Posts

Showing posts from September, 2016

Bodi ya mikopo mchana huu

Image
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu haitozi riba – Mwaisobwa  8:00 AM     ELIMU, KITAIFA    Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisobwa amesema Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu pamoja na kwamba inatoa mikopo kwa wanafunzi haitozi riba katika marejesho ya mkopo huo. Akizungumza Jijini Dar es salaam katika Kipengele kinachoitwa KIKAANGONI cha EATV , Mwaisobwa amesema kwamba Bodi ya Mikopo inachokifanya kwa walipaji ni kutoza tozo ya kulinga thamani ya mkopo ambao mnufaika alichukua. 'Tunatoza kiwango cha asilimia 6% ya tozo ya kulinda thamani ya mkopo kiwango ambacho ni tofauti kabisa na riba, ukiangalia benki kwa sasa hivi kuna ambazo zinatoza zinatoza zaidi ya asilimia 20 hivyo sisi kazi yetu tunasaidia kutoa elimu na siyo kunufaika zaidi” Amesema Mwaisobwa. Aidha Mwaisobwa amesesitiza kwamba kwa wote ambao walichukua mikopo na wanajificha kukwepa kulipa, watalipa tuu kwa kuwa uhakiki kwa sasa huivi unafanyika ...

KWANINI YANGA HAWATOSALIMIKA KWA SIMBA?

Image
Kwanini Yanga hawatasalimika mbele ya Simba, hizi hapa sababu kadhaa kutoka kwa Omog Kwa mwendo iliyonao Simba ya sasa, ni wazi kwamba usitie mguu maana utavunjika tu! Hii ni kutokana na kasi ya ajabu iliyoanza nayo msimu huu, ikiwa ndiyo timu pekee iliyokusanya pointi nyingi zaidi katika mechi tano za mwanzo. Simba iko kileleni na pointi 13, ikiwa imedondosha pointi mbili tu huku Azam FC na Yanga zikifuatia kwa pointi 10 kila moja, lakini Yanga ina mchezo mkononi. Hata hivyo, Simba imefichua sababu kuu nne ambazo zimeifikisha hapo, ambazo inasema ndizo hizohizo zitakazoiua Yanga wiki ijayo kama ilivyokuwa kwa Azam wikiendi iliyopita walipoichapa bao 1-0. Kabla ya hapo, tayari walikuwa wameshinda mechi dhidi ya Ndanda, Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar huku wakitoa suluhu na maafande wa JKT Ruvu. Kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja ‘Mia Mia’ ametamba kasi yao ni hiyohiyo kwa mechi zinazokuja ikiwemo ya Oktoba Mosi mwaka huu dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga kwenye Uwanja wa T...

UJUE MKANDA WA JESHI

Image
By Dk Emanuel : MKANDA WA JESHI NI NINI ?     Mkanda wa jeshi (shingles) ni jina linalotumika mitaani kuutaja ugonjwa unaoshambulia ngozi na kujenga tabaka la vijipele vikubwa venye majimaji ambavyo mara nyingi hukamata upande mmoja wa mwili . Ingawa vijipele vya mkanada wa jeshi vinaweza kutokea sehemu yo yote ya mwili , mara nyingi hupenda kuota kifuani , shingoni , usoni , mgongoni na mikononi . Vijipele hivi hukaa juu ya ngozi kwa muda wa wastani wa wiki mbili hadi sita kisha hupotea . Vipele vya mkanda wa jeshi huambatana na maumivu makali na kusikia ngozi kuwaka moto. Aghalab ugonjwa huu humrudia mtu zaidi ya mara moja . Mkanda wa jeshi huwapata zaidi watu wenye umri mkubwa , zaidi ya miaka 50, utafiti ukionyesha kuwa zaid ya nusu ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 80 hupatwa na mkanda wa jeshi . Vilevile huwapata zaidi watu waliopatwa na magonjwa yanayopungu...

