oktoba 1997,akiwa afrika kusini, Capetown alitoa hotuba inayotambulika leo Kama "argue and don't shout" ukisoma hotuba hii utaelewa namna gani tunapaswa kuwa wamoja, namna gani ulaya wapo kwa maslahi yao,namna gani afrika imetengwa.
Hivyo basi muda sasa tuone namna gani tunaweza kupata kinu chetu (smelter/smelting plant).kwaniaba ya kuchenjua mchanga sisi wenyewe tunaweza katika sera ya madini ya 2009,imeeleza wazi kuwa katika (statement) kuwa serikali ijenge smelter.
Kwa taarifa ni kuwa uwezo wetu wa kuzalisha mchanga huo ni tani 60000,kwa mwaka na smelting plant inahitaji kuchenjua kwa mwaka tani 150000,kwa mwaka ambapo sisi uwezo wetu ni mdogo wa uzalishaji.
Kwa manufaa tuingie ubia na nchi ambazo huwa zikisafirisha mchanga huwa japani, jermani, mfano Congo, Zambia, tuwe na kinu chetu tuchenjue makinikia ili kufikia uwezo wa tani 150000 unaohitajika. Badala ya kupeleka nje.
Au tujenge kinu chetu alafu tuwe tuna import /ingiza mchanga wa nchi jirani zenye madini hayo.
Hapa tutakuwa tumeepuka unyonyaji mkubwa unaofanywa na nchi za kigeni pia makampuni ya kimataifa.
Hongera Mh.Raisi kwa uzalendo wa hali ya Juu.
Imetolewa na
Abdul Omar Nondo.
0659366125
0762082783.
Comments
Post a Comment