Bodi ya mikopo mchana huu

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu haitozi riba – Mwaisobwa  8:00 AM     ELIMU, KITAIFA    Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisobwa amesema Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu pamoja na kwamba inatoa mikopo kwa wanafunzi haitozi riba katika marejesho ya mkopo huo. Akizungumza Jijini Dar es salaam katika Kipengele kinachoitwa KIKAANGONI cha EATV , Mwaisobwa amesema kwamba Bodi ya Mikopo inachokifanya kwa walipaji ni kutoza tozo ya kulinga thamani ya mkopo ambao mnufaika alichukua. 'Tunatoza kiwango cha asilimia 6% ya tozo ya kulinda thamani ya mkopo kiwango ambacho ni tofauti kabisa na riba, ukiangalia benki kwa sasa hivi kuna ambazo zinatoza zinatoza zaidi ya asilimia 20 hivyo sisi kazi yetu tunasaidia kutoa elimu na siyo kunufaika zaidi” Amesema Mwaisobwa. Aidha Mwaisobwa amesesitiza kwamba kwa wote ambao walichukua mikopo na wanajificha kukwepa kulipa, watalipa tuu kwa kuwa uhakiki kwa sasa huivi unafanyika katika maeneo mbalimbali na wakibainika penati ya asilimia 10 itawahusu wote wanaokwepa ila kwa wanaojitokeza kulipa kwa hiari watatozwa asilimia 8% ya pato lao kwa mwezi. Pamoja na hayo Bodi hiyo imewataka wanufaika wa mikopo hiyo kutambua kwamba fedha zinazotakiwa kulipwa ni zote kuanzia za chakula, ada pamoja na fedha za mafunzo kwa vitendo. Weka Mao

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?