NGOMA MPYA YA DIAMOND( salome)

ingia hapa kupakua ngoma mpya ya salome , ( traditional) aliyo imba diamond platinum, nime kuwekea hapa mtu wangu wa muhimu ,  click here ku downlodge >>> > https :// mkito .com /s ong/13465   pia tangaza nasi  piga 0766605392

TAMBUA SIKU ZA HATARI

Image
By docta EM ANUEL : ZITAMBUE SIKU ZA HATARI ZA KUSHIKA MIMBA{ NAJIBU MASWALI YA WENGI NA MMOJA WA MDAU WANGU KUTOKA KATIKA POST ILIYOPITA NAONA WENGI HAWAKUELEWA VYEMA ILA KWA SASA NIMEFAFANUA VYEMA KABISA} Nimeamua kuandika makala hii ili kujibu swali la moja wa mdau wa Wangu mmoja ambaye ameuliza kwamba, anahitaji kushika mimba na je, kwa mfano mwezi huu alianza period yake tarehe 17 Juni, ni zipi siku zake za kushika mimba? Ndugu mdau kwanza kabisa nachukua nafasi hii kukuomba samahani kwa kuchelewa kujibu swali lako. Pengine ninapoandika makala hii utakuwa tayari umeshashika mimba, basi kama ni hivyo hakuna tabu bali natumaini swali lako litakuwa limewasaidia wengine ambao pengine wana tatizo kama halo. Pia umeualiza je, ukitaka mtoto wa kike ufanyeje? Nachukua nafasi hii kwanza kujibu swali lako la kwanza kabla sijaenda kwenye swali lako la pili. Kwani kuelewa vyema swali la kwanza kutasaidia kuelewa swali la pili pia. Inafaa tufahamu kuwa ili kuweza kujua ni siku zipi za mwezi mw...

MASHELE BLOG: MPYA:HII HAPA LIST YA VYUO VILIVYOTOA SELECTION YA...

MASHELE  BLOG: MPYA:HII HAPA LIST YA VYUO VILIVYOTOA SELECTION YA... : Habari yako , Masshele blog , tumedhamiria kuwapa vitu roho inapenda hap tembelea blog hii mara kwa mara upate habari za uhakika

STAA TANZANIA AKIRI SIMBA IPO VIZURI

Image
Kiungo wa Azam FC, Himid Mao, amekubali yaishe baada ya kusema kuwa kikosi cha Simba msimu huu kipo vizuri ukilinganisha na msimu uliopita. Mao aliyasema hayo baada ya juzi Jumamosi Simba kuitembezea kichapo cha bao 1-0 Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Championi Jumatatu, Mao alisema kuwa msimu huu kikosi cha Simba kipo vizuri na hiyo ni kutokana na usajili waliofanya. “Tulipambana sana uwanjani lakini mwisho wa siku Simba ndiyo walioibuka na ushindi, nawapongeza kwa hilo lakini pia nimegundua kuwa kikosi chao safari hii kipo vizuri. “Hata hivyo tumekipokea kipigo hicho kwa mikono miwili, upungufu wote uliojitokeza katika mchezo huo, najua kocha atakuwa ameuona na ataufanyia kazi ili kuhakikisha tunafanya vizuri katika mechi zetu nyingine kwa sababu kupoteza mchezo huo siyo kwamba ligi imeisha, tunatakiwa kushinda michezo yetu mingine iliyobakia,” alisema Mao.

KAMA UTANI HAJIB HATAKUWEPO KWENYE HI MECHI

Image
Ajibu kukaa nje mechi ya Majimaji Jumamosi, sababu zimetajwa na benchi la ufundi. Kuna kila dalili, Simba itataka kumlinda mchezaji wake Ibrahim Ajibu asipate kadi ya tatu ya njano. Ajibu ana kadi mbili za njano na benchi la ufundi la Simba, linaweza kujithatiti asijeze mechi ijayo dhidi ya Majimaji ili kuhakikisha anaivaa Yanga Oktoba Mosi. “Kweli Ajibu ana kadi mbili za  njano na sisi watu wa benchi la ufundi tumeliona hili. Lakini bado utabaki kuwa uamuzi wa kocha mwenyewe (Omog),” kilieleza chanzo. Simba inaivaa Majimaji Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Baada ya hapo Simba watakuwa kwenye maandalizi ya mechi yao dhidi ya watani wao Yanga, Jumapili inayofuatia. Hivyo suala la tahadhari linaweza kufanya Ajibu akose mechi hiyo ili kuhakikisha anakuwepo kusaidia safu ya ushambulizi dhidi ya Yanga.

