MAANA YA KITABU NA UTATA WAKE
Kwa mujibu wa Neil Fraistal (1985), wanafafanua kuwa kitabu ni makala iliyoandikwa kisanaa na makala hii inaweza kuzalishwa na mtu yoyote yule mwenye uwezo wa kufanya hivyo. Tunaona fasili hii inajikita katika swala la sanaa na kufanya kitabu kiwe kipana zaidi kwani swala la sanaa ni pan asana na mtaalamu huyu hafafanui ni sanaa ipi. Halikadhalika, TUKI (2014), wanafasili kitabu ni maandishi yaliyowekwa pamoja katika kurasa zilizoandikwa kwa mkono au zilizopigwa chapa na kupangwa kwa utaratibu maalumu na kutiwa jalada. Tunaona fasili hii inajikita katika kurasa kuelezea maana ya kitabu huku haiweki wazi utaratibu maalumu ambao kitabu inabidi kiwe nao. Pia Kamusi pevu ya Kiswahili (2016) wakifafanua maana ya kitabu wanaeleza kuwa ni kurasa zenye maandishi zilizofungwa pamoja kwa utaratibu. Pia fasili hii inajikita katika kuelezea utaratibu maalumu na kurasa lakini pia haiweki wazi huo utaratibu maalumu ni upi. Kwa mujibu wa Oxford Advanced Leaners Dictionary (2012), wa...