STAA TANZANIA AKIRI SIMBA IPO VIZURI

Kiungo wa Azam FC, Himid Mao, amekubali yaishe baada ya kusema kuwa kikosi cha Simba msimu huu kipo vizuri ukilinganisha na msimu uliopita. Mao aliyasema hayo baada ya juzi Jumamosi Simba kuitembezea kichapo cha bao 1-0 Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Championi Jumatatu, Mao alisema kuwa msimu huu kikosi cha Simba kipo vizuri na hiyo ni kutokana na usajili waliofanya. “Tulipambana sana uwanjani lakini mwisho wa siku Simba ndiyo walioibuka na ushindi, nawapongeza kwa hilo lakini pia nimegundua kuwa kikosi chao safari hii kipo vizuri. “Hata hivyo tumekipokea kipigo hicho kwa mikono miwili, upungufu wote uliojitokeza katika mchezo huo, najua kocha atakuwa ameuona na ataufanyia kazi ili kuhakikisha tunafanya vizuri katika mechi zetu nyingine kwa sababu kupoteza mchezo huo siyo kwamba ligi imeisha, tunatakiwa kushinda michezo yetu mingine iliyobakia,” alisema Mao.

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?