HUU NDIO UKWELI KUHUSU KIFO CHA JOHN CENA

Image
Katika siku za hivi karibuni mcheza mieleka maarufu John Felix Anthony Cena amekuwa moja ya wahanga wa mitandao ya kijamii baada ya kuzushiwa kifo. Habari zimesambaa kwa wingi mtandaoni kuwa Cena amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kupata ajali ya gari,vyanzo vingine vinadai Cena amefariki baada ya kuumia kichwani alipokuwa mazoezini na mcheza mieleka mwingine maarufu Dwayne Johnson(The Rock) Uongozi mzima wa WWE umekanusha habari hizo na kuziita habari zisizokuwa na tija zaidi ya kuzitafutia umaarufu baadhi ya media.

Wanafunzi wa vyuo vikuu kuendelea kulipwa 8500

Image
Wanafunzi Vyuo vikuu kuendelea kulipwa Sh8,500/-  12:25 AM     ELIMU, KITAIFA    Ads by Kwanza   Serikali imekataa kuongeza fedha za kujikimu kwa wanafunzi wa elimu ya juu wanaopatiwa mikopo na Serikali kutoka Sh8,500 hadi kufikia Sh10,000 kwa siku. Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Stella Manyanya amelieleza Bunge kuwa kiwango hicho kitaendelea hadi utakapofanyika utafiti baada ya miaka miwili. Manyanya alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum,  Zainabu Katimba (CCM), aliyetaka kujua kama Serikali itakuwa tayari kuongeza fedha kwa wanafunzi hadi kufikia Sh 10,000 kwa madai gharama za maisha zimepanda. Amesema bodi ya mikopo ilifanya ongezeko la fedha za kujikimu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa Sh1,000 kutoka Sh7,500 hadi kufikia 8,500 katika mwaka 2015/16. “Ongezeko hilo haliendani na kasi ya mfumuko wa bei uliorekodiwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kutoka asilimia 4.2 Februari 2015 hadi kufikia asilimia 5.6 Februari 2016,” amesema Katimba. Naibu waziri amesema ...

LIST OF NAMES BACHELOR FIRST ROUND SELECTED 2016/ MARIAN UNIVERSITY COLLEGE

Image
click here to see the list  your name is here plix click to see 

V

MGANDAMIZO MKUBWA WA DAMU

Mgandamizo wa juu wa Damu Category: Makala mpya za afya Published on Saturday, 05 December 2015 12:45 Written by Afya Bora Hits: 111 inShare Na Dk Mkweli, huu ni ugonjwa unaosababishwa na kuongezeka kwa msukumo wa damu kwenye mishipa ya ateri na hivyo kuufanya moyo hufanye kazi zaidi ili uweze kusukuma damu.   Kwa kawaida msukumo wa damu hutegemea wakati misuli ya maumivu ya kichwa hasa sehemu ya nyuma ya kichwa kupoteza uwezo wa macho kuona, kupoteza fahamu.      Umri mkubwa husababisha misuli ya moyo kulegea na kushindwa kufanua kazi na matumizi ya vyakula vyenye mafuta kwa wingi. Kwa kutumia tiba mbadala nimefanikiwa kuwa tibu baadhi ya watu waliokuwa na matatizo haya.   Cheti changu nilichopewa na mkemia wa serikali pamoja na wizara ya afya baada ya kupeleka dawa zangu kwa uchunguzi imekua chachu ya kuaminika na kuonyesha wagonjwa mbali mbali.   Magonjwa haya husababisha vifo vya ghafla, tatizo wenye magonjwa makubwa kama haya ndo wale wasioamini tiba mbadala na matumi...

TEZI DUME

Hii ni tezi ya wanaume yenye sifa zifuatazo. ~Ina umbo km yai(oval shape) ~Ina ukubwa wenye vipimo hivi, upana 4cm na unene 3cm ingawaje hivi vipimo vinatofautiana kwa kila mwanaume.  ~Tezi hii ipo inazunguka shingo ya kibofu cha mkojo na kuzunguka mrija unaopeleka mkojo nje(urethra) ~Tezi hii hua yenye ukubwa wa kawaida lakini huongezeka ukubwa kadri ya umri. ~Tezi hii hutengeneza majimaji yenye rutuba ya mbegu za kiume(shahawa) SEHEMU KUU ZA TEZI YA KIUME 1.PERIPHERAL ZONE(SEHEMU YA NJE) ~Hii ni sehemu ya nje ya tezi ambayo madakari wengi hutumia hii tezi kubaina kama kuna tatizo kwenye tezi kwani ni virahisi kiugusa km daktari akiingiza ikiingiza index fingure(kidole cha kusontea) kwenye njia ya haja kubwa. Kukua kwa sehemu hii hakuwezi kuathiri utokaji wa mkojo. 2. TRANSITIONAL ZONE(SEHEMU YA KATI) ~ Hii ni sehemu ya tezi ambayo ikikua yani ikiongezeka ukubwa tunasema KUVIMBA KWA TEZI TUME kitalamu BENIGN PROSTATIC HYPERPLASIA (BPH) kuna uwezekano mkubwa wa tezi dume iliyovimb...

