Nagona Nagona ni riwaya fupi ya kifalsafa na kibaadausasa inayoibua kira kuhusu falsafa na maana ya uhai, maisha, dhamira na hata kira yenyewe. Mhusika kiini wa novela hii anajikuta katika mazingira ya ajabuajabu katika nyakati tofauti tofauti. Si rahisi kubaini iwapo ni maono, njozi, kra ama matendo halisi, pengine ni vyote kwa pamoja. Unachoweza kubaini ni kuwa, katika hali zote hizi, yu akidadisi ama safarini kusaka jambo fulani. Katika safari yake hii anakutana na wahusika tofauti na wenye sifa za ajabuajabu. Wahusika hawa, wanaonekana kufurahi kumwona na wanabainisha kuwa yeye pekee ndiye waliyekuwa wakimsubiri muda wote na ndiye tegemeo lao. Yumkini yeye ndiye mkombozi wa pili. Hivyo, wanajiunga naye na safari inaendelea, ila fumbo linabaki, ukombozi gani anapaswa kuleta? Dhidi ya nini? Na, kwa vipi? Je, itakuwa lini? Hivi vinabaki kuwa ni vitendawili vya kifalsafa. Katika matukio yote haya, ambayo mengi hayasawiri moja kwa moja uhalisia wa duniani bali kuwa katikati ya kir...