NAGONA
![]() |
Nagona |
Nagona ni riwaya fupi ya kifalsafa na kibaadausasa inayoibua kira kuhusu falsafa na maana ya uhai, maisha, dhamira na hata kira yenyewe. Mhusika kiini wa novela hii anajikuta katika mazingira ya ajabuajabu katika nyakati tofauti tofauti. Si rahisi kubaini iwapo ni maono, njozi, kra ama matendo halisi, pengine ni vyote kwa pamoja.
Unachoweza kubaini ni kuwa, katika hali zote hizi, yu akidadisi ama safarini kusaka jambo fulani. Katika safari yake hii anakutana na wahusika tofauti na wenye sifa za ajabuajabu. Wahusika hawa, wanaonekana kufurahi kumwona na wanabainisha kuwa yeye pekee ndiye waliyekuwa wakimsubiri muda wote na ndiye tegemeo lao. Yumkini yeye ndiye mkombozi wa pili. Hivyo, wanajiunga naye na safari inaendelea, ila fumbo linabaki, ukombozi gani anapaswa kuleta? Dhidi ya nini? Na, kwa vipi? Je, itakuwa lini? Hivi vinabaki kuwa ni vitendawili vya kifalsafa. Katika matukio yote haya, ambayo mengi hayasawiri moja kwa moja uhalisia wa duniani bali kuwa katikati ya kira ama imani na uhalisi, muda unakwenda kwa kasi kubwa na inaonekana wazi kuwa ulimwengu upo katika changamoto za kiutawala, kifalsafa na hata kiimani. Katika mirengo yote hii, kinachotamalaki ni kukandamizwa kwa kira na dhamiri, kushamiri kwa uongo dhidi ya ukweli, kicho dhidi ya uwazi na hata giza dhidi ya mwanga. Kila lililozoeleka linaonekana kuwa kikwazo dhidi ya ukweli ama usahihi ambao hauonekani licha ya kuwa bayana. Hali hii imetamalaki kiasi cha kusababisha hofu, vifo, kutokiri na mikwamo katika mambo yote. Katika safari yake, mhusika kiini anakutana na wahusika waliowahi kufanya safari ya ukombozi ila wote wanakiri kuwa walikwamishwa na wanadamu na sasa mhusika kiini ndiye anayetarajiwa. Ili kuleta ukombozi, mkombozi mpya anapaswa kumbaini nagona, ambaye ingawa yu karibu naye siku zote, atafanikiwa kumshika endapo tu patatokea ajali katika bonde la taaluma, palipo chanzo cha madhila yote na chimbuko la mwangaza. Novela hii inatambuliwa kuwa pacha wa novela nyingine ya E. Kezilahabi ya Mzingile.
Credit : apenetwork
Comments
Post a Comment