About ulcers

Makala za Afya PichaMawasiliano Magonjwa Tunayotibu SHINIKIZO LA DAMU KUONGEZA CD4 MWILINI MOYO MPANA KUKOJOA KITANDANI KISUKARI (DIABETES) FIGO MALARIA (TYPHOD) PUMU (ASTHMA) ALEJI (ALEGEY) KIFAFA VIDONDA VYA TUMBO (ULCER) UPELE NA CHUNUSI MKOJO MCHAFU (U.T.I) MAGONJWA YA ZINAA (S.T.D) NA KUONGEZA CD 4 MWILINI FANGASI AINA ZOTE (FUNG) MIGUU, KIUNO NA MGONGO. JINO BILA KUNG'OA UVIMBE TUMBONI (FIBROID) KUPUNGUZA UNENE NA UZITO PAMOJA NA KUONDOA SUMU MWILINI MARADHI YA MACHO NGIRI AINA ZOTE. TUMBO LA CHANGO NA UZAZI KWA AKINA MAMA KUPOOZA (STROCK) TEZI DUME ( PROSTATE GLAND ) Vidonda vya tumbo Category: Makala mpya za afya Published on Saturday, 05 December 2015 12:45 Written by Afya Bora Hits: 102 inShare Na  Dk Mkweli kutoka kliniki ya Mkweli Herbal & Clinic (Afya bora clinic). Makala hii nakuelezea kuhusu vidonda vya tumbo ambao unawatesa  watanzania na kushindwa kujua namna ya kupona huku wengine wakuhusisha na imani za kishirikina   Vidonda vya tumbo vinavyotokea...

UGANDA WAFUZU AFKONI

Image
Timu ya taifa ya Uganda, The Cranes imefuzu kucheza Kombe la Mataifa Afrika baada ya kuichapa Comoro kwa bao 1-0. Ushindi huo umeifanya Uganda kufikisha pointi 13 sawa na vinara wa kundi D, Burkina Faso na kuwaacha Comoro na Botswana wakirejea nyumbani kama ilivyo kwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Bao la Uganda limefungwa na Farouk Miya mbele ya mashabiki kibao wa Uganda jijini Kampala leo. Michuano hiyo itafanyika mwakani nchini Gabon. Uganda inafuzu kucheza Kombe la Mataifa Afrika ambalo ilishiriki mara ya mwisho mwaka 1978 ikiwa chini ya Kocha Mserbia, Sredejovic Milutin 'Micho' aliyewahi kuinoa Yanga. Kufuzu kwa Uganda, huenda kutakuwa changamoto kwa Tanzania kwamba kuna mambo yanayotakiwa kupunguzwa kama ubinafsi na zaidi kuangalia maendeleo kwa ajili ya taifa.

TANGAZOOO!! JE WEWE NI MHITIMU WA KIDATO CHA NNE

Image
JE WEWE NI MHITIMU WA KIDATO CHA NNE NA UNATAKA MAFANIKIO?  kama jibu ni ndio  CHUO CHA UALIMU NA BIASHARA MOUNT SINAI kina kutangazia nafasi za masomo CHUO CHA UALIMU MOUNT SINAI KILICHOPO ENEO LA BUNJU "A"  MANISPAA YA KINONDONI DAR ES SALAAM NI MIONGONI MWA VYUO VINANE NCHINI TANZANIA VILIVYO TEULIWA NA SERIKALI KUPITIA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI KUTOA MAFUNZO YA KOZI  ZA UALIMU STASHAHADA YA YA ELIMU YA UALIMU KATIKA SHULE ZA MSINGI (diploma in primary education SIFA ZA MWOMBAJI _Awe amemaliza kidato cha nne _Awe na cheti cha ualimu wa shule za msingi(GD) muda wa mafunzo ni miaka miwili 2.STASHAHADA YA ELIMU YA UALIMU WA SHULE ZA MSINGI ( diploma in primary education _ pre service ) Sifa za mwombaji _Awe amemaliza kidato cha nne _Awe na ufaulu usiopungua D nne katika masomo manne MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA MITATU   mawasiliano 0766605392 and 0673824667 @@@@@@@@@@ KOZI ZA BIASHARA 1_certificate in Business Administration 2_certific...

