Taarifa kuhusu uteuzi wa pili na kuongezwa muda wa kutuma maombi NACTE

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA PILI NA KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA CHETI NA DIPLOMA KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017Date Posted: 2nd September 2016 17:20:21 Posted By: NACTE   Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi za cheti na diploma na Umma kwa ujumla kuwa lilifunga dirisha la maombi mnamo tarehe 13 Agosti 2016 ili kuruhusu uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa kozi hizo. Uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa cheti na diploma ulitarajiwa kutangazwa tarehe 31 Agosti 2016 lakini kwa sababu zilizo nje wa uwezo wetu umesogezwa mbele mpaka tarehe 5 Septemba 2016. Baraza pia linapenda kutoa taarifa  kuwa Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) kwa waombaji wa cheti na diploma utafunguliwa tena tarehe 5 Septemba 2016 hadi tarehe 15 Septemba 2016 ili kujaza nafasi za udahili zitakazokuwa wazi baada ya uchaguzi wa awamu ya pili. Hatua hii itawezesha kuruhusu machaguo mapya kwa wale ambao hawakuchaguliwa katika kozi walizoomba pamoja na  kuruhusu waombaji wapya ambao kwa njia moja au nyingine hawakuomba udahili hapo awali.   Baraza linaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kutokana na mabadiliko hayo.   Imetolewa na Ofisi ya Katibu Mtendaji NACTE Tarehe: 02 September, 2016

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?