TAASISI YA KUPAMBANA NA RUSHWA -UDSM(CEOAC).YAPATA UONGOZI MPYA.

TAASISI YA KUPAMBANA NA RUSHWA -UDSM(CEOAC).YAPATA UONGOZI MPYA.
          
Taasisi ya kuzuia na kupambana rushwa chuo kikuu cha Daresaalam yaani "combined Efforts Organization against corruption"(CEOAC-UDSM), tarehe 28/05/2017,imefanya uchaguzi wake na kupata viongozi wake katika nafasi ya Raisi ,makamu, ukatibu, muweka hazina,kama inavyoeleza katika katiba yao ambapo uraisi alishinda Abdul Omar Nondo, na umakam alishinda Veronika Kipingu, katibu mrisho Rashidi, P.R.O Gikaro Bernard na bulahya maiko, system admin. Benedictor eliji, Mhasibu, masaka Omary.


Akiongea na MASSHELE BLOG, Abdul Nondo, raisi mteule alishukuru uongozi uliopita kwa kutua mzigo wa majukumu kwao na akaahidi, kufanya Kazi na uongozi wake kikamilifu, " nashukuru uongozi uliopita ni muda sasa kufanya taasisi hii kukua ndani na nje ya jumuiya yetu ya chuo,sababu lengo kubwa ni kuwa na jamii itakayotambua umuhimu wao katika mapambano ya rushwa, jamii itakayokasirishwa juu ya vitendo vya rushwa, pia kutoa nafasi kwa wanafunzi na jumuiya kutoa mawazo yao njia gani stahiki za kutokomeza rushwa, pia kupokea taarifa na kufanya uchunguzi juu ya tendo lolote la rushwa na kuchukua hatua stahiki,kutengeneza jamii ya kizalendo na hofu juu ya madhara ya rushwa, alisema Abdul Nondo. 

Pia aliendelea kwa kusema kuwa Chuo kikuu ndio viongozi wanazaliwa kwa kasi lazima tufahamu wote madhara ya rushwa, tukemee na tutoe taarifa muda wowote tukianza mapambano dhidi ya petty Corruption (rushwa ndogo ndogo) katika jamii yetu ni njia rahisi ya kuwa na hofu hata dhidi ya grand corruption (rushwa kubwa kubwa), hivyo tutakuwa na viongozi na jamii yenye hofu juu ya rushwa hapo baadaye,alisema Abdul Nondo. 

Kuhusu usajili wa wanachama wapya alisema, "sasa hatujakabidhiwa mikoba, tukikabidhiwa na kuonana na mlezi wetu Dr.Jingu , na takukuru wilaya ya kinondoni na makao makuu, tutatoa utaratibu na kuwatangazia wanafunzi juu ya usajili kwa wanachama wapya watakao shiriki kikamilifu na baadaye kupewa kitambulisho, na mwisho wa uongozi cheti cha uanachama baada ya kutumikia kwa muda wa mwaka mmoja kama mwanachama, alisema Abdul Nondo.

Aliongeza sema ,tutakuwa tukifanya makongamano mbali mbali, na kutoa vipeperushi vya elimu juu ya athari za rushwa, pia tutajikita kutembelea shule za sekondari kuongea na wanafunzi juu ya athari za rushwa, inaongozwa kwa mujibu wa katiba, na taratibu zote, pia hatutafumbia macho tendo lolote la rushwa, ndani ya jumuiya yetu ya Chuo au hata nje ya chuo Chetu kwa kushinikiza serikali kupitia PCCB ichukue hatua, rushwa zinazofanyika ndani ya jumuiya yetu ya chuo tutazishughulikia sisi kwa mujibu wa Sheria na taratibu baada ya kupata taarifa husika. 

Changamoto kubwa aliyoisema, raisi mteule wa taasisi hiyo ni ukosefu wa ofisi, jambo ambalo lipo linashughulikiwa kikamilifu, na tutapata ongea zaidi na mlezi wetu DR. JINGU juu ya tatizo hili, hii taasisi ni nyeti, unaweza kuwa na taarifa za siri, ni hatari kuziweka chumbani, alisema Abdul Nondo.

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?