Taarifa kuhusu uteuzi wa pili na kuongezwa muda wa kutuma maombi NACTE

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA PILI NA KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA CHETI NA DIPLOMA KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017Date Posted: 2nd September 2016 17:20:21 Posted By: NACTE   Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi za cheti na diploma na Umma kwa ujumla kuwa lilifunga dirisha la maombi mnamo tarehe 13 Agosti 2016 ili kuruhusu uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa kozi hizo. Uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa cheti na diploma ulitarajiwa kutangazwa tarehe 31 Agosti 2016 lakini kwa sababu zilizo nje wa uwezo wetu umesogezwa mbele mpaka tarehe 5 Septemba 2016. Baraza pia linapenda kutoa taarifa  kuwa Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) kwa waombaji wa cheti na diploma utafunguliwa tena tarehe 5 Septemba 2016 hadi tarehe 15 Septemba 2016 ili kujaza nafasi za udahili zitakazokuwa wazi baada ya uchaguzi wa awamu ya pili. Hatua hii itawezesha kuruhusu machaguo mapya kwa wale ambao hawakuchaguliwa katika ...

ATOLEWA MACHO KWA USHIRIKINA

Image
Kijana mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa jimbo la kaskazin magharibi mwa Nigeria la Bauchi anasema kuwa macho yake yalitolewa na watu waliotaka kuyatumia kwa ajili ya sababu za ushirikina. Viungo vya mwili wa binadamu ambavyo hutumiwa katika imani za uchawi ama kwa ajili ya mazingaombwe hutolea kutoka kwa watoto nchini Nigeria, na mara nyingi watu wazima huwa hawaathiriwi. Hussain Emmanuel, ambaye kwa sasa anatibiwa katika hospitali ya mji wa Bauchi, anasema shabulio lililomuacha bila uwezo wa kuona tena, lilitokea wiki mbili zilizopita katika kijiji kilichoko eneo lisiloweza kufikiwa kwa urahisi la Tafawa Balewa. Anasema alirubuniwa na watu wawili katika kijij cha Marti kilichopo karibu na mto waliomshawishi aende kuogelea. Bw Emmanuel, ambaye hufanya kazi yake ya kibinafsi kama fundi wa magari, anasema alikuwa pamoja na watu hao wawili kwasababu mmoja wao alimuahidi kumpa kazi kusini mwa Nigeria. Lakini walipokwenda mtoni walimshabulia, wakataka kumnyongana na mnyororona shingoni ...

DU! Kumbe MUGABE alisha wahi kufa na kufufuka!!

Image
Rais Mugabe amesema alikuwa Dubai kwa masuala ya kifamilia Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amepuuzilia mbali taarifa za hivi karibu za uvumi juu ya afya yake, kwa kutoa mzaha kwamba alikufa na akafufuka. Akionekana mwenye furaha, Mugabe mwenye umri wa 92, aliyasema hayo alipokuwa akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Harare akitokea nje ya nchi. Taarifa ya safari yake ilisema kuwa ndege yake ilikuwa ikielekea mashariki mwa Asia, na kwamba badala yake ilikwenda Dubai. Bw Mugabe alisema kuwa alikwenda huko kwa masuala ya kifamilia. Mnamo mwezi Mei, Mke wa Mugabe, Grace, alisema kuwa mumewe ataongoza nchi hata akiwa kaburini. Taarifa za uvumi kuhusu safari zake za ndege na nyinginezo, zilisababisha kuenea kwa tetesi kwamba afya ya Bw Mugabe ilikuwa mbaya na kwamba alikwenda Dubai kwa matibabu ama hata alikuwa tayari amepoteza maisha. Tovuti ya Gazeti linalochapishwa kila siku la Southern Daily, ilituma makala yenye kichwa cha habari "Robert Mugabe anauwa kiharusi, Mnangagwa sasa ndi...

Wallahi dunia imeisha Angalia ANACHO FANYA HUYU ASKOFU

Image
Askofu mmoja wa kanisa la kianglikana nchini Uingereza amekuwa wa kwanza kutangaza hadharani kuwa anashiriki mapenzi ya jinsia moja na sasa yuko kwenye uhusiano. Kasisi Nicholas Chamberlain, amesema kuwa walioshiriki katika mchakato wa kumteua mwaka uliopita walialewa fika mwelekeo wake wa jinsia. ''Watu wanajua nashiriki mapenzi ya jinsia moja, lakini si kitu cha kwanza nachoweza kumwambia yeyote. Jinsia ni sehemu ya yule niliye, lakini ni kazi yangu ya kitume ambayo ninataka kuiangazia ." Nicholas Chamberlain anasema hata hivyo anafuata kanuni za kanisa zinazosema kuwa haruhusiwi kuoa. Msemaji wa kanisa la England amesema: "Nicholas hajamkera yeyote na amekua wazi na mkweli ukiuliza. Suala lake si la siri, ingawa ni la kibinafsi kama ilivyo kwa wale walio katika mahusiano ya kimapenzi ." Inadhaniwa kuwa hakuna askofu yeyote anayehudumu aliyewahi kutangaza hadharani msimamo wake wa kingono. Kanisa la kianglikana kote duniani limegawanyika sana miaka ya hi...

UGONJWA WA UTI

Image
UTI ni ugonjwa ambao unasumbua watu wengi; watoto, vijana na watu wazima. UTI ni kifupisho cha Urinary Tract Infection. Huu ni ugonjwa ambao hushambulia figo (kidneys); ureters; ambayo ni mirija inayounganisha figo na kibofu cha mkojo, kibofu cha mkojo (bladder) na urethra; sehemu inayotoa mkojo toka kwenye kibofu cha mkojo hadi nje ya mwili. Kwa kifupu ugonjwa wa UTI hushambulia viungo vinavyohusika katika kupitisha mkojo kabla haujatoka nje ya mwili. Hebu tuvitazame viungo hivi kabla ya kueleza chanzo cha ugonjwa na tiba ya UTI baadaye hapa chini. Kuelewa vizuri tunachokizungumzia hapa tazama picha ya viungo hivi na kwa kifupi hapa tutatoa maelezo ya picha hiyo. Figo ni viungo viwili vilivyopo kimoja kila upande wa uti wa mgongo eneo la kiunoni. Figo hufanya shughuli nyingi katika mwili wa binadamu ikiwepo ya kutoa uchafu na maji ya ziada katika damu, na huvitoa vitu hivi kama mkojo. Kwa sababu hii, figo ni muhimu sana katika kuweka msukumo wa damu kwenye kiwango kizuri. Figo p...

PEPO PUNDA

Na.Mwantumu Jongo Pepopunda ni ugonjwa wa hatari unaoambukiza na bacteria ambao huingia mwilini kupitia kwenye kidonda au jeraha .Ugonjwa huu huwapata watu wa rika zote .chanjo ya pepopunda kwa wanawake kila mwanamke kuanzia umri wa miaka kumi na tano na arobaini na nne ni muhimu akamilishe chanjo dhidi ya pepopunda . Katika sehemu nyingi duniani wanawake hujifungua katika mazingira machafu hii inamuweka mama na mtoto katika hali ya kupata ugonjwa wa pepopunda ambao huuua watoto wachanga wengi kama mama hakupata chanjo ya pepopunda mtoto azaliwaye ni rahisi kuupata ugonjwa huu. Vijidudu vya ugonjwa wa pepopunda huzaliana kwenye majiraha machafu hii inaweza kutokea ikiwa kiwembe kisu kichafu kitatumika kukatia kitovu cha mtoto au kitu chochote kichafu kikiwekwa kwenye kitovu cha mtoto mchanga .kitu chochote kinachotumika kukatia kitovu cha mtoto ni sharti kwanza kioshwe au kiunguzwe kwenye moto na baadae kuachwa kipoe. Wanawake wote wanaofikia umri wa kuzaa wapate chanjo dhidi ya pep...